Ungonoishaji ni kitendo cha kupata maana ambayo
inadhana ya ngono pindi mtu anapozungumza sentensi fulani.
Yafuatayo
ni maneno ya Kiswahili ambayo hungonoishwa na wazungumzaji wa lugha ya
kiswahili. Maneno haya tutayaainisha kwa kuyatungia sentensi na kufafanua utata
wa maana zake.
(i)
Sentensi hizo ni kama ifuatavyo;
1. Juma amemkata Asha jana.
Maana
ya msingi; Juma
ametumia kifaa chenye ncha kali kama vile sindano, kisu, panga na vinginevyo kumuweka
jeraha mwilini mwa Asha.
Maana
ngonoshi; Juma
amefanya mapenyi na Asha.
2. Yeye alimwambia rose “naomba tigo”
Maana
ya msingi; Alimuomba
Rose ampatie aidha vocha ya mtandao au kampuni ya mawasiliano ya tigo au laini
ya tigo
Maana
ngonoshi; Yeye
alimuomba Rose afanye naye mapenzi kinyume cha maumbile.
3. Nilipokuwa nasafiri kwa daladala kwenda
mbagala nilisikia mama mmoja akimwambia kondakta wa daladala “nitakupa ikisimama”.
Maana
ya msingi: Alimwambia
atatoa nauli endapo gari litakuwa limesimama kituoni.
Maana
ngonoshi; Hii
inamaana kwamba watafanya nae mapenzi endapo uume utakuwa imesimama.
4. Rafiki yangu aliniambia “atanipa mbele”.
Maana
ya msingi; Rafiki
yangu atanipa kitu fulani tulichoaidiana mbele ya safari tunapoelekea.
Maana
ngonoshi; Rafiki
yangu atanipa sehemu ya mbele yaani uke au uume wakati tukifanya mapenzi.
5. Naomba usinitie hapa tafadhali.
Maana
ya msingi; Anaomba
usimhusishe au usimjumuishe au kumuhusisha na tendo au tukio lolote.
Maana
ngonoshi; Anaomba
usifanye naye mapenzi katika eneo hilo labda kwa sababu lipo wazi sana au
halifai.
6. Raheli alimwambia Kanyamaishwa
kuwa “ndizi yake” ni kubwa kuliko ya Jabiri.
Maana
ya msingi; Tunda
aina ya ndizi alilokuwa nalo Kanyamaishwa
lilikuwa ni kubwa kuliko la Jabiri.
Maana
ngonoshi; Kanyamaishwa
ana uume mkubwa kuliko wa Jabiri.
7. Jamila ana shimo kubwa sana
Maana
ya msiingi; Jamila
ana sehemu kubwa aliyoichimba kwenda
chini kwa ajili ya kuweka vitu kama vile takataka.
Maana
ngonoshi; Jamila
ana uke mkubwa sana (mpana)
8. Amina alimwambia Jabiri kuwa “watafanya”.
Maana
ya msingi;
Wakikutana watatekeleza mambo fulani ya msingi waliyokuwa wameahidiana.
Maana
ngonoshi; Watakapo kutana hawatafanya mapenzi.
9. Pita amemchoma Meri
Maana
ya msingi; Pita
ametumia kitu chenye ncha kali kwa kumjeruhi meri kama vile sindano.
Maana
ngonoshi; Pita
amefanya mapenzi na Meri hadi akaridhika.
10. Asha alimwambia Deo “leo umenifikisha kileleni”.
Maana
ya msingi; Asha
ailmwambia Deo kuwa leo amekwea naye hadi mwishoni mwa kikomo au tamati ya mlima.
Maana
ngonoshi; Asha
alimwambia Deo kuwa leo amefanya nae mapenzi akaridhika.
11. Juma alimwambia Asha apanue aingize vizuri.
Maana
ya msingi; Juma
alimwambia Asha afungue vizuri kitu kama
mfuko au gunia ili aweke kitu fulani kwa uangalifu.
Maana
ngonoshi; Juma alimwambia
Asha atanue vizuri miguu ili sehemu zake za siri yaani uke uonekane vizuri ili
aingeze uume vizuri.
12. Jana shangazi alimwambia mjomba achomoe taratibu.
Maana
ya msingi; Shangazi
alimwambia mjomba atoe kitu fulani kilichokuwa kimeingizwa mahali fulana kama
vile msumari ukutani taratibu.
Maana
ngonoshi; Shangazi alimwambia mjomba utoe uume wake
taratibu kwenye uke wa shangazi.
13. Daaa!!!! Rafiki yangu anamtambo mkubwa sana.
Maana
ya msingi; Rafiki
nyangu ana mashine kubwa sana ya kurahisishia kazi kama vile jenereta na n.k.
Mmana
ngonoshi; Rafiki yangu ana uume mkubwa.
14. Jabiri amelala na Asha.
Maana
ya msingi; Jabiri
alipumzika pamoja na Asha kitandani au chini.
Maana
ngonoshi; Jabiri alifanya mapenzi na Asha.
15. Dada alimwambia kondakta “nikikaa vizuri nitakupa”.
Maana
ya msingi; Dada
atamwambia kondakta atampa nauli aliwa amekaa vizuri.
Maana ngonoshi; Dada atampa konda uke
akikaa vizuri.
16. Siku hizi bakari anatembea na dada yangu.
Maana
ya msingi; Bakari
anaongozana na dada yangu katika matembezi yao.
Maana
ngonoshi; Bakari
anamahusiano ya kimapenzi na dada yangu.
17. Musa ameacha kusimamisha siku hizi.
Maana
ya msingi; Musa
ameacha tabia yake ya kuzuia kitu fulani kama vile gari, pikipiki au baisikeli visiendelee
na safari.
Maana
ngonoshi; Musa,
uume wake haufanyi kazi kama mwanaume kamili.
18. Yeye amemwagia Dada mbegu kichwani.
Maana
ya msingi; Ina maana
yeye alimmwagia nafaka kama vile mahindi, maharage na kadhalika kichwani.
Maana
ngonoshi ; Yeye alimmwagia
manii/ shahawa kichwani.
19. Alinitaka
sana mara ya kwanza nikakataa lakini
mara ya pili nilikuballi.
Maana
ya msingi; Kunihitaji
tushirikiane naye sana katika kufanikisha jambo au mabo fulani aliyokuwa nayo
mfano kazi.
Maana
ngonoshi; Kumwomba
awe na uhusiano wa kimapenzi naye.
20. Jana nilikunwa vizuri sana kuliko siku zote.
Maana
ya msingi; Jana
alinikwangua kwangua au kunisugua sugua kwa kutumia kitu kama kucha au kijiti
kuliko siku zote.
Maana
ngonosho; Jana
alinidhisha kimapenzi kuliko siku zote.
21. Halima hatamwacha Munisi kwa sababu alimsugua vizuri.
Maana
ya msingi; Munisi
alimkuna / alimsugua vizuri alipokuwa anawashwa.
Maana
ngonoshi; Halima alifanya naye mapenzi hadi aridhike.
22. Hapo mwanzo alitulia sana siku hizi anagawa
sana.
Maana
ya msingi; Alikuwa
hatoi vitu kama vile msaada kwa watu.
Maaana
ngonoshi; Alikuwa
hajihusishi na masuala ya mapenzi lakini kipindi hiki anafanya sana mapenzi kwa
kila mtu.
23. Pale nimepita lakini sijafurahi kabisa.
Maana
ya msingi; Kuendelea
na safari kwa kupitia njia ile ile lakini hufurahii safari.
Maana
ngonoshi; Kufanya
mapenzi na mtu fulani bila kupata raha yoyote.
24. Juma ndie aliyewabandua wale wasichana wawili.
Maana
ya msingi; Kutoa
mabango au vipeperushi vya wasichana wawili vilivyokuwa vimewekwa sehemu fulani
kama kwenye mbao za matangazo.
Maana
ngonoshi; Juma
ndiye aliyewatoa bikira wasichana wale wawili.
25. Alipotoka pale alikuwa tayari kaloana.
Maana
ya msingi; Nguo
alizokuwa amevaa zilikuwa na majimaji.
Maana
ngonoshi; Alipotoka
pale nguo zake zilikuwa zimeloa shahawa.
26. Juma hajui kulenga mpaka aongozwe.
Maana
ya msingi; Hana
shabaha hadi aongozwe .
Maana
ngonoshi; Juma
hawezi kuingiza uume wake kwenye uke hadi aongozwe.
27. Ingawa ya kwangu ni nyembamba lakini ya
kwake ni nene zaidi.
Maana
ya msingi; Maneno “ya
kwake” na “ya kwangu” yanarejelea
nomino yoyote iliyomo katiaka ngeli ya mofolojia ya nomino. Kwa mfano simu,
nyumba, chupa na n.k.
Maana
ngonoshi; Maneno “ya kwangu” na “ya kwake” huweza kurejelea na kumaanisha sehemu za siri za mwanamke
au mwnaume. (uke na uume)
28. Leo nina hamu sana kwasababu nimemkosa siku nyingi.
Maana
ya msingi; Nina
shauku ya kumuona kwa sababu sijamuona siku nyingi.
Maaana
ngonoshi; Nina
nyege naye za kufanya naye mapenzi kwa sababu sijafanya naye siku nyingi.
29. Joni hupenda sana kuzama chumvini.
Maana
ya msingi; Joni
anapenda kuingia sehemu yenye majimaji yenye asili ya chumvi.
Maana
ngonoshi; Joni
anapenda sana kunyonya au kulamba sehemu za siri za mwanamke yaani uke.
30. Ingawa alinishughulikia vizuri sikuridhika.
Maana
ya msingi; Ingaw
alifanya haraka katika kufanikisha jambo fulani / kujitahidi kufanikisha jambo
fulani.
Maana ngonoshi; Ingawa alinipa mapenzi
vizuri lakini sikiridhika
31. Ingawa anamtaimbo mkubwa hawezi kuutumia
Maana ya msingi; Ingawa ana fimbo kubwa
ya chuma ya kuvunjia miamba hawezi kuitumia.
Maana
ngonoshi; Ana uume
mkubwa lakini hawezi kuutumia.
32. Japokuwa amenichokonoa hakufanikiwa.
Maana
ya msingi; Japokuwa
alinidadisi kwa kuniuliza maswali lakini hakifanikiwakupata majibu
aliyoyahitaji.
Maana
ngonoshi; Aliingiza
uume au kidole kwenye uke bila kutimiza haja ya mwanamke.
33. Jana alinikaza kuliko siku zote.
Maana
ya msingi; Jana alinifanyia uimara kuliko siku zote
Maana
ngonoshi; Alinifanyia mapenzi mazuri kuliko siko zote
34. Ingawa alimpa kidogo ila alikojoa sana.
Maana
ya msingi; Ingawa alipata kinywaji kidogo alienda haja
ndogo mara nyingi.
Maana
ngonoshi; Alitumia sehemu za siri (uke au uume) kidogo
lakini alitoa shahawa nyingi.
35. Aise! Siku hizi huoni mtu anayefyeka ovyo ovyo.
Maana
ya msingi; Siku hizi
huoni mtu anayejua kukata miti au majani
ili yawe mafupi ovyo ovyo.
Maana
ngonoshi; Siku hizi
huwezi kuona mtu akifanya mapenzi na kila msichana bila kuchagua.
36. Yeye ananimegea vizuri kuliko wewe.
Maana
ya msingi; Yeye ananivunjia
kitu au kunikatia kitu kinacholiwa vizuri kuliko wewe.
Maana
ngonoshi; Yeye
alinipa mapenzi mazuri yasiyokuwa na choyo kuliko wewe.
37. Kutokana na tundu lako dogo nilishindwa kutimiza haja yangu.
Maana
ya msingi; Kutokana
na uwazi mdogo mfano tundu la choo nilishindwa kutimiza haja yangu.
Maana
ngonoshi; Kutokana
na uke wako mdogo nilishindwa kufanya mapenzi vizuri nikatimiza haja yangu.
38. Juma hupenda kunyonya maziwa kila siku kabla hajalala.
Maana
ya msingi; Juma
hupenda kunywa maziwa yaliyosindikwa katika pakiti au mifuko.
Maana
ngonoshi; Juma hupenda
kunyonya matiti kila siku usiku.
39. Jana yeye alimtafuna kutwa nzima.
Maana
ya msingi; Jana
alisaga kwa meno kitu fulani kutwa nzima.
Maana ngonoshi; Jana alifanya nae
mapenzi siku nzima.
40. Juma alipochomoa nilihisi maumivu makali.
Maana
ya msingi; Juma alipotoa
kitu kama sindano matakoni mwangu nilipata maumivu makali.
Maana
ngonoshi; Juma alipochomoa
uume kwenye uke nilihisi maumivu.
41. Mama alimwambia dada kuwa “usafi unaanzia chini”.
Maana
ya msingi; Mama alimwambia dada usafi huanzia
sehemu ya kawaida kabisa tenga katika ngazi ya
chini.
Maana
ngonoshi; Mama
alimwambia dada kuwa usafi unaanzia sehemu za siri yaani uke au uume.
42. Ikiingia huwa ninasinzia.
Maana
ya msingi; Ikipenya
kuingia ndani kitu kama sindano ya usingizi huwa ninasinzia.
Maana
ngonoshi; Kila uume
uingiapo ndani ya uke wangu huwa ninasinzia
43. Alipoiweka ilizama yote.
Maana
ya msingi; Baada ya
kuingia au kuzama ndani ya kitu kama vile kimiminika ilizama yote.
Maana
ngonoshi; Uume
ulipoingia ndani ya uke ilizama yote.
44. Kila nikifikia katikati huwa nndio ninapata utamu.
Maana
ya msingi; Kila
nikifika katikati ndio nanogawa kwa kitu au jambo.
Maana
ngonoshi; Kila
nikiingiza kwenye uke (katikati) ndio napata utamu.
45. Wewe unapenda nyeti.
Maana
ya msingi; Wewe unapenda
kudeka
Maana
ngonoshi. Wewe unapenda
sehemu za siri ( uke au uume)
46. Mchi wake
unatwanga vizuri.
Maaana
ya msingi. Kifaa chake
cha kutwangia vitu kama nafaka na madawa
kwenye kinu unatwanga vizuri.
Maana
ngonoshi; Uume wake
unaweza kufanya mapenzi vizuri.
47. Akina mama huko mbele mtanipa. (aliuliza mgombea). Na akina baba je huko
nyuma mtanipa.
Maana
ya msingi; Akina
mama mliokaa mbele na akina baba mliokaa nyuma mtanipia kura.
Maana
ngonoshi; Neno “mbele” na “nyuma” yana maana sehemu za siri yaana “mbele” ni “uke” na “nyuma” ni “mkundu”.
48. Sina
hamu kabisa na yule kaka maana kitendo alichonifanyia huko nyuma sitakisahau kabisa.
Maana ya msingi: Sina hamu kabisa na yule kaka, kwani kuni jambo alilonifanyi hapo zamani sitalisahau
kabisa.
Maana ngonoshi: Sina hamu kabisa na yule kaka maana
kitendo alichonifanyia kwenye matako/ mkundu sitakisahau.
49. Jamaa wa lori alilazimishia mpaka
akafanikisha kumchomekea kwa mbele
yule dada aliyekuwa anaendesha gari aina ya Prado.
Maana
ya msingi: Jamaa wa lori
alilazimisha mpaka akafanikisha kutanguliza gari lake aina ya lori katika nafasi ya mbele ya gari la yule dada mwenye Prado.
Maana ngonoshi: Jamaa wa lori alilazimisha mpaka
akafanikisha kuingiza uume wake katika
uke wa dada yule mwenye Prado.
50. Dada
mwenye pikipiki alimwambia yule
kijana yule pale sheli, “ingiza vizuri
pipe yako usije ukamwaga nje”.
Maana
ya msingi: Dada mwenye
pikipiki alimwambia yule kijana pale sheli, “weka mpaka ndani bomba la
mafuta usije ukamwaga mafuta nje.
Maana ngonoshi: Dada mwenye pikipiki alimwambia yule
kijana pale sheli,
“ingiza uume wako mpaka ndani usije akamwaga
shahawa nje”.
Kutokana na data ya kwanya kategoria
zinazongonoishwa zaidi ni pamoja na;
·
Vitenzi.
Kwa mfano choma, liwa , ingiza, chomoa ,liwa, tia, tiwa.
·
Nomino.
Kwa mfano shimo, tundu, mtaimbo, mchi.
·
Vivumishi.
Kwa mfano, yake nene, pana.
·
Vihusishi.
Kwa mfano, ya kwake, ya Asha
Kategoria
zinazongonoishwa zaidi ni vitenzi kwa sababu ndio msingi na muhimili wa
sentensi. Vile vile ndio msingi unaobeba utendaji katika tungo.
Kategoria
ambazo haziwezi kungonoshwa ni viunganishi na vielezi.
Wanaopenda kungoisha zaidi ni;
Wazungumzaji
wa Kiswahili hupenda sana kunganosha maneno kwa sababu hufikiria zaidi ya maana
ya msingi ya neno husika kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia na
kusababisha dhana ya ngono kukaa akilini mwa watu hasa vijana.
Kati ya msemaji na msikilizaji
anayengonosha maneno yanayosemwa ni msikilizaji kwani yeye ndiye mlengwa na mfasiri wa
dhana inayosemwa. Yeye ndiye anayetafuta maana ya lile lisemwalo na Hakuna ruwaza maalumu na dhabiti ya
ungonoishaji.
Kundi la watu wanaongonoisha zaidi ni
kundi la vijana
kwa misingi ya rika kwa sababu rika hili huwa na mawazo yalivofungamana zaidi
na mambo ya ngono.
Anayeelewa maana ngonoshi za maneno ya
Kiswahili ni wazungumzaji
na watu waliofungamana na maana hizo za ngono. Wasioelewa maana ya ngonoshi ni
wale ambao wapo nje ya muktadha na rika
hilo la vijana. Mfano baadhi ya wazee.
Katika taaluma ya isimu ungonoshi una
mchango kama ufuatao;
·
Huonyesha
uhusiano wa maana za maneno. Kwa mfano unaweza kujua ni neno lipi lina maana ya
msingi na lipi lina maana ngonoshi.
·
Husidia
katika kuonyesha ukubalifu wa maana za maneno kulingana na matumizi. Yaani neno
linapata maana kutokana na jinsi linavyotumika, watumiaji wenyewe katika
mzingira fulani.
·
Hutusaidia
kupata maana za ziada. Kwa mfano neno “mbele”
inaweza kuwa na maana ya “kutangulia” na maana ya ziada ikawa
ni “sehemu za siri” yaani uke au uume.
Athari za ungonoishaji ni pamoja na;
· Kwanza athari ni kupotosha maana ya
msingi. Kwa mfano msemaji alikusudia kuomba kura kwa kusema “kina mama hapo mbele mtanipa” kama
kuwauliza wanaompiga kura lakini wao wakapata maana potofu ya kuwaomba sehemu
za siri yaani uke
· Pili ni kuongeza uziada dufu katika
lugha. Ungonoishaji huaongeza maana ya ziada katika neno. Maana isiyo ya msingi
katika neno.
· Tatu ni kuleta utata katika tungo. Kwa
mfano “ikiingia huwa nafumba macho”.
Mtu anaweza kujiuliza nini inayoingia.
· Pia huibua mgogoro katika jamii. Kwa
mfano msemajia anapomwambia msikilizaji (kwa mfano wa kike) ambaye hana mzoea
naye utungo kama “unashimo kubwa”,
kauli hii yaweza kuleta malumbano baina ya msemaji na msikilizaji.
· Hupelekea uzalilishaji wa kijinsia.
MTAZAMO WANGU;
Ungonoishaji wa maneno ya Kiswahili ni jambo
jipya lililoibuka ingawa maneno yanayotumika yalikuwepo. Kimsingi maneno haya
yalizingatia maana za msingi za maneno husika. lakini kutokana na maendeleo ya
sayansi na tekinolojia pamoja na utandawazi maneno haya yameanza kupewa maana
ya ziada inayofungamana na ngono yaani ungonoishaji. Na hii hutokana na mawazo
ya watumiaji kufungamana na ngono.
USHAURI WANGU;
Suala
la ungonoishaji ni suala la kukemewa na kubezwa kwani linapotosha maadili na
uwezo wa kukamilisha mawasiliano na lengo lililokusudiwa. Kwa mfano kama mtu
anafundisha anaweza kujikuta anachekwa baada ya kutumia neno liloibua dhana ya
ungonoishi kwa wanafunzi au wasikilizaji. Hivyo suala hili likiendelezwa mwisho
wake maana ya msingi imefifizwa na wanatumia maana ungongoshi tu.
Marejeo.
TUKI, (2004), Kamusi ya Kiswahi Sanifu. Oxford University Press: Nairobi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni