Fasihi






MGAWANYO WA TANZU NA VIPERA VYA FASIHI SIMULIZI.

 M.M Mulokozi(1989)


Katika makala hii tunaanza na kuelezea maana ya fasihi, fasihi fasihi simulizi kwa kutumia wataalam mbalimbali, baada ya kuelewa vizuri dhana hizi tutajadili vigezo vilivyotumika katika mgawanyo wa tanzu na vipera vya fasihi simulizi katika makala ya M.M Mulokozi (1989) na hatimaye tutaangalia ubora na udhaifu wa uainishaji wa tanzu hizo, na kumalizia na hitimisho, kielelezo na mwisho marejeo.
Fasihi ni sanaa itumiayo lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii bila kujali kuwa imeandikwa au haijaandikwa. Fasihi ambayo haijaandikwa ni fasihi simulizi na fasihi iliyoandikwa ni fasihi andishi.
Ama kuhusu Fasihi simulizi, Wamitila ( 2002) anaeleza kuwa Fasihi simulizi ni fasihi ambayo huwasilishwa kwa njia ya mdomo kwa kusimuliwa, kuimbwa , kutongolewa au kughanwa.
Naye Mulokozi (1996) anaelezea kuwa fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya mdomo na vitendo bila maandalizi.
Kwa ujumla fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya masimulizi  ya mdomo na vitendo bila maandishi.
Katika makala ya M.M Mlokozi (1989) katika mulika ya 21 amejaribu kuzigawa tanzu za fasihi simulizi ya Tanzania katika tanzu zake mahususi kwa kuzingatia VIGEZO vifuatavyo;
Umbile na tabia ya kazi inayohusika;upande wa umbile na tabia ya kazi ya sanaa ameangalia vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa mwelekeo au mwenendo ilionao.Vipengele hivyo ni namna lugha inavyotumika(kishairi,kinathali,kimafumbo,kiwimbo, kighani nakadharika) pia muundo wa fani hiyo na wahusika kama wapo.
Kigezo cha pili ni muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira (hili linazingatia pia dhima yake kijamii) hapa Mulokozi amezingatia ukweli wa msingi kuwa fasihi simulizi ni sanaa inayo pita, isiyofungwa katika umbo maalum, wala matini maalum yasiyo badilika. Fasihi simulizi inatawaliwa na vitu muhimu vitatu yaani watu, wakati na mahali. Mwingiliano huu ndio muktadha, na muktadha ndio unaamua fani fulani ya fasihi simulizi ichukue umbo lipi? Iwasilishe vipi kwa hadhira, kwenye wakati na mahali hapo.

Zifuatazo ni tanzu na vipera vya fasihi simulizi kama zilivyoainishwa na M.M.Mlokozi(1989) katika mulika 21 na jinsi alivyo ziainisha kwa kutumia vigezo hivi viwili, yaani kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishwaji kwa hadhira, na vipera vyake.
M.M.Mulokozi ameainisha tanzu sita ambazo ni; mazungumzo, masimulizi, maigizo (drama) ushairi semi na ngomezi (ngoma). Hivyo ufuatao ni uainishaji wa tanzu hizi za fasihi simulizi na vipera vyake kwa kutumia vigezo vya Mulokozi katika mulika ya 21.
Mazungumzo, ni maongezi au maelezo ya mdomo katika lugha ya kawaida, juu ya jambo lolote lile. Si kila mazungumzo ni fasihi mazungumzo ili yawe fasihi lazima yawe na usanii wa aina fulani, na uhalisia baada ya kuunakili.
Tanzu zinazoingia katika fungu la mazungumzo; Hotuba, Malumbano ya watani, Ulumbu, Soga na mawaidha. Katika kuainisha tanzu hizi ndani ya mazungumzo M.M.  Mulokozi ametumia vigezo vyote viwili; Hotuba, malumbano ya watani, ulumbu, soga na mawaidha. Kwa kuzingatia kigezo cha kwanza kinachozingatia msingi wa umbile na kazi inayohusika, tunaona tanzu hizi zote zina vipengele vya vinvyoumba sanaa na kuipa muelekeo au mwenendo ulionao, katika hotuba, malumbano ya watani, ulumbu, soga na mawaidha vyote vinavipegele vyake. Pia tanzu hizo zote zina maana ya lugha inayotumika. Mfano katika hotuba lugha rasmi ndiyo inayotumika, katika malumbano ya watani lugha ya kejeli mara nyingi ndio hutumika zaidi, mawaidha hutumia lugha rasmi au lugha za kikabila hutumika.
Pia katika kigezo umbile na tabia ya kazi inayohusika,katika kuainisha tanzu hizi mulokozi ametumia muundo wa fani na wahusika kama wapo.Tanzu zote hizo katika mazungumzo zina fani yake. Mfano katika malumbano ya watani ni tanzu inayozingatia fani zifuatazo; Kuna utani wa mababu, mabibi na wajukuu, utani wa mashemeji, utani wa kikabila na utanu wa marafiki. Kila kimojawapo kati ya fani hazi huwa na kanuni zake, miktadha yake na mipaka yake katika jamii zinazohusika.
Pia katika kuanisha tanzu za mazungumzo Mulokozi ametumia kigezo chake cha pili yaani kigezo kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira hili linazingatia pia dhima yake katika jamii kama ifuatavyo;

Ndani ya mazungumzo kuna hotuba, mawaidha, ulumbu, malumbano ya watani, soga; Tanzu hizi zote zinazingatia msingi wa fasihi kuwa ni sanaa inayopita, isiyofungiwa katika umbo maalum, wala matini yasiyobadilika. Mfano Hotuba ni sanaa inayopita, isiyofungwa katika umbo maaluma na matini yake hubadilika kulingana na matukio kama vile; matukio ya kidini, sherehe na kadharika. Hotuba hufuata wakati, watu na mahali. Katika kigezo hiki kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira huzingatia wakati, watu na mahali.Tunaona katika mazungumzo na tanzu zake zinazingatia wakati watu na mahali, mfano mawaidha huzingatia watu gani,wana umri gani, je ni vijana wa kiume au wa kike. Pia huzingatia mahali yaani tukio linapofanyika, mfano sebuleani au chumbani na pia wakati gani asubuhi, mchana au jioni.
Tanzu ya mazungumzo kwa ujumla imeainishwa kwa kutumia vigezo vyote viwili yaani kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira.
Masimulizi; ni fasihi yenye kusimulia habari  fulani.  Mulokozi (1989) anasema kuwa masimulizi ni fasihi ya kihadithi na fani zake huwa na sifa zifuatazo; hueleza atukio katika mpangilio fulani mahsusi, huwa na wahusika yaani watendaji au watendwaji katika matukio yanayosimulia, hutumia lugha ya kimaelezo, utambaji wake au utoaji wake huweza kuambatana na vitendo au ishara, na huwa na maudhui ya kweli au ya kubuni na yenye mafunzo fulani katika jamii.

Katika mulika 21 Mulokozi amegawanya masimulizi katika tanzu zifuatazo; za kihadithi na Tanzu za Kisalua.
Katika tanzu za kihadithi amezigawa katika makundi yafuatayo;
Ngano  ni hadithi za kimapokeo zitumizo wahusika kama wanyama,miti na watu kuelezea au kuonya kuhusu maisha.Utanzu huu unajumuisha fani kadhaa kama vile; istiara,mbazi,na kisa.
Tanzu za kisalua zimegawanywa katika fani zifuatazo; visakale, tarihi, visasili,. Hivyo tunaona kuwa katika uainishaji wa tanzu hii ya masimulizi mulokozi ametumia vigezo vyote viwili kama ifuatavyo; katika msingi wa umbile na tabia ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa mwenendo ulionao. Na vipengele hivyo ni kama; lugha ya kimaelezo, maudhui, matukio na wahusika.Pia ameonyesha namna lugha inavyotumika mfano. Ngano hutumia lugha ya kimaelezo na visakale, mapisi, tarihi, kumbukumbu na visasili. Vipera hivi vyote hutumia lugha ya kimaelezo.
Pia katika msingi wa umbile na kazi inayohusika, kigezo hiki huzingatia muundo wa fani na wahusika kama wapo.Tanzu ya masimulizi ina fani zifuatazo kutokana na Mulokozi. Hueleza matukio katika mpangilio fulani mahususi, huwa na wahusika yaani watendaji au watendwaji katika matukio yanayosimuliwa, utambaji au utoaji wake huweza kuambatana na vitendo au ishara, huwa na maudhui ya kweli au ya kubuni na yenye mafunzo fulani na hutumia lugha ya kimaelezo.   
Semi ni tungo au kauli fupifupi zenye kubeba maana fulani au mafunzo muhimu katika jamii, Mulokozi ameaimisha tanzu za semi kama ifuatavyo:-
Methali ni semi fupi fupi zenye kueleza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na uzoefu wa jamii. Methali huwa na sehemu mbili kwanza sehemu ambayo huanzisha wazo fulani sehemu ya pili ambayo hulikanusha au kulikamilisha wazo hilo. Methali ni utanzu tegemezi ambao kutokea kwake hutegemea fani nyingine mfano maongezi, majadiliano mazito, muktadha maalum katika methali Mulokozi ameainisha tanzu hii kwa kutumia kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika, katika kigezo hiki Mulokozi ameonyesha matumizi ya lugha. Mfano methali hutumia tamathali, sitiari na mafumbo. Pia methali huwa na wahusika wa fani zake zinazojitegemea. Mfano Haraka haraka / Haina Baraka. Wahusika kuna anayeuliza Haraka haraka na anayejibu Haina Baraka. Pia lugha aliyotumia katika methali hii ni lugha ya kinathari na kishairi.

Pia methali huwa na fani zake. Mulokozi anasema methali ni utanzu tegemezi ambao kutokea kwake hutegemea fani nyingine, fani hizo ni maongezi au majadiliano mazito, muktadha maalumu, huwa na sehemu mbili sehemu ya kwanza ambayo huanzisha wazo fulani na sehemu ya pili ambayo hulikamilisha au kukanusha wazo hilo.
Ndani ya kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishaji methali huwa na dhima ya kutoa mafunzo, kuadibisha, kuonya na kuhamasisha jamii. Methali huendana na wakati, watu na mahali kwa kuzingatia tukio pia huwa na matini yanayobadilika. Mfano Haraka haraka haina Baraka, methali hii inatoa onyo kuwa ukifanya jambo kwa haraka unaweza kukosea, hivyo polepole ndio mwendo.
Vitendawili; hizi ni usemi uliofumbwa ambao hutolewa kwa hadhira ili waifumbue. Fumbo hilo kwa kawaida huwa linafahamika katika jamii hiyo na mara nyingi lina mafunzo muhimu kwa washiriki mbali na kuwachemsha akili zao.  Vitendawili hutegemea uwezo wa kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina mbalimbali vilivyomo katika maumbile, ni sanaa inayojitegemea, inayotendwa na ina jisimamia yenyewe.
Katika kigezo cha umbile na tabia inayohusika vitendawili hutumia lugha ya mafumbo na huwa na washiriki yaani wahusika ambao ni yule anayetoa kitendawili na anayejibu. Mfano  Mmoja huuliza Kitenawili na mwingine anajibu tega. Mfano; Kaa huku na mimi ni kae kule tumfinye mchawi (kula ugali), Mfano huu huhamasisha ushirikiano baina ya watu.
Pia vitendawili huwa na fani kama wahusika (pande mbili) wanaouliza na wanaojibu, muktadha maalumu (mazingira) katika muktadha na namna ya uwasilishaji Mulokozi amesema vitendawili huwa na mafunzo fulani zaidi ya chemsha bongo. Vitendawili huzingatia mazingira (mahali) watu na wakati maalum mfano watoto, mahali (shuleni au nyumbani) na huwa na wakati maalum.
Misimu, ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Msimu ukipata mashiko ya kutosha katika jamii hatimaye huingia katika kundi la methali za jamii hiyo. Mfano  Tamu tamu mahonda ukinila utakonda.

Katika kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira misimu ni sanaa inayopita isiyofungiwa katika umbo maalum wala matini maalum yasiyobadilika. Misimu ina dhima ya kutoa mafunzo, kuonya, hutumika katika siasa pia misimu huenda na wakati, watu na mahali. Mfano Matteru (1987) anasema ‘tamu tamu mahonda ukinila utakonda’ . Katika  mfano huu unaonyesha madhara ya pombe iliyokuwa inatengenezwa na kiwanda cha mahonda (Zanzibar). Katika kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika misimu hutumia lugha isiyosanifu kwani huzuka na kutoweka mfano; mdebwedo, utajiju, yeboyebo,  buzi na kimeo.
Mafumbo ni semi za maonyo au mawaidha ambazo maana zake ni za ndani na zimefichika. Fumbo hubuniwa na msemaji kwa shabaha na hadhira maalum hivyo ni tofauti na methali ambazo ni semi za kimapokeo. Katika kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishwaji mafumbo huwa na dhima ya kutoa maonyo na mawaidha kwa jamii kwani hubuniwa kwa hadhira maalum. Mfano  Mbele ya bata kuna bata na nyuma ya bata kuna bata, jumla nina bata wangapi’?  Fumbo hili huonyesha umakini katika katika kufanya kitu. Katika mafumbo ndani ya kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohisika huangalia namna lugha inavyotumika, katika mafumbo ambayo maana yake ya ndani imefichika mafumbo huundwa na wahusika na fani yake. Mfano yule anayetoa fumbo (anasema fumbo mfumbie mjinga ) Yule anayejibu (mwerevu ataling’amua) hapa anamainisha mjinga hawezi akalifumbua fumbo ila mwerevu hulifumbua pia mjinga anaweza akadanganywa ila mwerevu hawezi kudanganywa. Fumbo hili linahamasisha mtu afanye juhudi katika mambo ili afanikiwe kama mwerevu.
Lakabu ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa au kujipatia kutokana na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia au kimatendo. Majina haya huwa ni sitiari. Majina haya huweza kumsifia mtu au kumkosoa. Mfano Mkuki uwakao – Jomo Kenyatta, Sakarani – mlevi, Simba wa yuda – Haile sellasie.
Katika kigezo cha umbile na tabia inayohusika Mulokozi ameonyesha lakabu hutumia maneno yenye maana iliyofungwa na sitiari, pia lakabu huwa na wahusika yule anayepewa sifa. Mfano mkuki uwakao – Jomo Kenyatta na anayetoa sifa.
Katika muktadha na namna ya uwasilishaji lakabu huwa na dhima mbalimbali kama kusifia, mfano baba wa taifa, inatoa sifa ya utendaji bora wa kazi, simba wa yuda inaonyesha mshupavu. Mkuki uwakao inaonyesha kiongozi  mchapa kazi. Pia lakabu hukosoa na kuonya mfano sakarani- ulevi hapa inaonyesha kuwa mtu mlevi hafai katika jamii. Lakabu huwa na matini yanayobadilika, hivyo ni sanaa inayopita, lakabu hufuata watu wakati na mahali.
Ushairi, ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo mashairi na tenzi. Zaidi ya kuw na vina ushairi una ufasaha wa kuwa na maneno machache au muhtasari mawazo na maono ya ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu. Mulokozi (1989) anasema ushairi hupambanuliwa na lugha ya kawaida kwa kutumia lugha na mbinu za kimuktadha. Kauli za kishairi hupangwa kwa kufuata wizani maalumu na mawimbi ya sauti na mara nyingi lugha ya mkato na mafumbo hutumika ushairi una fani zinazoambatana na muziki wa ala na wakati mwingine hupata wizani wake kutokana na mapigo ya muziki huo wa ala. Mulokozi (1989) amegawa ushairi katika mafungu mawili ambayo ni nyimbo na uwasilishaji.
Nyimbo ni kila kinachoimbwa hivyo hii ni dhana panainayojumuisha tanzu nyingi za kinathari kama vile hadithi huweza katika kundi la nyimbo pindi zinapoimbwa . Vipera  vya nyimbo ni tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, tenzi, tendi, mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa, nyimbo za watoto na nyimbo za kazi.
Katika kuainisha tanzu hiii ya nyimbo Mulokozi  ametumia vigezo vyote viwili, tukianza na kigezo cha kwanza ambacho ni umbile na tabia ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha jinsi vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa mwelekeo. Vipengele vilivyo katika nyimbo ni namna lugha inavyotumika .
Mfano: nyimbo za maombolezo hutumia lugha za maombolezo yenye maneno ya  Kufariji  tofauti na nyimbo za sherehe huwa na lugha ya furaha na  kuchangamsha.
Katika kigezo hiki pia cha umbile na tabia ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha muundo wa fani na wahusika katika nyimbo.  Mfano: mambo muhimu yanayotambulisha nyimbo ( fani ya nyimbo) Muziki wa sauti ya muimbaji au waimbaji( wahusika), Muziki wa ala (kama ipo), Matini au maneno yanayoimbwa,Hadhira inayoimbiwa,Muktadha unaofungamana na wimbo huo mfano sherehe, ibada na kilio.
Pia Mulokozi katika kuainisha tanzu ya nyimbo ametumia kigezo cha pili yaani muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira katika kuainisha tanzu hii ya nyimbo amezingatia wakati, watu (wahusika) na mahali. Pia nyimbo ina matini yanayobadilika, yasiyofungiwa katika umbo maalumu yaani ni sanaa inayopita.
Mfano: kuna nyimbo zinazoimbwa kwa kufuata wakati wake, mahali mahususi, na mahali maalumu, mfano wawe na vave hizi ni nyimbo za kilimo, mbolezi hizi ni nyimbo za kilio au maombolezi. Mbolezi huimbwa wakati maalumu, na waombolezaji ambao ni watu( wahusika) na mahali maalumu (mfano msibani)
Maghani ni ushairi unaotolewa kwa kalima badala ya kuimbwa. Zipo maghani za aina mbili, kuna maghani ya kawaida, ambayo huundwa na fani mbalimbali za ushairi simulizi mfano mapenzi, siasa, maombolezo, kazi za dini na kadhalika. Maghani ya masimulizi hutambwa ili kusimulia hadithi, historia au matukio fulani ambayo huambatana na nyimbo. Tanzu za maghani ni sifo, vivugo, tondozi, rara, ngano na tendi.
 Maghani ni tanzu iliyoanishwa kwa kutumia kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira. Molokozi ameonyesha maghani huwasilishwa kwa kalima badala ya kuimba, pia dhima za maghani ni kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa kuzingatia matukio
Mfano uhuru  kesi za mauaji
Mulokozi anasema maghani huundwa na fani mbalimbali za ushairi simulizi mfano mapenzi, siasa, maombolezo, kazi na dini. Zifuatazo ni fani za ushairi simulizi ambazo ni, Masimulizi hutolewa kishairi, huhusu matukio muhimu ya kihistoria au jamii, huelezea habari za ushujaa na mashujaa, huwasilishwa kwa kughanwa (ala ya muziki), hutungwa papo kwa papo.
Pia maghani huwa na wahusika, na huambatana na muziki wa ala. Mulokozi anasema mutambaji wa ghani hizi huitwa Yeli au Manju na kwa kawaida huwa ni bingwa wa kupiga ala fulani ya muziki (mtambaji huyu ndiye mhusika mkuu)
Maigizo, (drama) ni sanaa inayotumia watendaji kuiga tabia au matendo ya watu na viumbe wengine ili kiburudisha na kutoa ujumbe fulani. Maigizo ni sanaa inayopatikana katika makabila mengi. Mulokozi anasema drama (maigizo) ya kiafrika huambatana na ngoma mtambaji wa hadithi au matendo ya kimila. Kwa  mfano jando na unyago , yapo maigizo yanayofungana na michezo ya watoto, uwindaji , kilimo, na kadhalika. Drama hutumia maleba maalumu kama vizuizui (mask).
Katika kuainisha tanzu hii mulokozi ametumia vigezo viwili,kwa kuanza na kigezo cha kwanza Mlokozi ameainisha,mambo na vipengele vinavyopatikana ndani ya maigizo ambavyo ni maigizo yanayohusu matendo ya kimilana michezo ya watoto,matanga, uwindaji, kilimo na nyinginezo.
Kwa msingi wa umbile na tabia inyohusika vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa muelekeo tanzu hii ya maigizo ni lugha inavyotumika katika kuigiza fani na wahusika mfano wahusika wa maigizo wapo na hawa ndio watendaji wakuu katika kufikisha ujumbe. Maigizo hutumia lugha mfano lugha ya kejeli na hata lugha rasmi pia maigizo huwa na fani inayotendwa.
Mulokozi Pia katika kuainisha tanzu hii ya maigizo ametumia kigezo cha pili kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira, maigizo ni sanaa inayopita isiyofungiwa kaika umbo maalum wala matini yasiyobadilika ila maigizo hubadilika kutokana na tukio linaloigigwa na kuzingatia wakati, watu na mahali mfano maigizo huhitaji sehemu maalumu (jukwaa au uwanja wa kutendea) , wahusika ambao ndio waigizaji wakuu na pia maigizo huenda na wakati.
Ngomezi ni midundo Fulani ya ngoma kuwakilisha kauli Fulani katika lugha ya kabila hilo. Mara nyingi kauli hizo huwa ni za kishairi au kimafumbo
Mulokozi ametumia vigezo vyote viwili katika kuainisha tanzu hii, kwa kuanza na umbile na tabia ya kazi inayohusika ameangalia vipengele ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa mielekeo na mienendo ulionao.Vipengele hivyo ni namna lugha inayotumika, kishairi, kinathari, kimafumbo, kiwimbo au kighani. Mfano, katika ngomezi hutumia lugha na kauli za kishairi au kimafumbo.
Pia kigezo hiki huangalia fani na wahusika kama wapo, katika ngomezi huwa na wahusika ambao hupiga na kuandaa ngoma hizo.hii hujionyesha katika  utofauti wa upigaji wa ngoma hizi kutokana lengo lake  ambapo inaweza kutoa taarifa, tahadhari au ngomezi za uhusiano.
Katika kigezo cha pili muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira Mulokozi ameonyesha jinsi ngomezi ilivyo ni sanaa ambayo huandaliwa kwa matukio maalum. Pia ngomezi hutawaliwa na vitu vitatu muhimu katika kigezo hiki ambavyo ni watu, wakati na mahali.
M.M Mulokozi katika mulika amejitahidi kuelezea na kuzigawa tanzu na vipera vya fasihi simulizi kwa kuzingatia vigezo vyote viwili, yaani umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira.
Pamoja na kujitahidi huko, kuna baadhi ya mapungufu ambayo yamejitokeza kama;
Mulokozi ameonyesha utenzi wa ngomezi, ila hajayuonyesha vipera au vitanzu vinavyojitokeza au kupatikana katika utanzu huu.
Mulokozi ameainisha na vipera vya fasihi simulizi lakini yeye mwenyewe anakiri kuwa bado hakuna wataalamu walioshughulikia suala hili undani zaidi kwani tanzu za fasihi simulizi hutifautiana kati ya jamii na jamii, Hivyo Mulokozi ameonyesha udhaifu wa kitaaluma
Mulokozi ameshindwa kutofautisha istilahi ya Tanzu na Vipera. Badala ya kutumia vipera yeye ametumia tanzu: vipera vya hadithi yeye anasema fungu au tanzu za kihadithi.
Mulokozi pia ameonyesha udhaifu pale anaposema misimu ikipata mashiko huingia kwenye methali, wakati misimu ikipata mashiko ya kutosha si lazima kuingizwa kwenye methali tu bali huingizwa kwenye msamiati wa lugha sanifu mfano: ngunguli, ngangali na ulanguzi
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, uainishaji wa tanzu na vipera vya fasihi simulizi kama vilivyoainishwa na Mulokozi vinaingiliana kifani na  kimaudhui.
KIELELEZO KINACHOONYESHA TANZU NA VIPERA VYA FASIHI SIMULIZI.
MAREJEO
Mulokozi, M.M. (1989) Tanzu za Fasihi Simulizi Mulika 21:1-24, Dar es salaam: TUKI.
Mulokozi, M.M. (1996) Fasihi ya Kiswahili, Chuo Kikuu Huria cha Dar es salaam
Wamitila, K.W.(2002) Uhakiki wa Fasihi Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi, Phoenix, 
                         Publishers Ltd.


NADHARIA ZA UCHAMBUZI WA FASIHI



Wataalamu mbalimbali wameainisha nadharia mbalimbali za uchambuzi wa kazi yoyote ya fasihi. Miongoni mwa nadharia hizo ni pamoja na;
Nadharia ya umuundo (structuralism)
Umuundo ni nadharia inayojibainisha kwa kuangalia Ujumla wa uhusiano wa sehemu moja kwa nyingine katika kufanya kitu kizima. Kwa mfano muungano wa maneno hufanya sentensi na sentensi zikiungana zinaunda aya au onesho na onesho kuunda tamthiliya.
Ntarangwi (2004) anasema kuwa umuundo waweza kuelezwa kama mtizamo wa kitathimini ambao huzingatia zaidi miundo inayojenga kazi binafsi.
Mwasisi anayetajwa sana katika nadharia hii ni Ferdinard De saussure aliyependekeza mtizamo mpya kuhusu lugha. Kinyume na wataalamu wengine walioshughulikia historia na sura maalum za lugha fulani, Saussure alivutiwa na miundo inayohimili lugha zote, huku akijaribu kuonyesha kwamba lugha zote za ulimwengu zaweza kutathiminiwa kwa kaida maalum za umuundo. Alizua istilahi `parole' na `langue' kueleza maoni yake: `Parole' au uzungumzi ni lugha katika matumizi na hiki ndicho walichokizingatia wanaisimu wa awali, lakini Saussure alivutiwa na mfumo wa kinadharia unaounda lugha zote au `Langue' - yaani masharti au kaida zinazoiwezesha lugha kuwepo na kuweza kufanya kazi.
Hata hivyo, kazi ya Saussure ilikuwa imetengewa wanaisimu peke yao. Katika miaka ya 1950, mtizamo huo wa Saussure ulianza kusambaa katika masomo mengine hasa wakati mawazo yake yalipozingatiwa na Mwanaanthropolojia Claude Levi-strauss. Kwa kuchukua maoni ya isimu ya Saussure na kuyaingiza katika sayansi ya kijamii . Hasa alichotaka kuendeleza kidhana ni kwamba pana viwango viwili katika kuelewa maisha ya jamii, isimu, lugha na chochote kingine kile. Viwango hivi ni cha juu juu (surface) na cha ndani (deep).
Mkondo huu wa mawazo ya umuundo kuhusu sayansi za jamii ulianzia ulaya na kuathiri mtazamo wa elimu mbalimbali (duniani) kama vile: Falsafa, Anthropolojia, Historia, Uhakiki wa kifasihi na Sasiolojia.
Kwa hivyo twaweza kuangalia jamii katika muundo wake wa kijuu juu na kuielewa lakini tukitaka kupata maana mwafaka lazima tuchunguze muundo wake wa ndani ambao hupatikana katika kila jamii ya wanadamu. Kwa hiyo hata katika kuielewa fasihi lazima tuifahamu lugha yake.
Katika kupata maana lazima kuwe na uhusiano wa kipembetatu yaani kuna DHANA, ALAMA na KITAJWA.
UMUUNDO NA FASIHI
Kama vile muundo wa lugha ulivyo mfumo, muundo wa fasihi pia una vipengele vinavyotegemeana na vinavyoelezwa katika muktadha wa vipengele vingine. Katika kazi ya fasihi kuna kitengo cha kisanaa kama vile maudhui, ploti, wahusika, muktadha na lugha. Hakuna kipengele cha fasihi kati ya hivi kitakachoelezwa katika upekee wake. Lazima kielezwe kwa kuzingatia kuwepo kwa jukumu la vipengele vingine. Kwa mfano katika kueleza au kuzungumzia ploti, wahusika watashirikishwa na lugha yao kuzingatiwa.
Kwa hiyo nadharia ya umuundo husisitiza vipengele vya kazi ya sanaa, jinsi vinavyohusiana hadi kuikamilisha kazi hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi za sanaa zilivyofungamana. Yaani Neno halihitaji urejelezi ili lipate maana, na Kazi yenyewe ilivyoundwa ndivyo hutoa maana. Yaani maana inavyoumbwa ina dhima kubwa kuliko maana yenyewe.
Wafula na Njogu (2007) wanasema kuwa Umuundo unapinga wazo la kijadi linalodai kwamba fasihi ni tokeo la mchango wa maudhui na fani. Dhana ya kimapokeo kuhusu fasihi inadai kwamba fasihi ni umbo lenye viungo viwili, maudhui na fani na kwamba viungo hivi vyaweza kutenganishwa.
Wahakiki wanoegemea mkondo wa Saussure huzingatia kwamba matini husika ni mfumo unaojisimamia na hivyo basi huwa hamna haja ya kutumia mambo ya nje ili kuhakiki kazi ya fasihi. Wahakiki huzingatia matini kama kiungo kamili kinachoweza kuhakikwa kivyake. Hivyo basi mhakiki wa umuundo hujaribu kuweka sarufi ya matini pamoja na sheria za jinsi matini hiyo hufanya kazi.

Mhakiki anayezingatia zaidi muundo wa lugha ya matini bila shaka hupuuza dhana ya jadi kuhusu kile matini hiyo huweza kutueleza kuhusu maisha; na hivyo basi hufanya mtindo wa kazi yenyewe kiini cha uhakiki wake. Kwa hivyo wahakiki wanaotumia nadharia ya umuundo hujaribu kuzingatia matini peke yake huku wakiepuka kuifasiri kazi ile kulingana na kaida zilizowekwa kuhusu jinsi matini hufanya kazi.
Hata hivyo, huenda njia hii isiwe ya kufaa sana kwa sababu huwa inachukulia kwamba kila kitu kimeundwa katika mpangilio halisi usiotatanika na usiotegemea mambo mengine yaliyo nje yake. Ama kwa hakika, hata lugha yenyewe haiwezi kabisa kufanya kazi bila kuathiriwa na mambo mengine kama vile mazingira yake (Ntarangwi 2004).

Nadharia ya umarx (marxism)
Kwa maana rahisi kabisa, tunapoongelea kuhusu nadharia ya U-Marx tuna maana ya kurejelea mikabala mbalimbali ambayo misingi yake mikuu ni mawazo yanayohusishwa na Carl Marx na Friedrich Engels.  Katika kitabu cha The Germany Ideology, Marx na Engels walisema kuwa kitu cha msingi katika maisha ya binadamu ni kula na kunywa, kupata malazi na mavazi na mambo mengine. Tendo la kwanza la kihistoria kwa hiyo ni kutafuta njia ya kuyakidhi mahitaji haya ya msingi. Ili kufanikiwa katika lengo hilo, binadamu hulazimika kujiunga pamoja au kuunda umoja ili kuimarisha umoja na wepesi wa kuizalisha mali ya kukidhi mahitaji hayo. Muungano huo huwa na ugawaji wa majukumu au kazi ambayo ndiyo msingi wa kuundwa kwa matabaka katika jamii. Hatua ya juu ya mwendelezo huu ni uzukaji wa mfumo wa ubepari. Katika mfumo huu, mali inamilikiwa na idadi ndogo ya watu. Watu hao wanaipata mali yao kutokana na unyonyaji wa umma na hasa wafanya kazi (Wamitila 2002:).

Kwa mawazo ya Marx,  maendeleo ya jamii huthibitika katika vipindi vya maisha ambavyo kizazi cha binadamu kimepitia. Kutokana na Marx tabaka la jamii hutoweka na lingine huchipuka kwa sababu ya mgongano wa kitabaka. Mgongano huu hutokea kwa sababu kuna tabaka la wanyonyaji na wanaonyonywa. Hivyo, inabidi kuwa na mapinduzi dhidi ya mifumo ya kuzalisha mali inayohimili unyonyaji. Mapinduzi yanayotokea baadaye yanaongeza tumaini la ujenzi na uimarishwaji wa jamii inayozingatia usawa. Marx anamwona binadamu kuwa kiini cha historia yote na matendo yote yanayotendeka humu duniani. Umarx unamwabudu binadamu, hivyo humpa tumaini binadamu la kung’oa mizizi yote ya unyonyaji na unyanyasaji na kujenga ulimwengu wa kinjozi usiokuwa na madhila (Wafula na Njogu 2007). Vidato ambavyo jamii ilipaswa kupitia kabla ya kufikia ukamilifu wa kinjozi ni vifuatavyo: Ujima, Utumwa, Umwinyi, Ubepari, Ujamaa na Ukomunisti
Kwa jumla, twaweza kusema kwamba mhakiki wa Ki-marx hukita nadharia yake kwenye itikadi za Karl Marx na Fredrick Engels, na hasa kwenye madai ya hao wawili kuwa, katika tathimini ya mwisho kabisa maendeleo ya historia ya binadamu pamoja na taasisi zake, yatakuwa ni tokeo la mabadiliko katika njia za kimsingi za uzalishaji mali. Kwamba mabadiliko kama hayo husababisha mageuko katika muundo wa matabaka ya kijamii ambayo katika kila kipindi huendeleza kung'anga'aniwa kwa uwezo wa kiuchumi, kisiasa na kijamii; na kwamba dini, fikra na utamaduni wa jumuiya yoyote (zikiwemo sanaa na fasihi kwa kiwango fulani) huwa ni `itikadi' na miundo maalum ya `kitabaka' ambayo ni zao la miundo na matabaka ya kijamii yaliyomo wakati huo.

Umarx huchukulia kwamba jamii zote za kitabaka huzalisha mkururo wa miundo ya urazini inayokinzana na kushindana. Katika jamii ya kikapitolisti, kwa mfano, aina tofauti za mitizamo kuhusu maisha huwakilisha haja tofauti za kitabaka ambazo hutegemea hasa mikinzano kati ya mapato na nguvu za kutenda kazi. Kwa hivyo Umarx huhusisha itikadi na uzalishaji mali na jukumu lake katika mivutano ya kisiasa katika jamii. Jinsi watu binafsi wanavyoelewa msingi wa maisha yao hutokea kuwa kamba ya mvutano ambapo wanaweza ama kubadilika au kuendelezwa.
HOJA ZA UMARX KWA UFUPI

i/ Katika historia ya mwanadamu, jamii na mahusiano yake, taasisi zake namna yake ya kufikiri; mambo yote hayo hutegemea mabadiliko ya mfumo wa uzalishaji mali. Yaani jinsi uchumi, uzalishaji, mgawanyo na umilikaji mali unavyoendeshwa.

ii/ Mabadiliko ya kihistoria katika msingi wa uzalishaji mali yanaathiri mabadiliko ya muundo wa matabaka ya jamii, na hivyo hutokeza (kwa kila wakati) tabaka tawala na tawaliwa ambayo huwamo katika mapambano na harakati za kugombea uchumi, siasa na faida za kijamii.

iii/ Urazini wa mwanadamu umeundwa na itikadi. Imani, thamani ya kitu, namna za kufikiri na kuhisi. Ni kupitia hivi, mwanadamu huuona ulimwengu wake, na huelezea yale yaliyomzunguka na yale anayoyaona kuwa kweli.

Kwa hiyo wazo kuu la U-Marx ni kwamba hata waandishi wa mkondo huo huandika kwa kutumia falsafa ya Marx jinsi alivyoiona historia ambapo wazo kuu ni kuwa: harakati za matabaka ndio msingi mkuu unaofanya mambo yawe kama yalivyo.


Umarx katika Fasihi

§  Usanii ni uumbaji wa Ukweli katika maisha.
§  Ukweli unaooneshwa katika kazi za fasihi hiyo ni usahihi wa mambo katika jamii? Kama ni Riwaya, Tamthilia, Ushairi na kadhalika inawakilishaje ukweli?
§  Kazi za kisanaa zinatakiwa kuonesha mivutano iliyopo katika jamii hasa kati ya wanyonyaji na manyonywaji.

Nadharia ya urasimi
Kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007) Urasimi ni wakati maalumu ambapo misingi ya kazi za sanaa huwekwa na kukubalika kuwa vipimo bora kwa kazi nyingine. Hii ina maana kwamba kila jamii ina urasimi wake. Urasimi katika Kiswahili ulikuwepo kati ya karne ya 18 na karne ya 18. Nao urasimi wa Kigiriki ulikuwepo baina ya karne ya nne (KK) na takriban karne ya nne (BK). Ieleweke kuwa si sahihi kuamini kama baadhi wanavyodhani kuwa unapozungumzia urasimi, huwa na maana ya msingi ya kitaaluma iliyowekwa na Wagiriki na Waroma wa kale.
Sifa za urasimi kwa ujumla
Pamoja na kwamba imeshatajwa hapo mwanzo kuwa kila jamii ina urasimi wake, lakini bado tunaweza kutoa sifa za jumla za urasimi mahali popote ulipo. Kwa mfano:
  • Kazi ya kirasimi huwasilishwa katika lugha inayoeleweka  kwa urahisi. Hii ina maana kuwa wazo linaelezwa moja kwa moja. Mitindo ya Kinjozi (mf. Nagona, Mzingile, Bina-Adamu, Walenisi)  haitumiwi. Uhalisia unasisitizwa.
  • Kazi nyingi za kirasimi hazichoshi kusoma. Hii ni kwa sababu kazi hizi ni kazi bora. Husomwa mara nyingi na watu wengi na kila unapoisoma wazo jipya hupatikana.
  • Fani na maudhui katika kazi za kirasimi ni mambo yaliyofinyangwa kwa kutumia mbinu kamilifu na teule. Daima kuna ufungamano uliokamilika kati ya kinachoelezwa na jinsi kinachoelezwa.
Katika urasimi wa Kigiriki watu mashuhuri ambao walikuwa wanarejelewa sana ni kama Plato, Aristotle, Horace na Longino. Kazi maarufu kwa upande wa Tamthilia inayoweza kutumika kama mfano wa urasimi wa enzi hizo ni kama ile ya Sofokile iitwayo Mfalme Edipode (1971) iliyotafsiriwa na Samuel Sateven Mushi.
URASIMI WA KISWAHILI
Njogu na Wafula (2007) wanasema kuwa kazi za kirasimi katika fasihi ya Kiswahili zipo.  Hata hivyo uhakiki wa kirasimi kuhusu kazi hizo ni nadra kupatikana. Msomaji wa kazi za kirasimi katika fasihi ya Kiswahili anapaswa kuhitamidi uhakiki wake kutokana na utunzi wenyewe. Urasimi wa Kiswahili ulifikia kilele chake katika karne ya 18 na 19. Kazi zinazodhaniwa kuhusishwa na urasimi wa Kiswahili ni pamoja na hizi: Utenzi wa Al-Inkshafi, Utenzi wa Hamziyya, Utenzi wa Mwanakupona. Kazi za watunzi wa mashairi ya unne (tarbia) kama Muyaka wa Muhaji, Mohammed Mataka na Ali Koti, “Sheria za kutunga mashairi na Diwani ya Amri” (1954) (Amri Abeid).
Kazi zingine za kirasimi kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007:21) ni kama vile riwaya za; Kiu (M.S.Mohamed, 1972), Utengano (S.A. Mohamed, 1980), Harusi za Buldoza na Hadithi nyingine (S.A. Mohamed, 2005)
Pia tamthilia kama: Kinjeketile, Mashetani (E.N. Hussein, 1969, 1971), Kilio cha Haki (A.M Mazrui, 1982), Sauti ya Dhiki (A.Abdalla, 1973).
Sifa ya fasihi ya Kiswahili katika misingi ya Kirasimi
·         Huu ni wakati ambapo misingi ya ushairi andishi wa Kiswahili ilipowekwa.
·         Mengi ya mashairi ya kirasimi yalipokezwa kwa mdomo na uhakiki pia ulifanywa kwa njia ya kimasimulizi.
·         Mashairi yalitumia lugha teule
·         Warasimi wa Kiswahili walitumia lugha rahisi iliyoeleweka na ujirani wao bila shida yoyote.
·         Masimulizi marefu kama vile utenzi yana mwazo, katikati na hatimayake.



JE ONTOLOJIA YA KIAFRIKA INAWEZA KUTUMIKA KAMA NADHARIA YA KUCHAMBULIA KAZI ZA FASIHI ZA KIAFRIKA?.


Katika kueleza mada hii tutaanza na ufafanuzi wa maana ya falsafa.
Wikipedia kamusi elezo huru wanasema,falsafa ni neno linalotokana na neno la kigiriki lenye maana ya upendo na hekima,wanaendelea kusema kuwa falsafa ni jaribio la kuelewa na kueleza ulimwengu kwa kutumia akili inayafuata njia ya mantiki .Falsafa huchunguza mambo kama vile kuweko,au kutokuweko,ukweli,ujuzi ,uzuri,mema, na mabaya,lugha na haki.
Kwa mujibu wa Wamitila (2003 ) anasema, falsafa ni mawazo anayoyaamini mtu au mwandishi  kuwa yana ukweli unaotawala misingi ya maisha.
Hivyo, Falsafa ni taaluma au mtazamo unaochunguza matumizi ya dhana,kupima hoja,mbinu za ujengaji hoja,kufanya uhakiki au tathimini,kuthibitisha au kutoa ushahidi wa hoja zinazozungumzwana nadharia mbalimbali zinazohusu maisha.Mfano,kuua ni tendo zuri au sio zuri?
Pia fasihi ya Fasihi ya Afrika, tunaweza kusema inamaanisha maandiko kuhusu na kutoka Afrika. Kama George Joseph anavyodokeza katika ukurasa wa kwanza wa sura yake katika kitabu chake cha ‘understanding contemporary Afrika’ wakati mtazamo wa fasihi ya ulaya kwa ujumla inahusu herufi zilizoandikwa, dhana ya Afrika inahusu fasihi simulizi.Pia ansema fasihi inaweza kuashiria matumizi ya maneno kisanaa kwa ajili ya sanaa pekee.
Kwa ujumla Fasihi ya Afrika ni sanaa yoyote, au fashi yoyote ile inayopatikana katika bara la Afrika.
Pia istilahi Nadharia, Kwa mujibu wa TUKI (2004), Wanasema nadharia ni mawazo, maelezo, mwongozo uliopangwa ili kusaidia kueleza,kutatua au kutekeleza jambo fulani.
Nao Njogu na Rocha (2008), wanasema nadharia ni kioo cha kumulika kila jambo au tendo limuhusulo binadamu ulimwenguni  inakuwa ngumu gizani.
Pia Wamitila (1996), Anasema kuwa, nadharia ni maarifa ya kitaalamu ambayo msomaji au mhakiki anapaswa kuyajua na kuyafahamu kabla ya kuanza kazi zake.
Hivyo basi sisi tunakubaliana na TUKI, kwa kusema nadharia ni mawazo, maelezo,mwongozo uliopagwa ili kusaidia kueleza,kutatua au kutekeleza jambo fulani.
Ama kuhusu Ontologia huu ni moyo wa falsafa. Ontologia ni tawi la falsafa ambalo huchunguza asili ya vitu, (binadamu ametoka wapi?,dunia imetoke wapi?,shetani ni nini?) Pia huchunguza uwepo wa vitu mbalimbali,vitu vilivyo hai na vitu visivyokuwa hai, vinavyoonekana na visivyoonekana.
Maana ya Ontologia tunaweza kusema ni falsafa ya utafiti wa asili nya kuwa wakati wa kuwepo au ukweli.wanaendelea kusema neno ontolojia asili yake ni kigiriki.
Ontolojia, pia ni nadharia ya vitu na mahusiano yao,inatoa vigezovya kubainisha aina tofauti ya vitu (halisi na kufikirika,uwepo na haipo,kweli na bora,kujitegemea na tegemezi) na mahusiano yao.
Naye Mihanjo A, (2010) akimnukuu Anselm katika nadharia yake ya kiontolojia,anselmamethibisha ontolojia kwa kuonyesha uishi wa Mungu.Anselm ameelezea na kuonyesha asili na uishi wa Mungu.
Kwaujumla Ontolojia  ni tawi la falsafa ambalo huchunguza asili ya vitu,(binadamu ametoka wapi?,dunia imetoke wapi?,shetani ni nini?)pia huchunguza uwepo wa vitu mbalimbali,vitu vilivyo hai na vitu visivyokuwa hai,vinavyoonekana na visivyoonekana.
Mkondo tulioutumia ni mkondo wa falsafa za kijamii na kisiasa . Mkondo huu unazingatia na kuangalia falsafa za jamii na siasa. Mkondo huu umefafanuliwa na kuelezwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Keneth  Kaunda na Kwame Nkurumah.
Tukianza na ; Mwalimu Julius Kambalage Nyerere ambaye anatetea mkondo huu kwa vigezo vifuatavyo;
Anadai kuwa ujamaa wa kiafrika ni kama Afrika pana ujamaa ambao unakuwa mwendelezo wa kifamilia na kuishi vizuri na watu vilevile anadai kuwa si ujamaa wa kimax ambao unatetea mgogoro wa kitabaka.Yeye anaona asili ya ujamaa ni jamii za kiafrika.
Sera ya mipango inajadiliwa na kurekebishwa na watu wote.Kila mtu alifanya kazi  katika ardhi ya jamii nzima na kila mtu alipata matunda kulingana na kazi yake.
Anaendelea kusema, ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga kumnyonya mtu.Hivyo wito wake ni kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.
Mtaalamu mwininge ni Kwame Nkurumah ambaye ametumia vigezo vifuatavyo;
Anadai kuwa ujamaa ulikuwa msingi  wa jamii za kiafrika kuliko ubinafsi hivyo ubepari utaiharibu Afrika, Afrika haita kuwa huru ikiwa itaendelea kuwa chini ya ubepari wa kimagharibi.
Huyu aliathiriwa na falsafa ya kimarx na renin lakini hakutaka kuitumia kama ilivyo alitaka uimalishwe ujamaa wenye asili ya kiafrika na vipengele vya kiislam na kikristo vya ulaya.
Keneth Kaunda alisema waafrika walifanikiwa  kuushinda ukoloni kwa sababu ya utu na sio nguvu katika kufikia ukamilifu wa utu binadamu lazima alenge kufanana na mungu. Mungu ni usawa wa kila kitu,mungu ni amani,upendo na utu,utu unavileta pamoja dini na siasa na kuzaa taifa la watu wanaopendana.
Anamalizia kwa kusema kuwa nguvu katika kujikomba si mbinu sahihi ya ukombozi bali nguvu inaweza kutumika katika kujilinda  aliandika  African humanism.
Baada ya kueleza mkondo na vigezo vya wataalam wa falsafa za kijamii na siasa ,tunachambua riwaya ya kufikirika ambayo ni kazi ya fasihi ya kiafrika kwa kutumia mkondo wa falsafa za kijamii  na kisiasa.
Riwaya ya kufirika ameandikwa na Shahban Robert chapa ya nne mwaka (2008) kufikirika ni riwaya inayohusu maisha na maswaibu yaliyo mkuta mfalme na malkia wa kufikirika kwa kuchelewa kupata mototo.
Uchambuzi wetu unaanza kama ifuatavyo;
Suala la imani, imani ni kuwa uhakika wa mambo yatarajiwayo. Nyerere anasema kuwa kila mtu alifanya kazi katika ardhi ya jamii nzima na kila mtu alipata matunda ya kazi yake. Katika riwaya hii( uk3-4), unaonyesha jinsi ,mfalme anavyoamini kuwa na watoto wengi ndio nguvu ya ufalme wake pia mfalme aliamini waganga, kafara,ramli,hirizi,mazinguo,mashetani na watabiri.(Uk 8-11), ndio maana mfalme aliwaita waganga wote wafike kwake ili waweze kuagua na kutabiri juu ya utasa na ugumba wao.
Utawala, katika riwaya hii mwandishi ameeleza suala la utawala kwa kumtumia mfalme kama mfano wa mtawala mwenye uongozi mbovu wenye mabavu “(uk 4) mfalme alipoamua waitwe waganga wote wa jadi mfano waganga wa mashetani,makafara,watabiri,hirizi,wa mizizi,mazinguo na mashetani asiye hudhulia apewe adhabu pia katika uk(23-25) mfalme anamfukuza mwalimu kazi.
Suala la ukombozi,ukombozi ni hali ya kujitoa kutoka hali  fulani kwenda hali nyingine .Katika riwaya hii kuna ukombozi wa kisiasa,mwandishi amemtumia mjinga,ameonyesha jinsi mjinga alivyosimama kisheria dhidi ya kifo kilichokuwa kinawakabili,kifo  ambacho hakikuzingatia utu wa binadamu (uk38.)KenethKaunda ansema, waafrika walifanikiwa kuushinda ukoloni kwa sababu ya utu sio nguvu,katika kuufikia ikamilifu wa utu binadamu lazima alenge kufanana na Mungu.
Matabaka katika jamii, matabaka ni mgawanyiko wa makundi ya watu  (kiuchumi,kisiasa,kielimu na kijamii) katika jamii. Katika riwaya hii kuna matabaka makuu mawili,tabaka la kwanza ni tabaka tawala,ambalo liliundwa na viongozi wa serikali, wanasheria,mahatibu na wafanya biashara,tabaka tawaliwa lilikuwa ni wakulima,(tabaka la mwisho),(uk 35-36).Matabaka katika jamii hayafai kwani huondoa umoja,Nyerere anapinga matabaka hivyo wito wake ni kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.
Athari za uongozi mbaya, huu ni uongozi usiofuata haki za raia wake, baada ya maamuzi ya mfalme kuwaruhusu waganga mfano;waganga wa mizizi walichimba mzizi ya mti,walitoa magome na kukata matawi ya miti,hali iiliyopelekea ukame wa  nchi na uharibifu wa mazingira na makazi ya wanyama,waganga wa kafara walitumia pia kwa moto na walihitaji damu za wanyama kwa ajili ya kafara,hivyo wanyama wengi walikufa.Ni vizuri kufikiri jambo kabla ya kutenda.
Umuhimu wa uzazi, katika riwaya hii mfalme aliona fahari yake yote si kitu kwani alikosa kuwa na mtoto (uk 1-3) anasema, “Nina majeshi ya askari walioshujaa, waongozi hodari raia wema,watii ambao hawalingani na Taifa lolote jingine katika maisha yake yote nashukuru kwa Bwana vitu vya faraja,visivyokwisha lakini nina sikitiko kubwa kwa kukosa mtoto”. Jamii ya kufikirika waliamini kuwa na watoto wengi ndio ujenzi wa nguvu wa Taifa lao. (uk 3) Mfalme anaamini watoto ndio nguvu ya ufalme wake.
Mapinduzi ya kisiasa,na kiutamaduni,mapinduzi ni kufanya mabadiliko, yaani kuondoa utawala au siasa ya kwanza na kuingia siasa mpya.katikas riwaya hii mjinga alitumia utu wake kufanya mapinduzi kwa kumsaidia mototo wa mfalme kupata dawa hospitalini,na kupona,wanakijiji wa kufikirika walizoea utamaduni wa kuwaamini waganga wa jadi na sio hospitali.Pia katika siasa mjinga alijaribu kutetea haki na sheria ya utu,kwa kuzuia kafara ya watu kutalewa kwani haina umuhimu.
Kazi nyingine ya fasihi  ipatikanayo Afrika ni ushairi wa fungate ya uhuru.Fungate ya uhuru ni diwani iliyoandikwa na Mohamed S. khatibu mwaka (1988). Diwani hii inajadili mambo yanayokwamisha ujenzi wa jamii mpya katika nchi zetu za Afrika. Katika diwani hii tutachambua mambo hayo kwa kutumia mkondo wa jamii na siasa. Uchambuzi wetu unaanza  kama  ifuatavyo;
Kuwa na uongozi bora ,uongozi mbaya ni kikwazo cha ujenzi wa jamii mpya.Katika diwani hii inaonyesha jinsi viongozi wanavyotumia  madaraka yao vibaya kuwanyonya wananchi wa kawaida.Nyerere anasema sera ya mipango inajadiliwa nakurekebishwa na watu wote.Pia ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga kumnyonya mtu,hivyo yeye anasisitiza kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.Diwani inaonyesha kuwa uongozi mbaya ni kikwazo cha ujenzi wa jamii mpya(uk15-16) shairi la “Viongozi wa Afrika”,hapa mwandishi amekemea viongozi wanaotumia madaraka vibaya.Mashari mengine yanayozungumzia uongozi mbaya ni “Fungate”, “Waja wa Mungu”, “Wizi”, “Utawala”, “Njama”, “ujamaa”.
Kupinga vita ukoloni mamboleo,ukoloni mamboleo ni ile hali ya nchi kupata uhuru kisiasa lakini njia nyingine za uchumi hutawaliwa au hubaki mikononi mwa mabepari aunyingine.Kwame Nkurumah anasema ujamaa ni msingi wajamii za kiafrika kuliko ubinafsi,hivyo ubepari utaiharibu Afrika,Afrika haitakuwa huru ikiwa itaendelea kuwa chini ya ubepari wa kimagharibi.Katika shairi la “Ruya”,anonyesha kuwa wazungu ndio waliondoka katika ardhi ya Afrika lakini unyoyaji bado upo.Pia katika shairi la “kunguru”,mwandishi ameonyesha athari za ukoloni mamboleo.
Kufanya mageuzi,mageuzi huleta mafanikio katika ujenzi wa jamii mpya.Keneth Kaunda anasema waafrika walifanikiwakuushinda ukoloni kwa sababu ya utu na sio nguvu,pia nguvu katika kujikomboa si mbinu sahihi ya ukombozi bali nguvu inaweza kutumika katika kujilinda.Mwandishi naye ametoa njia mbalimbali ili kufanikisha ukombozi katika shairi la “Unganeni”,pia mwandishi anapendekeza kutumia silaha katika mageuzi ikiwa unyonyaji hautaondoka kwa njia ya amanimfano katika shairi la “Siku itafika” (uk 30) na “Nikizipata bunduki).

Umoja na Ushirikiano, hii ni mbinu mojawapo ambayo mwandishi amependekeza  kama mojawapo ya njia ya ujenzi wa jamii mpya.Nyerere asisitiza watu kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Katika shairi la “unganeni” (uk 1) mwandishi anawataka waafrka wote tuungane ili kuendeleza mapambano ya kuleta haki na usawa.

Kujenga nchi itayofuata mfumo wa ujamaa, Nyerere anasema,ujamaa wa kiafrika ni kama Afrika pana, ujamaa ambao unakuwa mwendelezo wa kifamilia na kuishi vizuri na watu na sio ujamaa wa kimax unaotetea migogoro yakitabaka,mwandishi anashauri ujamaa kuwa ni sululisho la wanyonge,shairi la “Ujamaa” shairi hili linajadili wapinzani wa ujamaa.Mwandishi ansema ujamaa umeumbuliwa,umethiliwa,umekashifiwa na umesalitiwa.

Kupiga vita wizi wa mali ya umma,sehemu nyingi zimeoza kwa wizi,ikulu na viongozi wamejiunga na wahalifu.Katika shairi la “Wizi” na “Kunguru” (uk19) ameeleza wezi waliotimuliwa na kutawanywa, shairi la “Joka la mdimu” mwandishi anatanabaisha watu kuhusu uwezekano wa wakoloni kurudi kwa umbotofauti lakini athari ni zile zile,pia katika shairi la “Naona” (uk 33) anoonyesha taabu wazozipata wakulima na malipo duni wanayopewa kwa mazao yao.

Kitabu cha tamthiliya ya “Nguzo mama” iliyoandikwa na Penina Mhando(1982).Tamthiliya hii inasawiri na kuyaelezea matatizo mbalimbali yanayowakabili na kuwaelemea wanawake wengi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.Kwa kutumia mkondo wa kisiasa na kijamii tumechambua tamthiliya hii kama ifuatavyo;

Uongozi mbaya, katika tamthiliya hii mwandishi ameonyesha umuhimu wa uongozi bora, na kiongozi bora. Nyerere anasema ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga kumnyonya mtu, anasisitiza kuwa kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.Katika kijiji cha patata kulikuwa hakuna ujamaa. Katika jamii kiongozi anaweza kuipeleka jamii yake kwenye neema au kwenye mdomo wa simba kutegemeana na uongozi wake anavyoupeleka (uk 22), kijiji cha patata kilikuwa na uongozi mbaya wa kidikteta, mfano; Mwenyekiti, kamati ya halmashauri,wanatumia vitisho kumlazimisha Bi nane kusema asichokijua (uk24).

Uvivu na Uzembe, huwa haufai katika jamii,katika mkondo huu Nyerere anasema kila mtu alifanya kazi katika ardhi na kila mtu alikula matunda ya kazi  yake hivyo mtu akiwa mzembe atakula matunda ya uvivu na uzembe ambayo si mema.katika kijiji cha patata watu hawa walikuwa ni wavivu na wazembe,ndio maana ilipekea kufifia na kushindwa kuinua  Nguzo mama”. Wanawake hawa walikuwa hawawajibiki, mfano;(uk 34)

Mapenzi na ndoa, katika “Nguzo mama”kuna mapenzi yasiyokuwa ya kweli,yanayoyojali pesa na usaliti kati ya wanandoa.Mapenzi haya hayana utu kwani ndani ya utu kuna amani na upendo wa kweli.Usaliti huleta hali ngumu katika familia mfano;familia ya Bi tano wanalala njaa kwa kukosa chakula na mahitaji muhimu kwa kuwa Maganga baba yao anamaliza pesa zote kwa wanawake.mfano ;

“Wee Bi sita mshenzi unanichukulia mume wangu hivihivi kimachomacho”(uk 39)
Umoja na ushirikiano, hiki ni kitu muhimu sana katika jamii Nyerere anasisitiza kuwa na umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni .Asili ya ujamaa ni Afrika na si ujamaa wa kimarx unaotetea matabaka.Kijiji cha patata watu wake walikosa umoja na ushirikiano ndio maana walishindwa kuinua nguzo mama kwani kila mtu anajali mambo yake Bi moja anaacha kazi anaenda kuangalia khanga (uk 34
Dhuluma, hii imeghubika jamii yetu ya leo,katika tamthiliya hii ya Nguzo mama mwandishi amejaribu kutuonyesha jinsi jamii ya Patata kama zilivyo jamii iliyooza kwa dhuluma hasa pindi wanawake wanapofiwa na waume zao,mfano Bi saba anaoonyesha jinsi gani wanawake wengi wa kiafrikawanavyodhulumiwa mali na ndugu wa mwanaume zao pindi wanapofariki.Bi saba  baada ya kufiwa tu shemeji  walikuja kugawana vitu.mfano( uk 43);
.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kumba riwaya hii ya kufikirika,tamthiliya ya nguzo mama na ushairi wa fungate ya uhuru zimeweza kuchambuliwa vizuri na tawi hili la ontolojia.Tumeweza kuona ni jinsi gani vitu halisi na vingine vya kufikirika vikitendeka katika kazi hizi,vilevile suala zima la falsafa za kijamii na siasa kama zilivyokwisha elezewa hapo mwanzo.Ujamaa unaonekana kuwa ni hali inayopelekea maendeleo katika jamii,ontolojia ya kiafrika hutumika kuchambulia kazi za fasihi za kiafrika.

MAREJEO
1.Mihanjo A,(2010)Falsafa na ufunuo wa maarifa.Toriam.Morogoro Tanzania.
2.Mohamed S.k (1988)Fungate ya uhuru.Dar-es-salaam university place(DUP).
3.Muhando p (1982) Nguzo mama. Dar-es-salaam university place(DUP).
4.Njogu na Chimera R(1999)Ufundishaji wa fasihi,Nadharia na Mbinu.Jomo Kenyatta.Nairobi
5.Tuki(2004)Kamusi ya Kiswahili sanifu.Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.Dar-es-salaam.
6.Robert,S.(2008) Kufikirika.Mkuki na nyota:Dar-es-salaam Tanzania.
7.Wamitila K.W (1996) Utangulizi wa Kiswahili.Chuo kikuu cha Dar-es-salaam.Dar-es-salaam.



                      CHIMBUKO LA RIWAYA YA KISWAHILI.


Katika kujadili mada hii, mjadala huu, utajikita zaidi kutoa maana ya riwaya kutoka kwa wataalamu mbalimbali, maana ya riwaya ya Kiswahili, maana ya chimbuko, Kisha mjadala huu utaelekea zaidi katika kuelezea chimbuko la riwaya ya Kiswahili kutokana na wataalamu mbalimbali waliopata kueleza asili ya riwaya hiyo ya Kiswahili, na hicho ndio kitakachokuwa ni kiini cha swali. Mwisho tutahitimisha mjadala wetu.
Kwa kuanza na maana ya riwaya imejadiliwa kama ifuatavyo:
Wamitila (2003), anasema riwaya ni kazi ya kinathari au kibunilizi ambayo huwa na urefu wa kutosha, msuko uliojengeka vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina, yenye kuchukua muda mwingi katika maandalizi na kuhusisha mandhari maalumu.
Muhando na Balisidya (1976), wanaeleza riwaya ni kazi ya kubuni, ni hadithi ambayo hutungwa kufuatana na uwezo wa fanani kuibusha mambo kutokana na mazoea au mazingira yake.Wanaendelea kusema kuwa riwaya yaweza kuanzia maneno 35000 hivi na kuendelea.
Nkwera (1978), anasema riwaya ni hadithi iliyo ndefu kuweza kutosha kufanya kitabu kimoja au zaidi. Ni hadithi ya kubuniwa iliyojengwa juu ya tukio la kihistoria na kuandikwa kwa mtindo wa ushairi iendayo mfululizo kwa kinaganaga katika kuelezea maisha ya mtu au watu na hata taifa. Anaendelea kusema kuwa riwaya ina mhusika mkuu mmoja au hata wawili.
Senkoro, anasema riwaya ni kisa ambacho urefu wake unakiruhusu kitambe na kutambaa vizingiti vingi vya maisha kama apendavyo mwandishi wake. Anaendelea kusema kuwa ni hadithi ndefu ya kubuni, yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja na yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatiwa kwa undani na upana wa maisha ya jamii.
Hivyo inaonyesha kuwa ili kujua maana ya riwaya ni vyema kuzingatia mambo kadhaa ambayo ndiyo ya msingi, na mambo hayo ni; lazima riwaya iwe na lugha ya kinathari, isawiri maisha ya jamii, iwe na masimulizi ya kubuni na visa virefu, wahusika zaidi ya mmoja, iwe na mpangilio na msuko wa matukio, lazima na maneno kuanzia elfu thelathini na tano na kuendelea, na mwisho riwaya ni lazima ifungamane na wakati yaani visa na matukio ni lazima viendane na matukio.
Baada ya kuangalia maana ya riwaya kutokana na wataalamu mbalimbali sasa ni vyema kutoa maana ya riwaya ya Kiswahili kabla ya kujadili chimbuko la riwaya.
Riwaya ya Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya waswahili katika lugha ya kiswahili ambao hupatikanakatika nchi ya Afrika mashariki. Pia ni ile riwaya ambayo inawahusu waswahili wenyewe.
TUKI (2004) inasema chimbuko la maana yake ni mwanzo au asili.
Tanzu za asili zinaonyesha kuwa ndio zilichangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuibua riwaya za Kiswahili.Na yafuatayo ni mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya chimbuko la riwaya ya Kiswahili.
Madumulla (2009), ameeleza kuwa riwaya ilitokana na nathari bunifu simulizi kama vile hadithi, hekaya, na ngano inayosimuliwa kwa mdomo. Anaendelea kusema kuwa fasihi ilitokana na maandiko ya fani ya ushairi hususan ni tendi za Kiswahili katika hati za kiarabu kwa sababu ndiyo maanadishi yaliyotamba katika pwani ya afrika mashariki. Wazungu na waarabu hawakubadilishana maarifa kwa urahisi na hivyo pakapelekea kuwa na majilio ya taratibu za maandiko ya kinathari. Mwanzoni riwaya zilitafsiriwa kwa Kiswahili toka katika lugha za ulaya na kufanya riwaya za Kiswahili kutokea. Mfano wa riwaya hizo ni kama vile; Habari za mlima iliyoandikwa na Sheikh Ali Bin Hemed (1980).
Senkoro (2011) anaeleza kuwa riwaya zilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya kiutamaduni, uchangamano wa maisha ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni yaliyopelekea haja ya kimaudhui zaidi ya ngano na hadithi fupi. Anaendelea kusema kuwa riwaya za kwanza zilitafsiriwa toka riwaya za kizungu mpaka za Kiswahili. Anasema riwaya mojawapo ni ile ya James Mbotela ya Uhuru wa Watumwa. Ndiyo riwaya ya kwanza kutafsiriwa kwa Kiswahili. Pia anaeleza kuwa  riwaya ni utanzu uliozuka  kutokana na hali mahususi za kijamii. Riwaya kama ile ya kiingereza ya Robinson  Crusoe iliyoandikwa na Daniel Defoe  ni miongoni mwa riwaya za mwanzo. Anasema riwaya ilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya kiutamaduni na viwanda.Suala la ukoloni  na uvumbuzi pia liliumba hali ambazo zilihitaji kuelezwa kwa mawanda mapana zaidi  ya yale ya ngano na hadithi fupi. Kupanuka kwa usomaji hasa wakati wa vipindi vya mapinduzi ya viwanda huko ulaya kilifanya waandishi waandike maandiko marefu kwani wakati huo ndipo walipoibuka wasomaji hasa wanawake waliobaki majumbani wakati waume zao walipokwenda viwandani kufanya kazi.
Mulokozi (1996) anaeleza kuwa chimbuko la riwaya ya Kiswahili lipo katika mambo makuu mawili ambayo; ni fani za kijadi za fasihi pamoja na mazingira ya kijamii.
Fani za kijadi za fasihi, Mulokozi anaeleza kuwa riwaya haikuzuka hivihivi tu bali ilitokana na fani za masimulizi yaani hadithi, na ndipo zikapatwa kuigwa na watunzi wa riwaya wa mwanzo. Fani hizo zilizopata kuchipuza riwaya za mwanzo ni kama vile; riwaya za kingano, tendi, hekaya, visakale, historia, sira, masimulizi ya wasafiri, insha na tafsiri.
Ngano, Mulokozi anasema, kuwa ni hadithi fupi simulizi pia huwa ni hadithi za kubuni na nyinga hasa zinawahusu wanyama wakali, pia zinahusu malaika, binadamu, mazimwi na majini. Anasema kuwa mara nyingi ngano huwa na msuko sahihi na wahisika wake ni bapa na wahisika hao ni mchanganyiko wa wanyama, mazimwi na binadamu. Anatolea mfano wa ngano zilizo chukua visa vya kingano kuwa ni kama vile riwaya ya Adili na Nduguze ya Shaban Robart (1952), Lila na Fila ya Kiimbila (1966), Kusadikika ya Sharban Robart (1951) na baadaye yakafuata machapisho mengine kama vile; Mfalme wa Nyoka ya  R.K. Watts. Dhamira za riwaya za kingano ni kama vile choyo, mgongano wa kimawazo na tama.
Hekaya,ni hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio ya ajabu yaani yasiyokuwa ya kawaida. Mara nyingi masaibu hayo hufungamanishwa na mapenzi. Pia hekaya ni ndefu kiasi yaani sio ndefu kiasi cha kama riwaya. Katika jamii ya waswahili hekaya zilikuwa zimeenea sana kipindi cha kabla ya ukoloni.Mifano ya hekaya ni kama vile; Hekaya za Abunuasi ya C.M.C.A. 1915, Sultan Darai (1884), Kibaraka ya (1896) na hekaya ya Jonson, F. na Brenn, E.W. Katika hekaya ya Alfa-Lela-Ulela ya kuanzia 1929. Hizo ndizo baadhi ya hekaya za mwanzo lakini baadaye ziliathili riwaya za Kiswahili kama vile; Hekaya ya Adili na Nduguze ya Sharban Robart (1952), hekaya ya Ueberu Utashindwa ya Kiimbila (1971), na Hekaya ya A.J.Amiri, ya Nahodha Fikirini, (1972).
Tendi (utendi), ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa wa kihistoria na wa kubuni, ambao waweza kuwa ni wa kijamii au kitaifa. Kwa kawaida baadhi ya tendi zina sifa za kiriwaya ila tu badala ya kuwa na umbo la kinathari zenyewe zina umbo la kishairi. Kuna tendi za aina mbili ambazo ni tendi andishi na tendi simulizi. Riwaya pevu kama tendi husawiri mawanda mapana ya kijamii na kihistoria. Huwa na wahusika wababe yaani mashujaa wenye kuwakilisha pande zinazopingana. Mfano wa tendi ni kama vile; Utendi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mlima ya Hemedi Abdallah, (1895), Utendi war as (Ghuli), utenzi wa Fumo liyongo wa Mohamed Kijumwa K. (1913).Tendi katika riwaya za Kiswahili imetumia wahusika wawili tu ambao ni wahusika wa kubuni na wale wa kijadi wa kiafrika.
Visasili, hizi ni hadithi zinazohusu asili na hatima ya watu, vitu, viumbe, ulimwengu na mataifa, na pia huangalia uhusiano wa wanadamu na mizimwi pamoja na miungu. Hadithi za kivisasili zinapoonyeswa huaminika kuwa yakweli tupu hasa kwa kusimulia matukio mengi ya kiulumwengu.
Mfano wa visasili; Lila na Fila ya Kiimbila (1966) ambayo imekopa motifu ya asili ya ziwa ikimba huko Bukoba. Hadithi ya Mungu wa Kikuyu huko Kenya. Roza Mistika ya Kezilahabi (1971), Nagona (1987) na Mzingile (1991), Siku ya Watenzi Wote ya Sharban Robart.
Visakale, ni hadithi ya kale kuhusu mashujaa wa taifa,kabila au dini. Mara nyingi visa kale huchanganya historia na masimulizi ya kubuni, na hadithi hizi hupatikana karibu katika kila kabila kila lugha.Baadhi ya visakale vya Kiswahili masimulizi huhusu chimbuko la miji ya pwani, mijikenda, mwinyi mkuu huko Zanzibar.Visa kama hivi ndivyo vinavyopelekea kuandikwa kwa riwaya za kiswahili. Mfano wake ni riwaya ya Abdalla Bin Hemed bin Ali Ajjemy (1972) katika kitabu cha Habari za Wakilindi, Kisima cha na Giningi ya M.S.Abdulla (1968) na ile Hadithi ya Myombekela na Bibi Bugonoka na Ntulanalwo na Buhliwali (1980) ya A. Kitereza.
Visasuli, hizi ni hadithi zozote ambazo huelezea chimbuko au asili ya kitu chochote, na maranyingi visasuli havina uzito wowote kulinganisha na visasili.mfano wake ni; kwanini paka anapenda kukaa jikoni (mekoni), Kwa nini mbuni hana mabawa yaani hapai angani, kwa nini kima anamuogopa mamba, kwanini mbwa kuishi na binadamu, kwa nini fisi hupenda kula mifupa. Katika hadithi hizi watu huwa hawaamini sana bali wanachukulia kuwa ni utani tu.
Masimulizi ya kihistoria, haya ni masimulizi ya matendo ya, mwanadamu katika muktadha wa wakati, na ni fani muhimu sana katika jamii yeyote ile. Masimulizi halisi ya kihistoria yaweza kuwa ni ya mdomo au hata maandishi na yote huwa ni chemichemi nzuri ya riwaya. Mfano wa riwya hizo ni; Habari za pate za Fumo Omari Nabhany (1913) ambayo yalikuwa ni maandishi ya masimulizi na uchambuzi. Riwaya zingine zilizoathiriwa na matukio ya kihistoria ni; Uhuru wa Watumwa ya J. Mbotela (1934), Kifo cha Ugenini ya O. Msewa (1977), Kwa Heri Iselamagazi ya B. Mapalala (1992) na Miradi Bubu ya Wazalendo ya G. Ruhumbika (1992).
Sira, ni masimulizi ya kweli kuhusu maisha ya mtu au watu. Sira huweza kuwa wasifu yaani zinazohusu habari za maisha ya mtu zikisimuliwa na mtu mwingine au zaweza kuwa tawasifu yaani habari za maisha ya mtu zikisimuliwa nayeye mwenyewe. Sira iliathiri kuchipuka kwa riwaya hasa kwa kuonyesha masilimulizi ya maisha ya mtu toka utotoni mpaka uzeeni. Masimuliza ya riwaya hizi yalikuwa katika masimulizi na hata katika maandishi pia kwa maana kabla ya ukoloni yalikuwepo maandishi yaliyohusu maisha ya mitume na masahaba.Mifano ya hadithi hizi ni; Kurwa na Doto ya M. S.Farsy (1960),Rosa Mistika ya Kezilahabi (1971),Kichwa Maji ya Kezilahabi (1974) pamoja na Dunia Uwanja wa Fujo (1975),Mzimu wa Baba wa Kale ya Nkwera (1967),na riwaya ya Maisha Yangu baada ya Miaka Hamsini ya Sharban Robart (1951).
Msimulizi ya wasafiri, hizi ni habari zinazosimulia masibu nya wasafiri katika nchi mbalimbali. Hekaya za riwaya chuku za kale zilisaidia kukuza riwaya. Mfano Alfa Lela –Ulela na hadithi ya Robinson Kruso huko 1719 ilihusu safari ya baharini ya mhusika mkuu ambaye baadaye merikebu aliyokuwemo ilizama, ndipo akalazimika kuishi peke yake katika kisiwa kidogo. Na katika riwaya za Kiswahili kuna baadhi ya riwaya za masimulizi kama vile; Mwaka katika Minyororo ya Samweli Sehoza (1921), Tulivyoona na Tulivyofanya Uingereza (1932)  ya Martin Kayamba. Na  uhure wa Watumwa na Kwa Heri Eselamagazi.
Insha,  ni maandiko ya kinathari yenye kuelezea, kuchambua au kuarifu kuhusu mada Fulani.Zipo insha za zina nyingi kama vile, makala, hotuba, tasnifu, michapo, barua, sira  maelezo n.k insha nyingi ni fupi mfano kuanzia maneno kama 500 na 10000 japo zingine zaweza kuwa ni ndefu kiasi cha kuwa tasnifu za kufikia kiwango cha kuwa kitabu. Mfano wa insha ni Siku ya Watenzi Wote ya Sharban Robert na Kichwa Mji ya Kezilahabi.
Shajara, ni kitabu cha kumbukumbu za matukio ya kila siku. Uandishi wa shajara ulianzia huko Asia na baadaye ndio ulipopata kuibuka ulimwenguni kote.Jadi hii ya kiasia iliathiri utunzi wa riwaya hasa zile za kisira. Mfano wa shajara ni ile iliyotungwa na Lu Shun iitwayo Shajara ya Mwendawazimu (1918).
Romansia (chuku) hii ni hadithi ya mapenzi na masaibu ya ajabu.Zikua maarufu sana huko Uingereza hasa karne ya 6 na 12 na Ufaransa pia zilikuwepo na pamoja na China ambapo hadithi zilizofanana na riwaya zilitungwa.mfano hadithi za Hsiao-shuo .Watunzi wa riwaya za kisasa zimekuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na riwaya hizo za chuku hii ni kwa sababu watunzi wengi wlikuwa wamesoma kazi nyingi za riwaya za wakati ule.
Drama, maigizo mengi hasa ya tamthiliya yaliathiri sana riwaya hasa kwa upande wa usukaji wa matukio na uchanganyaji wa ubunifu na uhalisia. Mfano ni riwaya nyingi za Charles Dickens zina msuko uliosanifiwa kwa uangalifu kama msuko wa tamthiliya.
Baada ya kujadili fani za kijamii hatuna budi sasa ya kujadili mazingira ya kijamii kama yalivyopatwa kuelezwa na Mulokozi. Anaeleza kuwa, kufikia karne ya 16 fani za kijamii zilikuwa zimekwisha enea na kufahamika katika maeneo mengi, hivyo kulihitajika kuwe na msukumo wa kijamii, kiteknolojia na kiuchuni. Msukumo huo wa kundeleza fani za kijadi ulikuwa ni wa aina tatu ambao ni;
Ukuaji mkubwa wa shughuri za kiuchumi huko ulaya, ukuaji huo ulifungamana na biashara ya baharini ya mashariki ya mbali na kuvumbuliwa kwa mabara mawili ya amerika na ukuaji wa viwanda hasa vya nguo huko ulaya. Mabadiliko haya yalizua tabaka jipya la mabwanyenye waliomiliki viwanda na nyenzo nyingine za kichumi.Tabaka hilo lilihitaji fani mpya za fasihi, lilikuwa na wakati wa ziada wa kujisomea, uwezo wa kifedha wa kujinunulia vitabu na magazeti. Hivyo tangu mwanzo ilitawaliwa na ubinafsi uliojidhihirisha kiitikadi. Kwa mfano Robinson Kruso ni riwaya ilyosawili ulimbikizaji wa mwanzo wa kibepari. Ilimhusidhs muhusika asiye staarabika aitwaye Fraiday au Juma. Ubinafsi huu ulijitokeza pia katika utungaji wake, na haikusomwa hadharani bali kila mtu alijisomea mwenyewe chumbani mwake.
Mageuzi ya kijamii na kisiasa, mabadiliko haya yalifungamana na mabadiliko ya kiuchumi. Mataifa ya ulaya yalianza kujipambanua kiutamaduni na kisiasa yaliyojitenga na dola takatifu ya kirumi. Mabadiliko hayo yalianza kujenga utamaduni wa kitaifa na mifumo ya elimu iliyo hiyaji maandishi katika lugha zao wenyewe. Mfano wa mageuzi ya kijamii na kisiasa iliyofanyika ni kama vile; Misahafu ya Dini Kama Biblia ilanza kutafsiriwa kwa lugha za ulaya, Martin Lther alichapisha  Biblia kwa lugha za kidachi miaka ya 1534. Hivyo basi inaonyesha kuwa kadiri elimu ilivyopanuka na nduvyo wasomaji wa vitabu walivyoongezeka na kufanya kuwe hadhira kubwa nzuri ya wasomaji na watunzi wa riwaya.
Ugunduzi wa teknolojia ya upigaji chapa vitabu, yaani kwa kutumia herufi iliyoshikamanishika.Ugunduzi huu uliofanywa na Johnnes Gutenberg huko ujerumani mwaka 1450 uliorahisisha kazi ya uchapaji vitabu katika nakala nyingi nakuondoa kabisa haja ya kunakili miswada kwa mikono. Bila ugunduzi huo kufanyika haingewezekana kuchapisha riwaya nyingi na kuzieneza kwa bei nafuu.Nmifano ya riwaya hizo ni kama vile; Pamela ya Samwel Richardson (1740).
Kutokana na wataalamu mbalimbali kuelezea chimbuko la riwaya ya Kiswahili, inaonekana kuwa, riwaya ni utanzu wa fasihi ambao kuzuka kwake kulifungamana na fani za kijadi pamoja na mazingira ya kijamii. Fani za kijamii kama vile, ngano, visasili, visasuli, visakale, insha, na nyinginezo zizosimuliwa bila ya kuandikwa kabla ya karne ya 16, zilichochewa na kupewa mwendelezo baada ya kukua kwa sayansi na teknolojia huko ulaya,hasa baada ya ugunduzi wa mitambo ya kupiga chapa kazi za fasihi.
MAREJEO
Madumulla, J.S. (2009), Riwaya ya Kiswahili, Historian a Misingi ya Uchambuzi. Nairobi:                                           Sitima Printer and stations L.td.
Mulokozi, M.M. (1996), Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam. TUKI.
Mhando, P. na Balisidya, (1976), Fasihi na Sanaa za Maonyesho. Dar es Salaam: Tanzania                                                                  Publishing House.
Nkwera, F.V. (1978), Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: Tanzani Publishing                                            House.
TUKI,(2004),Kamusi ya Kiswahili Sanifu.Nairobi.Kenya:Oxford University Press.
Senkoro,F.E.M.K.(2011), Fasihi Andishi.Dar es Salaam.Kauttu L.t.d.
Wamitila,K.W.(2003),Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publication. 

DHANA  NA DHIMA  YA USHAIRI WA KISWAHILI


Katika makala hii tutaeleza historia fupi ya ushairi na mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya ushairi.
Tukianza na Mulokozi (1996) anasema, wataalamu wengi wamekubaliana kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi, hasa ngoma na nyimbo zinazofungamana na ngoma.
Kabla ya karne ya 10 BK ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kughanwa  kwa ghibu bila kuandikwa.  Wataalamu hao waliojadili historia ya ushairi ni kama (Chiraghdin 1971: 7:10, Massir 1977:1  Ohly 1985:467).
Dhana ya ushairi imejadiliwa kwa kuangalia makundi mawili ya waandishi wa mashairi ya Kiswahili, makundi hayo ni kundi la wanamapokeo, na kundi la wanausasa.
Tukianza na kundi la wanamapokeo.  Wataalamu mbalimbali wamejadili dhana ya ushairi kama ifuatavyo:
Kwa mujibu wa Shaaban Robert (1968) anasema kuwa Ushairi ni Sanaa ya vina  inavyopambanuliwa,  kama nyimbo, mashairi na tenzi  zaidi ya kuwa sanaa ya vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache  au muhtasari, uliza  swali wimbo, shairi na tenzi ni nini?  Wimbo ni shairi dogo na shairi ni wimbo mkubwa na utenzi ni upeo wa ushairi pia anauliza kina na ufasaha huweza kuwa nini?  Anasema  kina ni mlingano wa sauti za herufi, na kwa maneno mengine huitwa mizani ya sauti, na ufasaha ni uzuri wa lugha, mawazo, maono na fikra za ndani  zinapoelezwa kwa muhtasari wa ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu.  Hivyo  katika ufafanuzi wake wa ushairi inaonesha dhahiri kuwa Shaaban Robert anagusia vipengele viwili maalumu yaani fani ya ushairi na maudhui ya ushairi.
Naye Mnyampala (1970) kama alivyonukuliwa na Massamba D.P.B. katika  Makala ya Semina ya Kimataifa  ya waandishi wa Kiswahili (2003) anasema ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale.  Ndicho kitu kilicho bora sana katika maongezi ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalumu kwa shairi.
Hapo tunaona dhahiri kuwa Mnyampala anauona ushairi ukiwa umejengwa na vitu viwili mahususi, ambavyo ni maneno ya hekima na sanaa yenyewe.  Tena Mnyampala katika dibaji hiyo hiyo anasisitiza juu ya sanaa ya ushairi kwa kusema:
(i)                   Shairi liwe na “poetical Swahili”  yaani Kiswahili kinachohusu mwendo wa mashairi bora.                                                                                                       
(ii)                 Shairi liwe na urari wa mizani kamili zinazohusika na ushairi wa kawaida waka lugha ya Kiswahili kisichokuwa na kashfa au matusi  ndani yake.
(iii)                Shairi liwe  na vina vinavyopatana hususani mwishoni mwa kila ubeti kwa shairi lolote zima ingawa vina vya katikati vikosane kwa utenzi wake.
(iv)               Shairi lazima liwe na muwala
(v)                 Lisizidi mno maneno ya kurudia rudia.

Kwa mujibu wa Abdilatifu Abdalla (1973) katika makala ya semina  ya kimataifa ya waandishi wa Kiswahili anasema maana ya ushari ni utungo ufaao kupewa jina  la ushairi ni utungo wowote tu bali ni utungo ambao katika kila ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada  ya chenziye,  wenye vipande vilivyoona ulinganifu wa mizani zisizo pungufu wala kuzidi na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato maalumu  na yenye lugha nyofu, tamu na laini, lugha ambayo ni telezi kwa ulimi wa kutamka, lugha ambayo ina uzito wa kifikra, tamu kwa mdomo wa kuisema, tambuzi kwa masikio ya kuisikia, na yenye kuathiri moyo uliokusudiwa na kama ilivyokusudiwa.
Kutokana na hayo yaliyokwishasemwa, tunaona kuwa dhana ya ushairi ya wana jadi imefinywa kwenye umbo maalumu lenye utaratibu wa vina na urari wa mizani ambayo kwa kweli ni dhana ya kimaandishi.
Kundi la pili ambalo limefafanua dhana ya ushairi   ni kundi la wanausasa.  Hawa wamejadili dhana ya ushairi kama ifuatavyo:
Kwa mujibu wa Wamitila (2010) anasema ushairi ni sanaa inayotambulishwa na mpangilio maalumu wa sentensi au vifungu, mpangilio ambao una mdundo maalumu  au ruwaza fulani inayounda wizani, lugha ya mkato na mafumbo pamoja na mpangilio usio wa kawaida wa vifungu fulani.
Mulokozi, (1989) anasema ushairi ni sanaa ya lugha inayoonesha au kueleza jambo, wazo  au tukio kwa namna inayovuta hisia kutokana na mpangilio  maalum wa maneno yaliyoteuliwa, kauli za mkato, picha na tamathali  na inayowasilishwa kwa hadhira kwa njia ya nyimbo au maandishi.  Kwa mujibu wa ufafanuzi huo ushairi hueleza tu, bali hudhihirisha, au huonyesha kusawiri,  anaendelea kusema ushairi huwajumuisha watu wawili au zaidi.  Kihisia katika tukio linalowagusa wote,  ukawatosa katika dimbwi la uchungu, au furaha, hasira au ridhaa, na kuwatoa tena wakiwa wameburudika na kuelimika.
Kwa sababu hii ushairi  ndiyo sanaa ya fasihi inayokaribiana  zaidi na muziki na  mara nyingi sanaa hizi mbili hufungamana.
Mulokozi na Kahigi (1979) wanamnukuu Kezilahabi kwa kusema kuwa ushairi ni tukio, hali au wazo ambalo limeonyeshwa kwetu kutokana na upangaji mzuri wa maneno  fasaha yenye mizani kwa ufupi ili kuonyesha ukweli fulani wa maisha  jambo ambalo halikutiliwa maanani katika fafanuzi la wataalamu hawa ni dhima ya fasihi na ushairi kama vyombo vya kuburudisha na kustarehesha watu.
Wataalamu hawa wanaendelea kusema kuwa ushairi lazima uguse hisi, lazima umsisimue yule anayeusema, kusoma au kuimba na  yule ausikilizaye.  Hivyo shairi lisilogusa hisi ni  kavu na butu hata  kama limetafsiriwa katika vina na urari wa midhani, shairi hilo litaishia kuhubiri tu.
Kwa ujumla wanausasa wanadai kuwa ushairi  ni sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha  na yenye muwala, kwa  lugha   ya mkato, picha au stiari  au ishara.  Katika usemi, maandishi, au mahadhi ya wimbi ili kueleza wazo au mawazo, kujifunza au kueleza tukio au hisi fulani.  Kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.
Kutokana na mawazo hayo ya washairi mbalimbali wa kimapokeo na wana usasa wote wameonesha  mambo fulani ambayo yamefanana kwa  namna moja ua nyingine.
Wote wanakubaliana kwamba katika ushairi fani na maudhui ni vitu vya muhimu kabisa na kwamba kila kimoja  kati ya vitu hivyo kina wajibu maalumu.
Pia washairi wengi huamini kwamba lugha ya ushairi lazima iwe ya mkato, yaani iweze kusema mambo mengi kwa kutumia maneno  machache.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa ushairi ni  sanaa ya lugha yenye ughunaji na yosawiri, kueneza au kuonesha jambo lenye  hisi au hali fulani kwa namna  ya kuvutia hisia katika mpangilio  mahususi wenye urari wa vizani na sauti.
Baada ya kuangalia  wataalamu mbalimbali walioelezea dhana ya ushairi, zifuatazo ni dhima za ushairi wa Kiswahili.
Ushairi husaidia kurithisha  maarifa kwa jamii, kupitia ushairi jamii inaweza kujifunza mambo mbalimbali kama vile namna ya kuepukana na magonjwa, umuhimu wa kutunza mazingira.                                                                                                           
Mfano:  shairi la Binti katika diwani ya dhifa iliyoandikwa na Kezilahabi e, Mwandishi anarithisha jamii maarifa kwa kusisitiza jamii izingatie umuhimu wa elimu: anasema
                        Soma soma kwa kujiamini.
                        Elimu ni kikata kiu,
                        Huondoa pia ukungu,
                        Pasipo njia pakawa
                        Fanya kazi utayopata,
                        Kazi ni kinga ya  heba
                        Sasa umekuwa na uwe,
                        Huu usinga na kupa
                        Na unyoya nakuchomekea nyweleni.

Ushairi husaidia kuhamasisha jamii, ushairi hutumiwa kama njia ya kuwahamasisha wanajamii katika shughuli mbalimbali. Mfano: katika utendi wa Fumo Loyongo ubeti wa kumi na tatu, anahamasisha wanajamii kuwa na nguvu kama simba, anasema:
                        “Ni mwanaume Swahili
                        Kama simba unazihi
                        Usiku na asubuhi
                        Kutembea ni mamoya.

Pia katika diwani ya Wasakatonge, shairi la Wanawake wa Afrika, mwandishi anawahamasisha wanawake kujikomboa, anasema:
                        Wanawake wa Afrika
                        Wakati wenu umefika,
                        Ungeneni
                        Shikaneni
                        Mjitoe utumwani,
                        Nguvu moja!                                                                                                                 
Ushairi husaidia kudumisha na kuendeleza utamaduni katika jamii, kupitia ushairi wanajamii wanadumisha na kuendeleza utamaduni wao na  kwa njia hii  huhakikisha kuwa unabaki hai. Mfano katika  tohara huwa kunakuwa na nyimbo zenye mafunzo kwa vijana wanaofanyiwa jando na unyago, kama vile kuandaa wanaohusika kwa majukumu ya utu uzima.
Ushairi huburudisha  hadhira, ushairi ni nyenzo kuu ya burudani, katika jamii licha ya majukumu mengine ya nyimbo, msingi mkuu ni uwezo wake wa kuweza  kuathiri hisia za wasikilizaji au washiriki wake na kuwaburudisha.  Mfano katika shairi la watoto wawili kutoka kwa mwandishi Kezilahabi Kichomi (1974 uk. 62):
            Mtoto wa tajiri akilia  hupewa mkate,
            Mtoto wa tajiri akilia hupewa picha ya kuchezea,
            Akilia mtoto wa tajiri huletewa kigari akapanda,
            Akiendelea kulia hupanda mgongo wa yaya,
            Akikataa kunyamaza ulimwengu mzima hulaumiwa.

Ushairi husaidia kukuza lugha kwa kawaida ushairi hutungwa kwa lugha nzito yenye ishara  na jazada zinazoeleweka na wanajamii wanaohusika, na kwa njia hii  hutusaidia kukuza hisia za kujitambua kwao kama watu wa kundi fulani lenye mtazamo, imani na mwelekeo fulani.
Hivyo kwa kuhitimisha tunaweza kusema kwamba aidha ushairi uwe wa kimapokeo au  wa kisasa unaonesha mambo muhimu yanayoilenga jamii husika.  Mfano katika mambo ya kidini, kisiana na kiutamaduni.                                                                                                                        
MAREJEO
Abdilatifu, a (1973), Sauti ya Dhiki, Oxford London.
Kezilahabi, E (1974), Kichomi, Heinemann; London.
Massamba, D.P.B. (2003), Utunzi wa Ushairi wa Kiswahili katika makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili (III).  Fasihi.  Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaam.
Mulokozi, M.M na Kahigi K.K. (1979), Kunga za Ushairi na Diwani Yetu, TPH, Dar es Salaam.
Mulokozi, M.M. (1989) Uchambuzi wa Mashairi:  Mulika Namba 21; TUKI, Dar es Salaam.
Mulokozi, M.M. (1996), Fasihi ya Kiswahili, chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es Salaam.
Robert, S (1968) Kielelezo cha Insha.  Nelson London.
TUKI, (2003), Makala za Semina ya  Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili III : Utunzi wa Ushairi wa Kiswahili, TUKI Dar es Salaam.
Wamitila, K.W.  (2010) Kichoche cha Fasihi Simulizi na Andishi, English Press.  Nairobi.

CHIMBUKO LA USHAIRI; UBORA NA UDHAIFU WAO.

Dhana ya ushairi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo:
Mssamba, D.P.B. (2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.”
Mnyampala (1970) anasema kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora sana maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.”
Amri Abeid (1954:1) anasema kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana.”
Encyclopedia American (EA) inaeleza kuwa ushairi ni kauli zenye hisia na ubunifu, mpangilio fulani wenye urari, uwasilishaji wa tajiriba au mawazo ya mtunzi kwa maana ambayo huibua tajiriba kama hiyo katika nyayo za wasomaji au wasikilizaji na kutumia lugha ya picha yenye wizani wa sauti.
Mulokozi na Kahigi (1982) wanasema ushairi ni “sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalum na fasaha na wenye muwala, kwa lugha ya picha, sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kuleta wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisia fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.”
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa ushairi ni kazi ya sanaa yenye kuandikwa au kuimbwa kwa kufuata kanuni za ushairi au kutofuata kanuni za ushairi ikiwa na maana kuwa ushairi waweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa ilimradi ushairi huo uwe na ujumbe.
Dhana ya chimbuko inafasiliwa na TUKI (2004) kuwa ni mwazo au asili ya kitu.
Baadhi ya wataalamu wameweza kuelezea chimbuko la ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia mitazamo au nadharia mbili ambazo ni kama zifuatazo:
Nadharia ya kwanza inadai kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu.
Na nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la jamii ya waswahili wenyewe.
Kwa kuanza na nadharia ya kwanza isemayo kuwa chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu ambayo inaungwa mkono na wataalam mbalimbali kama vile Lyndon Harries (1962) na Knappet (1979)
Kwa kuanza na Lyndon (1962) “Swahili Poetry” anatoa hoja tatu ambazo ni ushairi wa Kiswahili umetokana na Uislamu, ushairi ulianzia kwenye upwa wa kaskazini mwa Kenya hususani Lamu. Na maudhui ya ushairi wa Kiswahili yalitokana na ushairi wa Kiarabu. Utungo wa kwanza wa ushairi andishi wa Kiswahili ni Tambuka, Mwengo bin Athmani (1728)
Ubora wa nadharia hii au mtazamo wa Harries kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni kwamba umesaidia wengine kuendelea kuchunguza zaidi kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili.
Udhaifu wa nadharia hii ni kuwa si kweli kwamba ushairi wa Kiswahili uliletwa na Uislamu bali ulikuwepo hata kabla ya ujio wa Uislamu, kwani ushairi hautenganishwi na jamii husika. Hivyo jamii za waswahili walitumia Nyanja mbalimbali za ushairi katika shughuli zao mbalimbali au shughuli zao za kila siku, kama vile; shughuli za kilimo na ufugaji.
Pia ushairi wa Kiswahili ulianza karne ya 10BK na ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kughanwa kwa ghibu bila kuandikwa. Wataalam wengi wanakubaliana kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo.
Udhaifu mwingine katika mtazamo wake wa kusema kuwa ushairi ulianzia pwani ya kaskazini ya Kenya si kweli kwa kuwa waswahili walikuwepo hata sehemu nyingine kama vile Kilwa na Bagamoyo ambapo ushairi wa Kiswahili ulitumika.
Hoja ya kusema ushairi wa Kiswahili ulitokana na Kiarabu haina mashiko kwa kuwa waswahili walikuwepo hata kabla ya waarabu na walikuwa na ushairi wao isipokuwa ujio wao ulileta athari kubwa kwa kuwa ulichanganya na mambo ya dini ya kiislamu na hati.
Knappert (1979) “Four centuries of Swahili verse” anasema; “Ushairi wa Kiswahili ulichipuka kwenye upwa wa Kenya kutokana na nyimbo na ngoma za waswahili na ulianza katika karne ya 17 na pia ni ushairi wa Kiislamu wenye kuchanganya sifa za tungo za kiafrika na za kiajemi.
Ubora wa hoja hii ni kwamba, ni kweli Knappert amekubali kuwa, ushairi wa Kiswahili ulitokana na waswahili wenyewe.
Hata hivyo hoja yake ina udhaifu kwa kuwa ushairi wa Kiswahili ulianza kabla ya karne ya 10 BK na pia amejikita katika maudhui ya mambo mengine kama vile siasa, uchumi na kijamii. Vilevile amechanganya chimbuko la ushairi wa Kiswahili na Uarabu.
Nadharia ya pili inasema kuwa ushairi ni zao la waswahili wenyewe. Nadharia hii imejadiliwa na wataalam mbalimbali akiwemo Shaban Robert, Jumanne Mayoka (1993) na F.E.M.K. Senkoro, Mulokozi na Sengo.
Jumanne, M. Mayoka (1993) anasema ushairi umetokana na jamii ya wanadamu wenyewe na umesheheneza ukwasi mkubwa wa lugha ambayo imekuwa ikitumika katika hatua zote za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika historia ambayo mwanadamu amepitia, Kwa mfano kuwa msamiati uliotumika tangu enzi za kuishi mapangoni, enzi za uwindaji, ujima, utumwa, vita vya makabila, uvamizi wa wageni, ukoloni na harakati za kupambana na ukoloni hadi kupata uhuru na maendeleo yake.
Ubora wa hoja hii ni kwamba ina mashiko ndani yake kwa sababu, kila jamii ina sanaa yake na ushairi ni moja kati ya sanaa hizo ingawa inaweza ikaathiriwa na sanaa ya jamii nyingine. Pia ushairi umekuwa ukikua na kuendelea kadri jamii inavyokuwa na kuendelea.
Udhaifu wa hoja hii ni kwamba si kweli kuwa katika kipindi hicho ushairi ulikuwa tayari umesheheni ukwasi mkubwa wa lugha, na kama ulikuwa kweli umesheheni huu ukwasi wa lugha alipaswa kutuonesha huo utajiri wa lugha anaouzungumzia katika ushairi.
Senkoro (1988) anasema kuwa ushairi uliibuka pale lugha ilipoanza katika kipindi cha uhayawani (kipindi ambacho mwanadamu alipoanza kupambana na mazingira yake) kwenda katika kipindi cha urazini (maana) ili kumwezesha binadamu na mazingira yake kwa mfano, zana za kazi zilizotumika ziliwafanya waimbe kwa kufuata mdundo wa zana hizo.
Ubora wa hoja hii ni kwamba unathibitisha kuwa chimbuko la ushairi ni waswahili wenyewe, kwani umefanikiwa kueleza kuwa katika jamii yoyote ile maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii huambatana au huenda sambamba na maendeleo ya sanaa mbalimbali ikiwemo ushairi uliotumika katika harakati mbalimbali za maisha ya mwanadamu.
Pamoja na kuwa nadharia hii imeonesha kukubalika na wataalamu mbalimbali kama vile Senkoro, Mayoka na Shekhe Amri Abeid, lakini bado ina mapungufu. Hii ni kwa sababu imeshindwa kuonesha muda maalumu ambapo ushairi wa Kiswahili ulianza na ni wapi ulianza kutumika. Hili ni suala ambalo linaumiza vichwa vya wataalamu mbalimbali hadi hivi sasa, kwani hakuna mtaalamu yoyote aliyefanikiwa kuonesha ni wapi na ni lini ushairi wa Kiswahili ulianza.
Hivyo basi, kutokana na nadharia hizo mbili tunaungana na nadharia inayosema kuwa, chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la waswahili wenyewe, kwa sababu waswahili wana utamaduni wao ambao ulikuwepo kabla ya ujio wa Waarabu. Na waliutumia ushairi huo katika shughuli mbalimbali za kijamii, kwa mfano katika harusi, jando na unyago.
MAREJEO:
Knappert, J. (1979). Four centuries of Swahili Verse. Heinemann. London.
Mayoka, J.K. (1993). Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka. Ndanda Mission   Press.Tanzania.
Mulokozi, M.M. (1996). Fasihi ya Kiswahili.Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.                                                             
Senkoro, F.E.M.K. (1987). Ushairi, Nadharia na Tahakiki. DUP. Dar-es-Salaam.
TUKI. (1983). Makala ya Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili. (Toleo la III) TUKI.Dar-es-Salaam.
TUKI. (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu.TUKI.Dar-es-Salaam.

UTHIBITISHO USHAIRI WA KISWAHILI UMEPITIA MIHULA ANUAI

Maana ya ushairi.
Massamba (2003) akimnukuu Shaaban Robert (1968) anasema Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya vina na mizani, ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhtasari.
Senkoro (1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, “Nadharia na Tahakiki” anasema ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake.
Kezilahabi, (1974) katika kitabu chake cha “Kichomi” anadai ushairi ni tukio, hali, au wazo, ambalo limeoneshwa kwetu kutokana na upangaji mzuri wa maneno fasaha yenye mizani kwa ufupi ili kuonesha ukweli fulani wa maisha.
Wamitila,  (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha na kimtindo zinamwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa kifupi na kwa mkokotezo mkubwa unaoelezea hisia, tukio, ama hali kwa lugha ya mvuto.
Kwa ujumla ushairi ni sanaa ya lugha ya mkato yenye ughunaji inayosawiri, kueleza au kuonesha jambo, hisia au katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa vina na wizani wa sauti.
Baada ya kuangalia tofauti ya ushairi ifuatayo ni tafsiri ya ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa kiswahili umeelezwa na Senkoro (1988) kuwa ni ule ushairi unaotumia lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha mawazo, fikra na vionjo vya moyo wa watu wanaotumia lugha ya Kiswahili.
Ushairi wa kiswahili umefafanuliwa tena katika mitazamo mingine miwili. Mtazamo wa Kimapokeo na mtazamo wa Kisasa.
Katika mtazamo wa Kimapokeo wanadai kuwa ushairi wa kiswahili ni ule unaotungwa kwa kufuata kanuni za urari wa vina na mizani, ambazo ni kanuni za ushairi wa Kiswahili. Miongoni mwao ni wazee na vijana wa UKUTA ( Chama cha usanifu wa Kiswahili na ushairi Tanzania) Amri Abedi.
Mtazamo wa wanausasa; Ushairi wa Kiswahili si lazima ufuate kanuni za utungaji wa mashairi. Vina na mizani si vya lazima katika ushairi. (Kezilahabi, E, Mulokozi, M.M na K. Kahigi) maelezo haya yanayofafanua maana ya ushairi wa Kiswahili yana mapungufu kadhaa kama ifuatavyo;
Wanamapokeo wameshindwa kuelezea vipengele vya maudhui. Wamejikita zaidi katika vipengele vya kifani (urari wa vina na mizani) hawajaeleza waswahili ni watu gani? Mashairi haya yanazungumzia mawazo yapi?
Wanausasa wamepinga hoja tu ya wanamapokeo kuwa ushairi wa kiswahili si lazima ufuate kanuni za urari wa vina na mizani. Hawajatoa maana yao kuhusu ushairi wa Kiswahili.
Kwa hiyo, ushairi wa Kiswahili ni utungo unaotumia lugha ya kiswahili kuelezea maisha ya waswahili (watumiaji wa lugha ya kiswahili) katika Nyanja mbalimbali za maisha, wenye kusheheni fani na maudhui yanayohusu watumiaji wa kiswahili
Ama kuhusu Muhula ni kipindi fulani katika mwaka kinachohusishwa na tukio fulani pia huzingatia kigezo cha mwaka muafaka.
Mihula ya ushairi wa kiswahili. Kwa mujibu wa Kezilahabi (1983) amebainisha Mihula ifuatayo;
Muhula wa Urasimu (hadi 1885). Katika kipindi hiki kanuni za utunzi ziliwekwa na ushairi ulitawaliwa sana na mitazamo ya kidini na Kimwinyi. Mfano; wa tungo za ushairi zilizokuwepo kipindi hiki ni utenzi wa tambuka 1728 kilichoandikwa na Bwana Mwengo, utenzi wa Hamziyyah 1690 Sayyid Abdarus , utenzi wa Al-Inkishafi utenzi uliojadili maswala ya matatizo na mazingira yaliyohusu Afrika Mashariki (1810-1820). Uliandikwa na Sayyid Abdalah A. Nassir. Makala za semina ya Kimataifa ya waandishi wa Kiswahili (uk. 148-150)
Muhula wa Utasa 1885-1945. Kipindi hiki ni kipindi cha mabadiliko ya kiutawala na kielimu. Kubadilika kwa hati ya maandishi kutoka Kiarabu kwenda Kirumi. Kipindi hiki maandishi machache yaliandikwa wakat huu, mengi yakiwa maandishi ya Hemed Abdallah. Baadhi ya tenzi zilizopatikana ni Utenzi wa Vita vya Majimaji. Kanuni za uandishi wa mashairi zilianza kupotea. Makoloni ya Ulaya yalikuwa yakigawanwa Afrika (uk. 149-150)
Muhula wa Urasimi mpya (1945-1960) kipindi hiki kilikuwa ndicho kipindi cha kufufua kanuni za utunzi. Shaaban Robert, Amri Abeid Khamis Amani, M. Mnyampala, Ahmmed Nassir na wengineo. Kipindi hiki ndipo kitabu cha sheria za kutunga mashairi kiliandikwa wakati ambao kilikuwa kinahitajika sana ili kuweka kiungo kizuri na wakati uliopo. Yaani  kueleweka vizuri katika wakati uliopo (1954)
Mtindo uliotumika sana ni ule wa mizani 16 yaani 8+8 kwa kila kipande cha mshororo katika mishororo minne . Mtindo uliotumika sana na Muyaka bin Haji katika karne ya 18
Wanamapokeo waliamini kuwa shairi liliandikwa ili liimbwe wakati huo mghani Radioni Athumani Khalfani alikuwa amezoea kuimba mtindo huo na katika mahadhi ya aina moja.
Muhula wa Usasa (1967-hadi leo) ni muhula wa mtazamo mpya kimawazo kisanaa, hivyo kuna mgogoro katika uwanja wa ushairi. Kipindi hiki washairi walikuwa wanatafuta uhuru wa kisanaa.
Mgogoro juu ya kanuni uandishi wa ushairi uliongezeka zaidi.
Muainisho huu wa mihula ya ushairi kwa mujibu wa Kezilahabi, unamapungufu yafuatayo yaliyobainika;
Hujahusisha usimulizi na usimulizi, inaaminiwaka kuwa asili ya ushairi wa kiswhili ni tungo simulizi hasa nyimbo zinazofungamana na ngoma. Wataalam wanaounga mkono hoja hii ni Chiraghdin (1971), Shariff (1988), Nassir (1977) na Ohly (1985).
Pia haja zungumzia ushairi kabla ya karne ya 17. Kutokana na wataalam inaonekana ushairi wa kiswahili ulianza kutungwa na kughanwa kwa ghibu/kuandikwa karne ya 10BK.
Hajabainisha wazi muhula wa Utasa uko vipi? Kwa sababu bado washairi wengi walikuwepo kutoka Tanga, Mombasa mfano; Shaabani Robert.
Kwa mujibu wa Anord, R. (1973) mtaalam huyu ameainisha mihula ya ushairi katika vipindi vitatu kama ifuatavyo;
Kipindi cha kabla ya Ukoloni: yeye alitumia mtazamo wa matabaka. Ushairi uliokuwepo ni ule ulioakisi hali ya watu, mamwinyi na ufalme. mfano; ushairi wa Mwanakupona ulisisitiza kuwatukuza mamwinyi na wafalme. Ushairi huu wa Mwanakupona uliandikwa na Bi Mwanakupona binti Mshamu.
Muhula wa Upinzani: ni kipindi ambacho upinzani ulijitokeza katika utetezi wa Uislam na mila za jadi dhidi ya Ukristo baada ya vita vya majimaji. Kipindi hiki ushairi ulipo na hadi kilipofika kipindi cha mwaka (1930). Kipindi hiki kiliwakilishwa na Shaaban Robert.
Kipindi cha baada ya Uhuru: hiki ni kipindi ambapo washairi wengi walitunga mashairi kushughulikia  masuala ya ujenzi wa jamii mpya. Hii ni kutokana na mabadiliko ya fani ya ushairi. Mfano; mashairi ya Mohammed S. Khatibu ya Fungate la Uhuru na Wasakatonge yanasisitiza juu ya ujenzi wa jamii mpya.
Mapungufu ya Anord.R (1973) katika uainishaji wa mihula ya ushairi wa kiswahili;
Hajaonesha muda halisi kwani anaweka muda katika majumuisho. Mfano; anasema “Kipindi kabla ya uhuru” kuanzia lini hadi lini, kipindi cha upinzani ni lini hadi lini na kipindi baada ya uhuru kuanzia mwaka gani hadi mwaka gani na lini?
Hajahusisha ushairi wa kiswahili na usimulizi kama ndicho chanzo (asili) ya ushairi wa Kiswahili, kwani nyimbo zilizofungamana na ngoma.
Kwa mujibu wa Ohly,R. (1973) mtalaam huyu amegawa mihula ya ushairi katika vipindi vifuatavyo;
Kipindi cha kabla ya mwaka 1888 kwa mujibu wa Ohly; anasema kipindi hiki kilibainisha mashairi/ushairi wa aina tatu. Ushairi wa Kidini uliozungumzia masuala ya kidini. Mfano; utenzi wa Hamziyya, pamoja na ule wa Inkishafi. Ushairi wa kawaida ni ushairi ambao ulikuwa haufungamani na upande wowote isipokuwa unatoa maadili ya dunia. Ushairi wa tungo za Jadi ambazo zipo 13 baadhi ya hizi tungo za jadi ni shairi, utenzi, wimbo, ukwafi, zivindo, kimai, Hamziyya, Inkishafi au Dura mandhuma.
Kipindi cha 1888-1918; mtalaam anaeleza kuwa katika kipindi hiki kumekuwapo na ushairi wa maelezo usiofungamana na siasa. Ushairi wa kutathimini, ushairi wa kupinga ukoloni mfano; Saadan Kandoro, Amri Abeid pamoja na Shaaban Robert. Mashairi ya vikaragosi ambayo ni ya wale wenye hali ya chini/duni. Mfano; mashairi ya Shaaban Robert, mashairi ya S. A. Kandoro.
Kipindi cha 1918-1949; Ohly anasema kuwa kipindi hiki kilitawaliwa na fasihi ya ukoloni. Mikondo ya ushairi iliyokuwepo kipindi hiki ni ushairi wa maadili, ushairi wa malimwengu, na tafsiri kama aliyoifanya Nyerere J.K. (1968) katika ushairi wa kidrama wa kazi ya Shakespeare ambazo ni kazi za mabepari wa Venis. Mfano wa ubeti;
            Nerissa: Naam nitampa bure bila ficha,
                          Poveeni na Jesika kutoka kwa myahudi,
                          Hati maalum ya hiba baada ya kifo chake,
                          Ataacha kwenu nyingi kila atakacho.
Mapungufu ya uainishaji wa Ohly (1973) yanakumbwa na changamoto zifuatazo;
a.       Hajatueleza uhusiano uliopo kati ya ushairi simulizi na ushairi aliouainisha katika vipindi vyake.
b.       hajaeleza baada ya muhula wa 1918-1949 mashairi yaliyoendelea mapaka leo yana maudhui gani
Baada ya kuangalia wataalam hawa katika kuainisha vipindi vya ushairi tunabaini kuwa mihula ya ushairi inaweza ikagawanywa kama ifuatavyo;
Muhula wa usahiri simulizi mpaka 1500. Muhula huu unatueleza kuwa asili ya ushairi unaonyesha kuwa ni Ngoma na nyimbo ambazo zinafungamana na ngoma. Mfano; utenzi / tungo za Fumo Liyongo.
Muhula wa Urasimu 1500-1890; kipindi hiki cha ushairi kilitambulika kwa kuwepo kwa tungo za utenzi wa Tambuka 1728, Utenzi wa Hamziyya 1644 na utenzi wa Al-Inkishafi 1820. Hiki kipindi ambacho kanuni za utunzi wa ushairi zilitumiwa kwa kiasi kikubwa. Kutokana na sababu hiyo pia kipindi hiki kilipewa jina la kipindi cha Utasa hii ni kwa mujibu wa Kezilahabi.
Muhula wa Mzinduko na Urasimi mpya 1946-1967 kutoka kipindi cha utasa ufufuo wa kanuni na mwongezeko wa kazi za ushairi zilionekana. Mfano; 1957 kitabu cha sheria za kutunga mashairi cha Amri Abeid kilichapishwa. Washairi kama vile M. M. Mlokozi na M. Mnyampala, Kandoro. S. Hivyo ikaonekana kazi za ushairi zimezinduka.
Muhula wa Mageuzi na Majaribio 1968-hadi leo. Kipindi hiki kinaonesha majaribio na migogoro mbalimbali juu ya kujadili kanuni za kutunga mashairi (ushairi). Majaribio hayo yamefanya kuzuka kwa ushairi mpya ujulikanao kama ushairi wa Mavue (masivina, huru, mlegezo) aina ya Bongo Flava, ambapo kuna uimbaji na utendaji.

NADHARIA ZA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA

Katika taaluma ya fasihi simulizi, suala la kuwa na mitazamo tofautitofauti miongoni mwa wataalamu ni kitu cha kawaida tangu kale. Fasihi simulizi kiulimwengu imekuwa ikitazamwa na kuchambuliwa kwa nadharia kadhaa tangu zamani. Katika bara la Afrika kuna wataalamu wengi kutoka ndani na nje ya bara hili waliotoa michango yao kadhaa katika kuichambua fasihi simulizi ya kiafrika (hasa kipengele cha ngano). Kwa ujumla nadharia hizi zinaonekana kujumuisha hata ngano za Kiswahili. Kwa hiyo hapa katika kuzijadili nadharia hizo tutachukulia kuwa nadharia hizo baadhi kati yake zinaweza kutumika katika kuchambua ngano za Kiswahili. Okpewho (1992:164-181) na pia Finnegan (1970:315-334) wanajadili nadharia mbalimbali zinazolinda fasihi simulizi za kiafrika hasa ngano kama ifuatavyo:
Mosi, nadharia ya ubadilikaji taratibu, (Evolutionism). Nadharia hii iliasisiwa na mwanabiolojia wa Kiingereza Charles Darwin na baadaye kuungwa mkono na wananadharia wa Kiingereza kama Edward Burnet Tylor, James George Frazer na Andrew Lang. Pamoja na kwamba asili ya nadharia hii ni mawazo ya kisayansi hasa biolojia, wanafasihi simulizi wanaitumia wakidai kuwa masimulizi tunayoyasikia hivi leo ni ubadilikaji wa taratibu kwa miaka mingi. Wataalamu hudai kuwa tafiti nyingi zinaonesha kuwa masimulizi mengi ya kiafrika hasa ngano hufanana kwa kiasi fulani, hii ni uthibitisho kuwa masimulizi haya yana asili moja kwa miaka mingi iliyopita. Inasemekana kuwa usimulizi wa msingi wa ngano hizi ulikuwa mmoja lakini kutokana na ubadilikaji taratibu kila jamii imekuwa ikiongeza vikorombwezo kadhaa katika masimulizi kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ili kuhahikikisha kuwa masimulizi haya yanabaki imara, jamii zimekuwa zikiaminishwa kuwa masimulizi mengi ni ya kweli lakini katika hali halisi, masimulizi haya hutokana na kuendelea kukarabati masimulizi ya mwanzo.
Nadharia hii ina udhaifu katika kuamini kuwa fasihi simulizi za kiafrika zinachukuliwa kuwa hazina mwenyewe, lakini ukweli ni kwamba fasihi simulizi za kiafrika ni mali ya jamii nzima, japo si kweli kwamba kila mtu katika jamii anaweza kuwa fanani kwa kiwango kile kile sawa na fanani mwingine.
Nadharia ya msambao au uenevu  (Diffusionism). Nadharia hii iliasisiwa na wataalamu kama Jacob na Wilhelm Grimm, baadaye mawazo yao yakaendelezwa na Max Muller. Mtaalamu mwingine ni Mmarekani Steve Thompson. Pamoja na kuwepo tofauti ndogondogo za wataalamu wa nadharia hii, mawazo yao yanalenga kueleza kuwa kuna kitovu cha fasihi simulizi dunia nzima. Kwa sababu ya jamii kuingiliana kutokana na sababu mbambali, masimulizi haya yalianza kuhama kutoka jamii moja hadi nyingine hasa kutoka kwenye jamii zilizostaarabika kimaisha kwenda kwenye jamii ambazo hazijastaarabika. Waataalamu hawa walisema kwamba kukitokea kufanana kati ya hadithi moja toka jamii mbili tofauti basi jamii hizo zilipata kuwasiliana na kuathiriana kwa upande wa utamaduni. Hapa wataalamu kama Jacob na Wilhelm walisema kuwa kama kuna kufanana kokote kwa ngano za kiafrika na ulaya, basi ngano za kiafrika ni chipukizi toka kwa wazazi wenye utamaduni wa India na Ulaya.
Tukichunguza ngano za Kiswahili kwa jicho la nadharia hii, tunaweza kusema kuwa ngano nyingi zinaonekana kufanana kutoka jamii mbalimbali za waswahili hivyo kuna uwezekano wa kuwepo kwa kitovu cha usimulizi huu katika jamii fulani. Lakini nadharia hii ina upungufu mkubwa hasa kwa kupuuza utu na utamaduni wa mwafrika, inapodai kuwa mwafrika alikopa ngano kutoka kwa mzungu na mhindi inaelekea kusema kuwa mwafrika kabla ya kuwa na mahusiano na watu hawa hakuwa na utamaduni suala ambalo ni la kibaguzi zaidi.
Nadharia ya kisosholojia. Nadharia hii iliasisiwa na Bronislaw Malinowski (1922, 1926) na kuwa na wafuasi kama Edmund Leach, Raymond Firth, William Bascom na kadhalika. Mtazamo wa nadharia hii ni kuwa ngano za kiafrika zipo na kuibuka kwa sababu ya utumizi katika jamii. Watafiti hawa kama wanasosholojia, waliamua kuchunguza vipera vya fasihi simulizi (na ngano zikiwemo) kwa upekee wa kila jamii. Walichunguza mila na desturi kwa kuzingatia uamilifu wake katika jamii. Wataalamu mbalimbali kwa kutumia nadharia hii waligundua kuwa ngano za kiafrika zina majukumu muhimu katika jamii husika kwa mfano, Jan Vansina katika kuzijadili simulizi za utawala wa Waganda aligundua kuwa simulizi hizo zinaakisi utawala wa kurithi unaolinda umoja wa jamii ya Waganda. R.G. Willis katika kuchanganua ngano za kihistoria za Wafipa wa Tanzania, anatumia ufafanuzi wa kiishara kugundua mihimiri miwili ya kimaendeleo katika jamii. Adward Shorter (1969) alifanya utafiti kwa Wakimbu wa Tanzania akagundua kuwa ngano za Wakimbu ni muhimu sana kwa kuhifadhi vipindi mbalimbali vya kihistoria katika jamii husika.
Nadharia hii katika ngano za Kiswahili tunaweza kusema kuwa maisha ya jamii za waswahili ndiyo yanayozifanya ngano ziwepo kutokana na matumizi mbalimbali kijamii. Kazi za ngano katika jamii za waswahili huwa mhimili wa kuwepo ngano hizo bila kupotea.
Nadharia ya urasimi (formalism). Kwa kiasi kikubwa nadharia hii ilikuja kupiku ile ya msambao au uenevu. Zote zililenga kuvunjavunja ngano ili kuona vipengele vinavyoiunda. Wakati nadharia ya msambao ikilenga kuivunjavunja ngano katika vipengele vyake na hatimaye kuanza kutafuta mahali ilipoanzia na hatimaye kuunda ngano chanzi, nadharia ya urasimi yenyewe iliona huu ni upotezaji wa muda na nguvu kwani yote haya yaliishia kuleta utata kimgawanyo. Wanaurasimi wao waliona kuna haja ya kuchunguza jinsi vipengele hivi vya ngano vimepangika kimfuatano katika kuiunda ngano yenyewe kuliko kuanza kuhangaika kutafuta dhamira na hatimaye kusema chimbuko la ngano. Mwaasisi wa nadharia hii ni mrusi aitwae Vladimir Propp (1928) na baadae kufuatiwa na Eleazer Meletinsky, Marion Kilson na Alan Dundes. Kwa kupanua mawazo ya Propp, Dundes (1971) baada ya kuzichunguza ngano za Uganda hasa zile zinazohusisha wahusika wajanja kama sungura na kobe, aligundua kuwa ngano hizi zina dhima tano. Mosi, zile za urafiki zinazoonesha umoja na mshikamano katika kudumisha urafiki, pili zile za mvutano unaolenga kupima urafiki. Tatu, zile ngano zinazoonesha kuharibu urafiki. Hizi ni ngano zinazoonesha kundi moja la urafiki kuonesha hali ya kuharibu uaminifu katika urafiki hasa kwa kuwadanganya wenzao. Nne, ngano zinazoonesha ugunduzi yaani upande wa urafiki uliodanganywa hugundua ujanja na uongo uliofanywa na kundi jingine katika kuharibu uaminifu. Tano, ni ngano zinazoonesha mwisho wa urafiki.  Ngano hizi huonesha hatima ya kuvunjika kwa urafiki wa makundi na mara nyingi huishia kutoa adhabu kwa mwanzilishi wa uhasama.
Nadharia hii katika ngano za Kiswahili tunaweza kusema, inamaanisha kuzielewa ngano hizi kwa kuchunguza jinsi ngano hizi zinavyoweza kuvunjwavunjwa katika vipengele vyake na hivyo kubainisha muundo wake.

Nadharia ya uhulutishi (hybridization). Nadharia hii ina wafuasi wengi wa kiafrika kwa mfano Ngugi wa Thiong’o, Chinua Achebe, Frantz Fanon na wengine. Mtazamo mkuu wa nadharia hii ni kuangalia namna ambavyo nadharia zingine zinaweza kufaa na kushirikiana katika kuchunguza fasihi simulizi za kiafrika. Hawa walilenga kuchunguza fasihi simulizi ya mwafrika kwa kuangalia uzuri unaojitokeza katika kazi za waafrika wenyewe. M.M.Mulokozi ni mfuasi wa nadhari hii kwa Tanzania. Mawazo ya wanauhulutishi yanajibainisha kwa kutoa matamko kadhaa wanayoyatoa kuihusu fasihi simulizi ya mwafrika, kwa mfano wanasema kuwa kuna haja ya kutojali mwonekano na uzuri wa nje wa fasihi na kujali zaidi utendekaji ambao umejikita kwenye utendaji halisi wa msanii na hadhira yake kifani na kimaudhui, utendekaji unatakiwa uwe na uwili unaokamilishana yaani usielekee tu kwenye utamu bali uwe sanjali na hadhira na mazingira yao, ni kosa kubwa kwa waafrika kuiga mambo bila kuchukua tahadhari ya kujua kama wayaigayo yanawafaa katika jamii zao, pia fasihi simulizi si sanaa ya kimapokeo isiyo na upya wowote bali inapaswa kutiwa ubunifu ulio hai.
MAREJEO
F. E. M. K. Senkoro (1982) Fasihi. Press and Publicity Centre. Dar es Salaam.
F. Ruth (1970) Oral Literature in Africa. Oxford: Clarendon Press
K. W. Wamitila (2004) Kichocheo cha Fasihi, Simulizi na Andishi. Focus Publications Limited: Nairobi
M.M. Mulokozi (1989) Tanzu za fasihi simulizi. Katika Mulika. Na 21
M. Msokile ( 1993) Misingi ya Uhakiki wa Fasihi. E.A.E.P. Nairobi
P.Mhando na N.Balisidya (1976) Fasihi na sanaa za maonyesho. T.P.H. Dar es Salaam
S. Okpewho (1992) African Oral Literature. Backgrounds, Character, and Continuity. Indiana University Press. U.S.A


MOTIFU YA SAFARI NA MSAKO NDIZO HUWA MWEGA MKUU WA DHAMIRA KATIKA FASIHI YA WATOTO NA VIJANA. “MARIMBA YA MAJALIWA

Kwa kujadili swali hili  tutaanza kuelezea maana ya fasihi, fasihi ya watoto, na maana ya motifu, na maaana ya dhamira. Kisha katika kiini cha swali letu tutachambua motifu mbalimbali  za safari na msako kama zilivyo jitokeza katika kitabu. Baada ya hapo kuonyesha dhamira mbalimbali
Wataalamu mbalimbali wameelezea maana ya fasihi. Mulokozi ( 1996:3) akimnukuu Egletoni (1983:20-21), anasema fasihi ni sanaa ya lugha yenye ubunifu bilakujali kama imeandikwa au laa.
Mulokozi mwaka (1996),  anasema ni sanaa ya lugha inayoangalia maisha na mazingira halisi. Anaendelea kusema kuwa ni sanaa ya lugha yenye ufundi wa hali ya juu ili kuweza kuwasilisha mawazo aliyonayo mtu kwa njia inayoweza kuathiri kwa kutumia sanaa hiyo  kimaandishi au  kimazungumzo.
TUKI (2004), wanasema mtoto ni mtu mwenye umri mdogo, katika maana hii hajatueleza umri huo ni wa kuanzia miaka mingapi hadi miaka mingapi lakini kutokana na maana hii Mulokozi (2008:338), anasema fasihi ya watoto na vijana ni ile fasihi inayorejelea matini au kazi ambazo kimsingi hadhira yake ni watoto na vijana, na hii ni kati ya umri wa miaka 0-10 na 11-17. Hivyo fasihi ya watoto na vijana huhusisha kazi zinazowahusu bibadamu kati ya miaka 0-17. Na kazi hizo zaweza kuwa riwaya, Hadithi fupi, Tamthilia au Ushahiri.
Motifu- Ni dhana au jambo linalojirudiarudia katika kazi ya fasihi. Ambacho kinaweza kuwa cha kifani au kinaudhui. Mfano wa motifu ni Motifu ya safari.
TUKI (2004), dhamira ni kiini cha jambo au habari iliyosimuliwa ama kuandikwa hasa katika fasihi
Madumulla (2009), Dhamira ni wazo kuu katika kazi ya fasihi. Kwa ujumla wote wanazungumzia jambo au  wazo kuu katika fasihi, Hivyo tunakubaliana na fasihi zote hapo juu. Marimba ya Majaliwa ni hadithi iloyoandikwa na Edwini Semzaba mwaka (2008) ambayo inaelezea kuhusiana na marimba ya Majaliwa iliyopotea. Mwandishi ameonyesha jinsi Majaliwa alivyokuwa anatafuta marimba yake mpaka akaipata. Majaliwa alisafiri kwa kutumia njia mbalimbali kama vile ungo, fagio, na maumbo ya samaki akizunguka Tanzania nzima akisaka marimba ya nyuzi ishirini (20). Alianza Mafia, akaenda Zanzibar, Tanga, Moshi na Arusha,Iringa, Mwanza, Kigoma, na miji mingine mingi. Na Kongoti bingwa wa Taifa wa Malimba akimchenga kila mara huku akinga’nga’nia Malimba ya Majaliwa ili amzuie kushinda na ashinde yeye na bila Marimba yenye ishirini (20) hakuna ushindi.
Kuanzia mwanzo hadi mwisho wa kitabu tunaona Majaliwa alisafiri sehemu mbalimbali hadi kufikia kiwango cha kuzunguka nchi nzima huku akimsaka Kongoti ili aweze kuilejesha Marimba yake. Safari ya Majaliwa ilianzia mafia mkoani pwani. Hii ni baada ya kuchukuliwa Marimba yake na watu ambao awali hakuwafahamu na baadae walikimbia kichakani (ukurasa wa 2). Kwa kuwa marimba nguvu zake ziliambatana na nguvu ya kuzimu, usiku wa manane marehemu bibi yake mzaa mama alimjia ndotoni na kumwambia majaliwa kuwa Kongoti Nachienga ndiye aliiba Marimba yake kwa wasiwasi wa kushindwa wakifika Dodoma kwenye mashindano ya marimba ya kitaifa. Katika upande wa kuzimu babu yake Majaliwa mzaa baba yake yupo upande wa Kongoti (ukurasa 3)
Safari ilianza rasmi usiku wa manane kisiwa cha mafia katika ufukwe wa kilindoni wa Bahari ya Hindi. (ukurasa 5). Walisafiri huku bibi yake akiwa katika umbo la samaki ( nguva na papa) (ukurasa 5) hadi Zanzibar ( ukurasa7-10). Akiwa huko Majaliwa aliendelea kumsaka Kongoti bila mafanikio (ukurasa 11). Majaliwa anaendelea na safari kuelekea Tanga. Wanatumia aina mbalimbali  za usafiri kama Ungo, Ufagio, Chai maharage, na basi mfano ukurasa (21,22 na 105). Majaliwa anakumbana na misukosuko mbalimbali baharini hatimaye anafika Tanga, lakini juhudi zake hazimpi mafanikio (sura ya 7-11). Majaliwa baada ya kusikia kwamba Kongoti alikuwa anaelekea Kilimanjaro alianzisha safari ya kuelekea huko ili aweze kuitwaa marimba yake sura ya (11-17) kwa usafari wa basi (ukurasa 46). Kutokana na misukosuko mbalimbali Majaliwa anachelewa. Kilimanjaro alikuta mashindano yamekwisha na Kongoti sasa anaelekea Arusha. Majaliwa nae ili kuisaka marimba yake aliamua kumsaka Kongoti lakini pasipo na mafanikio yoyote.
Baadaye Majaliwa alisafili kwenda Singida ( sura 26-27) baadaye Kondoa kwenda Tabora( sura ya 27-30) Pia Tabora kwenda Shinyanga. Katika safari zote hizo Majaliwa hakufanikiwa kutwaa marimba yake lakini hakukata tamaa aliendelea na safari ya msako ukurasa 239.
Majaliwa anaendelea na safari kutoka Shinyanga kwenda Mwanza baada ya kufika alishuka kwenye ndege na kupanda daladala kuelekea Mwanza (ukurasa131) baada ya hapo Majaliwa alisafiri kuelekea Butihama baadaye kurudi Mwanza kwa kujionea maeneo mbalimbali ya kihistoria (ukurasa wa 138-140) Wakiwa katika usafiri wa meli Majaliwa alivamiwa na Kongoti. Akapambana nae ili airejeshe marimba yake lakini Marimba ile ilitumbikia ziwani (ukurasa 141) Bibi yake alipotokea akamwelezea kisha akayafuatilia na kumwambia kuwa hayakuwa yenyewe. Wakatembelea sehemu mbalimbali za kihistoria za Mwanza maeri ilifika Kemondo Bukoba kagera ambapo palikuwa na mashindano pia na Kongoti angekuwa miongoni mwao alisafiri sehemu mbalimbali za karagwe kwa basi kutokana na ulinzi mkali aliondoka kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria (ukurasa 151)
Majaliwa aliendelea na safari ya kuelekea Kigoma (ukurasa 155) ambapo alitembelea sehemu mbalimbali za vivutio vya watalii baadaye mashindano yalifanyika hoteri ya Lake Tanganyika ambapo alipata nafasi ya kufanya ufunguzi na hakupata pesa nyingi hapo usiku walisafili kwa ungo kupitia Mbozi na milima ya mrengi baadaye Mbeya ambapo mashindano yalifanyika Kileleni lodge ambapo alitumia njia mbalimbali na kuipata marimba lakini haikuwa yenyewe (ukurasa 175) safari ya usiku ilikuwa ni kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria kuamkia Iringa ambapo Kongoti angatumbuiza kwenye maadhimisho ya shujaa Mkwawa (ukura wa 187) Baadaye Kidatu Njombe, Rudewa hadi Manda. Baadae Mji wa Tunduma Mola tena Mwanjerwa alisikia Kongoti bado anapiga marimba aliamini kuwa bado ana marimba yake (ukurasa 197)
Safari ya Majaliwa huko Mbeya kwenda Songea kwa basi la Scandinavia (ukurasa 198) Mashindano ya Ruvuma Lindi na Mtwara pia wakiwa Ruvuma walitembelea sehemu mbalimbali za kihistoria (ukurasa 200-205), Baadaye Ndanda, Newala, Mtwara, Mnazi bay, Lindi (Tengeru) (ukurasa 205) Baadaye ukumbi wa mkorosho mpya ambapo mashindano yalifanyika lakini majaliwa hakupata nafasi ya kumsogelea Kongoti (ukurasa wa 208) kwa usafiri wa Ufagio walienda Rufiji hadi Mafia, Mkuranga,Dar es salaam, Temeke,mwenge, Rugalo, Bagamoyo na sehemu mbalimbali za Dar es salaam (ukurasa 211).
Kutoka Dar Es Salaam alifunga safari yake hadi Morogoro (ukurasa 212) kwa usafiri wa basi baada ya kupita sehemu mbalimbali Majaliwa alifanikiwa kuikuta Marimba Mjini Morogoro akiwa katika harakati za safari ya kuelekea katika shindano la kitaifa huko Dodoma ilikuwa baada ya kubadilisha marimba katika sinia la ukaguzi hapo tena Majaliwa alianza kujiandaa kusafiri kwa basi kwenda Dodoma kwenye mashindano ya kitaifa pamoja na misukosuko ya kukatika kwa daraja (ukurasa 230) Baadae aliingia Dodoma kwa kupitia Chamwino Dodoma Mjini baadaye Milimani ambapo mashindano yalifanyika hoteli ya Milimani huko Dodoma na kuibuka Mshindi wa kuwabwaga wenzake wote pamoja na adui yake Kongoti na kukamilisha ndoto zake za kuwa bigwa wa Taifa.
Maana ya ujasili Kwa mujibu wa TUK (2004), hali ya kukabili jambo hofu uhodari na ushujaa. Ujasiri ni dhamira kuu katika kitabu hiki ambayo imejitokea katika motifu zote na misako ambayo imeandikwa katika kitabu hiki majaliwa ameonesha kuwa jasiri kuanzia mwanzo wa hadithi pale anapoanza kutafuta marimba yake iliyoibwa akisaidiwa na bibi yake. Hili limeonekana katika sehemu mbalimbali mfano:- katika ukurasa wa 72 sura ya 17 ambapo majaliwa anapambana na dereva taski baada ya kutaka kumwibia majaliwa pesa zake wakati wakimtafuta kongoti aliyekuwa kwenye pikipiki.
“Majaliwa akiwa ameshika jiwe lake la rubi alimpiga nalo Yule dereva kwenye macho yake yote mawili mara mbili”
Mfano mwingine ni pale majaliwa alipopambana na kongoti mlenzi wakinyang’anyana marimba majaliwa alikuwa mtoto mdogo lakini aliweza kukabiliana na kongoti ambaye alikuwa mtu mzima. Hili limeoneshwa katika ukurasa wa 141 sura ya 34.
Nalianza kukamatana na kuangushana na ingawa alikuwa mtoto tu, uchungu wa kudhulumiwa marimba yake ulimjaza ari na akachuana kishujaa”  
Hivyo basi kwa kuangalia hiyo mifano tunaona majaliwa alikuwa jasiri na mwandishi alionesha hili kama dhamila kuu
Dhamira nyingine ni Imani za kishirikina. Imani kwa mujibu wa Kamusi TUKI (2004), ni mambo anayoyakubali mtu kuwa ni ya kweli na anayopaswa kuheshimu, haswa katika dini, au itikadi. Ushikirina ni tabia ya kuamini mambo ya uchawi, mizimu, nk. Katika kitabu hiki dhamira ya imana ya kishirikina imejijenga sana katika motifu ya safari na msako iliyojitokeza katika kitabu hiki mfano katika kitabu hiki mwandishi alionyesha hili pale majaliwa alipokuwa anasafiri kwa njia ya kishirikina kama vile ungo, fagio, pia kuna wakati mwingine alikuwa anasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kufumba macho na kufumbua. Mfano mwingine ni ule kusafiri kwa ungo imeoneshwa (ukurasa wa 52), Bibi alimwambia Majaliwa apande kwenye Ungo.
“ Bibi alimwambia mjukuu wake sasa na wewe panda kwenye ungo” .
 Pia kusafiri kwa ufagio ( ukurasa wa 105) Majaliwa alimletea bibi fagio uliokuwa umeachwa kwenye takataka.
 “ Haya panda nyuma”
Kufumba na kufumbua wakajikuta wako angani.
Dhamira nyingi ni Rushwa. Rushwa ni fedha au kitu cha dhamani kinachotolewa na kupewa mtu mwenye madaraka ya kitu fulani ili mpaji apatiwe upendeleo. Katika kitabu hiki rushwa ilijitokeza pale ambapo Majaliwa alimpa fedha kwa sababu hakuwa na kibali cha kuingia sehemu za utalii ili aweze kumwachia. Hili limeoneshwa ukrusa wa 66
“ Majaliwa alipoangalia saa iliyotundikwa ukutani na kuona ni saa tano, alibadilisha uamuzi wake na kuongeza dola moja, hapo askari hakusema kitu”.
Hilo pia limeoneshwa katika ukurasa wa 213 sura ya 54.
 Tamaa  ni hamu kubwa ya kupata kitu au shauku au matarajio ya kupata kitu. Hili mwandishi pia amelibainisha kwa kuanza na Majaliwa ambaye yeye  alikuwa na tamaa ya kupata marimba yake iliyochukuliwa na kongoti kiasi cha kuamua kujitosa na kuanza kutafuta kwa kupitia hali  mbalimbali ingawa alikuwa ni mtoto. Tamaa pia imeoneshwa pale ambapo dereva teksi alitamani dora za Majaliwa alipokuwa anamwendesha mpaka akapata upofu kwa kupigwa na Majaliwa. Pia bibi alihadithia hadithi moja ambayo ilikuwa inaonyesha jinsi ambavyo tamaa ni mbaya ukurasa wa 123-126.
“ Bibi akamuuliza Majaliwa hadithi inakufundisha nini? Majaliwa anajibu Tamaa ni mbaya”. Katika ukurasa wa 72 dereva teksi aliona pesa za majaliwa na kuzitamani hivyo akampeleka porini. Dereva anamwabia,” toa pesa zote ulizonazo haraka”
Madhara ya kutokuwa mtiifu .Hili pia mwandishi amelionesha katika kitabu chake pale ambapo majaliwa alikuwa anakiuka maagizo ambayo alikuwa anapewa  na bibi yake na kupata madhara. Hili mwandishi amelionesha katika ukurasa wa 50 ambapo bibi  anamwambia majaliwa.
 siku zote utii ni bora”. ‘Si nilikukataza kula kitu chochote kupitia kinywani’
.Hapo ndipo Majaliwa akakumbuka alikula mayai kwenye tumbo la nyangumi.  Bibi akasema
“ hilo ndilo kosa ndio maana Rubi haikufanya kazi yake name nikakupa adhabu ya kuwa peke yako usiku wote wa jana.
Pia Bibi alimwadithia Majaliwa Hadithi ya madhara ya kutokuwa mtiifu katika ukurasa wa 169-171 ambayo lkimuelezea mvuvi ambaye alikosa utiifu na mwishowe akakosa utajiri kwa ajili hiyo.
Dhamra nyingineyo ni ile ya umuhimu wa kujua historia mbalimbali ya maeneo katika nchi. Hili mwandishi amelionesha wazi kwani limeoneshwa na kujengwa dhamira na motifu ya safari kwani katika safari ambazo Majaliwa alizifanya ndipo hapo aliweza kujua historia za sehemu mbalimbali alizosimuliwa na bibi yake. Kwa ujumla kulikuwa na hisoria ya mapango ya Amboni Tanga, Kondoa Iringa,  mji wa Tabora, hisotria ya ngome kongwe, Kaburi la Abeid Amani Karume, Wangoni. Makaburi ya watu waliokufa kwa ajili ya Treni, Meli iliyozama ya MV Bukoba na sehemu nyinginezo.
Pamoja na kuwepo na dhamira hizo hapo juu zilizoelezwa kwa mapana na marefu kulikuwepo pia dhamira nyinginezo ambazo zilizokuwepo katika kitabu hiki. Dhamira hizo ni pamoja na wizi, wivu, mashindano, kujikinga na ukimwi, chuki, nafasi ya mwanamke katika jamii, Ukombozi, Elimu, Ukatili, Umoja na mshikamano na hali ngumu ya maisha. Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kuwa mwandishi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujadili masuala mbalimbali yaliyoko katika jamii hasa jamii yetu ya Kitanzania.

MAREJEO:
Madumulla, S. (2009), Riwaya yaKiswahili: Mature Educational Publishers Lited.
Mulokozi, M. M. (1996), Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Dar Es
 Salaam.
Semzaba, E. (2008), Marimba ya Majaliwa. E&D Publishers Limited:Dar Es Salaam.
TUKI (2OO4), Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili: Dar Es Salaam.


KWA KIASI KIKUBWA FASIHI HUTAWALIWA NA FANTASIA ILI KUNOGESHA

USOMAJI. MAELEZO KWA KUTUMIA KITABU CHA MARIMBA YA MAJALIWA

Fasihi inafafanuliwa na Wamitila (2003) kwa kueleza kuwa ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kwa usanii na inayowasilisha suala fulani pamoja kwa njia inayoathiri, kugusana kuacha athari fulani na kuonyesha ubunilizi na ubunifu fulani na zinazomhusu binadamu. Kazi hizi za fasihi huweza kuwasilishwa kwa njia ya mdomo yaani fasihi simulizi au kwa njia ya maandishi yaani fasihi andishi. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa fasihi ni tawi la kisanaa litumialo lugha kama nyenzo kuu ili kufikisha ujumbe katika jamii lengwa.

Pia Wamitila (2003) anaeleza kuwa fasihi ya watoto kuwa hutumiwa kuelezea fasihi maalumu inayoandikwa kwa ajili ya watoto.Hii ni fasihi ambayo ni tofauti na ngano na hurafa.Mifano ya kazi za watoto ni kama vile Ngome ya  Mianzi ya M.Mulokozi, Yatima na Zimwi la leo ya Wamitila  na Mwendo ya Lema.

Wamitila (kaishatajwa) anaeleza kuwa fantasia ni sawa na njozi, njozi ni dhana inayotumiwa kuelezea kazi ya fasihi ambayo ina sifa ambazo zinakiuka uhalisi.Anaendelea kufafanua kuwa ni kazi yenye sifa za kindotondoto au kutaka kuamilisha hali isiyo ya kawaida. Njozi hupatikana sana katika maandishi yanayolenga hadhira ya watoto.Sifa za kinjozi huweza kupatikana katika fasihi inayohusishwa na matapo mbalimbali ya kifasihi.Hutumiwa kueleza kazi za kinathari ambazo huwa na mandhari ya ajabu, matukio magumu kukubalika katika hali ya kawaida na hata wahusika wasioweza kupatikana katika uhalisi. Kutokana na fasili hiyo ya Wamitila tunaweza kusema kuwa wahusika katika kazi zenye fantasia ni wahusika kama vile mazimwi, mashetani ,majini na vitu vingine ambavyo havidhaniwi kuwepo katika jamii, yaani haviwezi kupatikana katika uhalisia .
Ifuatayo ni historia fupi ya kitabu cha Marimba ya Majaliwa.
Marimba ya Majaliwa ni kitabu kilichoandikwa na Edwin Semzaba (2008), kinachoelezea harakati za kutafuta marimba ya Majaliwa yenye nyuzi ishirini, iliyoporwa na Ngongoti aliyekuwa bingwa wa kupiga marimba.Kitabu hiki kinahusisha msako wa marimba hiyo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, na hatimaye Majaliwa alifanikiwa kupata marimba yake na kushiririki katika mashindano ya kumtafuta bingwa wa kupiga marimba huko Dodoma ambapo Majaliwa aliibuka mshindi wa shindano hilo.

Ufuatao ni uchambuzi wa  baadhi ya fantasia zilizojitokeza katikakazi ya fasihi kama katia kitabu cha Marimba ya Majaliwa. Katika uchambuzi wa fantasia, tumejaribu kuziweka fantasia katika makundi tofauti tofauti.Makundi hayo ni kama vile fantasia zinazohusu usafiri, fantasia zinazohusu utokeaji tofauti tofauti wa bibi pamoja na umbo lake,fantasia zinazohusu jiwe la rubi, fantasia zinazohusu utokeaji wa babu na nyinginezo.Kwa kuanza na fantasia zinazohusu usafiri:-
Mwandishi Semzaba ameonyesha njia mbalimbali alizokuwa akizitumia Majaliwa na bibi kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine ambazo hazikuwa za kawaida katika maisha halisi ya binadamu.Njia hizo za ajabu alizokuwa akizitumia ni pamoja na :-
Kutumia ufagio, mfano (uk.27) alitumia ufagio kueleka uwanja wa kimataifa wa mifagio, (uk.103) alitumia ufagio kwenda mapango ya Amboni,(uk. 208) alitua uwanja wa Kigamboni kwa ufagio.

Kutumia ungo, Bibi pamoja na Wajaliwa walitumia ungo kwenda sehemu tofautitofauti kama inavyodhihirika katika (uk.77) kutoka Tanga kuelekea Kilimanjaro.

Kutumia njia ya kufumba na kufumbua.Katika njia hii, bibi alikuwa akiwambia Majaliwa afumbe macho akifumbua wanakuwa wamefika sehemu au eneo lingine.Aina hii ya usafiri inadhihirika katika (uk 77,107,107 na 209). Mfano (uk 107) bibi alimwambia majaliwa afumbe macho baada ya Majaliwa kufumbua macho akajikuta yumo ndani ya pango la Amboni. 
Pia msanii ameonyesha jinsi bibi Majaliwa alivyokuwa akipaa hewani kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Mfano uk. (182)…. alimwacha sehemu ya Mwandege halafu akapaa.Hivyo usafiri aliokuwa akitumia bibi na Majaliwa kwa hali ya kawaida katika jamii ni mambo ya kinjozi yaani hayapo katika maisha ya kiuhalisia na wala hayatarajiwi kuwepo.
Kundi lingine la fantasia ni namna ya utokeaji na uondokaji wa bibi pamoja na umbo lake
Msanii ameonesha hali isiyokuwa ya kawaida katika maisha ya binadamu kwa kumtumia mhusika ambaye ni bibi yake Majaliwa na kufanikiwa kuonyesha hali hiyo ya kinjozi.
Utokeaji wa bibi pamoja na umbo lake unadhihirika kama ifuatavyo:-
Katika uk. (5-7) tunaona bibi anajitokeza katika umbo la samaki na kumbeba Majaliwa na kuondoka naye hadi Unguja kusini.Bibi yake Majaliwa alijitokeza kama papa na kubadilika na kuwa nguva .Hili si jambo la kawaida kwa binadamu kubadilika badilika bali ni mambo ya kinjozi tu.
Katika uk. (143) mwandishi ameonesha jinsi bibi alivyogeuka na kuwa tai mkubwa  na kuruka, hali hii pia sio hali ya kawaida kwa binadamu bali ni dhana ya ufantasia aliyoitumia msaniii ili kukamilisha lengo lake.
Pia mwandishi amefanikiwa kuonesha matukio mbalimbali ya kifantasia aliyokuwa akifanya bibi yake Majaliwa na Majaliwa. Mfano nyoka kutoka mdomoni kwa mtu uk. (58) msanii anasema, “Bibi alipanua mdomo na kutoa nyoka ambao waliwameza wale vibwanga wote”.
Kumvisha Majaliwa nguo uk. (58) bibi alichukua kijani akakichomeka kichwani kwa Majaliwa na Majaliwa akajiona amevaa koti,suruali na viatu vya baridi.
Kuna ufantasia unaojitokeza katika hadithi ambazo bibi alikuwa akimsimulia Majaliwa mfano uk. (169) Bibi anamsimulia Majaliwa hadithi ya mvuvi aliyevua chupa, na ndani ya chupa akatoka ndege mkubwa na kuanza kuongea.
Pia michezo ya wanyama wakali, imeoneshwa na msanii katika uk.(78 na 79) ambapo ameonesha jinsi Majaliwa na bibi yake walivyokuwa wakicheza na wanyama wakali kama vile simba na tembo huko mbugani Arusha .Dhana hii ni ya kifantasia kwani haiwezekani kabisa katika hali halisi kwa wanyama wakali kucheza na binadamu.
Kwa upande mwingine msanii ameonesha dhana ya ufantasia pale ambapo walikuwa wakiingia katika sehemu tofauti tofauti kama vile hotelini mfano waliingia hoteli ya ngurudoto huko Arusha uk.(80), na hoteli ya Seventy seven uk.(88)
Hivyo mwandishi ametuonesha hali zisizokuwa za kawaida katika maisha halisi ya binadamu kama vile  kubadilika badilika kutoka binadamu na kuwa samaki,bibi kuja kwa umbo la mama yake Majaliwa, bibi kuja kwa umbo la  binti mdogo na vitu vinginevyo kama ndege sio jambo la kawaida katika maisha ya kila siku ya binadamu.

Kundi lingine la fantasia lililooneshwa na msanii katika kitabu hiki ni uwepo wa jiwe la rubi, hili ni jiwe ambalo Majaliwa alipewa na bibi yake kwa masharti. Jiwe hili lilimsaidia Majaliwa  kula chakula katika sehemu mbalimbali  alizokuwa akisafiri akitafuta marimba yake ingawa jiwe hili lilikuwa na masharti.Masharti aliyopewa Majaliwa ni kutokula kitu kwa kupitia mdomo.Mwandishi ameonesha jinsi Majaliwa alivyotumia jiwe hilo, hata alipokiuka masharti bibi yake alimpa tena jiwe kama lile.Uwepo wa jiwe hili unadhihirika katika kurasa kama vile (21,102,110,143).Majaliwa alitumia jiwe hili kwa kula pale tu alipotamka maneno kadhaa na akujikuta tayari ameshiba bila kutumia mdomo na kinywa.
Kundi linguine la mambo ya ajabu ajabu  ni nmna ya utokeaji wa babu.Mwandishi ameonesha kuwa mpinzani wa Majalia, Ngongoti alikuwa akipata nguvu za kusafiri kwenda mbali pamoja na kumtoroka Majaliwa kwa kutumia nguvu za kimiujiza alizokuwa akisaidiwa na babu.Nguvu za babu zilikuwa kipingamizi kilichomfanya Majaliwa kushindwa kufanikisha haraka zoezi la kupata Marimba yake.Msanii ameonesha jinsi babu alivyokuwa akijitokeza na kutuma vikwazo kama vile:-
Vibwengo uk.(53). Mwandishi anaeleza, Majaliwa aliona kundi kubwa la vibwengo likwaajia kutoka kushoto, kulia na mbele yao.Pia uk. (27,58 ,93 na194) unaonesha jinsi babu alivyotuma vibwengo kumkabili bibi na Majaliwa.
Pia babu alimtokea Majaliwa katika umbo la Mamba akiwa na nia ya kumuangamiza lakini bibi alimsaidia, haya yanajitokeza katika uk.wa (49). Zote hivi ni fantasia kwani si hali ya kawaida kwa vitu kama hivi kujitokeza kwa umbo la binadamu na binadamu kujibadilisha na kujitokeza katika hali tofautitofauti katika maisha halisi ya binadamu.
Fantasia nyingine alizozionesha msanii ni kama vile, Majaliwa alipofika Ukerewe aliona mawe mawili makubwa juu ya mlima ambapo jiwe moja la juu lilikuwa linazungukazunguka. uk.(146).Hali hii katika mazingira ya kawaida si halisi na wala hatutegemei kuona jiwe likizunguka lenyewe bila mtu kuligusa.
Baada ya kupitia baadhi ya fantasia katika kitabu ch Marimba ya Majaliwa , ufuatao  ni mchango wa fantasia katika kazi hiyo;
Kujenga dhamira : Msanii ametumia dhana ya fantasia kama vile uwepo wa jiwe la rubi kujenga dhamira tofauti tofauti kama vile kuwafanya watoto wawe na adabu na utii, kuwafanya watoto wafikiri zaidi mazingira ya uwezekano katika jamii . Vilevle fantasia za utokeaji wa babu  huwafanya watoto wawe na woga juu ya mambo mbalimbali na wawe na mawazo juu ya tamaduni mbalimbali za watu wa kale.
Kujega taharuki: hapa fantasia hujenga shauku kwa watoto au msomaji kutaka kujua nini kitaendelea baada ya kukutana na kikwazo fulani.Mfano fantasia ya kuingia hoteli ya Ngurudoto na hoteli ya Seventy seven kimiujiza inajenga taharuki ya kutaka kujua kwamba, je baada ya kupambazuka Majaliwa atashikwa au la.Pia hali ya utokeaji wa babu kama mamba pale mtoni alipokuwa akinawa majaliwa,msomaji hupata taharuki ya kutaka kujua kama Majaliwa atamezwa na yule mamba au la.Fantasia ya kupaa kwa ungo na kutua juu ya mlima Kilimanjaro, msomaji hupata taharuki ya kutaka kujua kuwa Majaliwa atasalimika kwenye barafu au la.
Pia kutua na kucheza na wanyama wakali mbugani, huzua shauku kwa msomaji ya kutaka kujua wataliwa na wanyama hao au la na watasalimikaje na wanyama hao.
Fantasia humjengea mtoto au msomaji taswira tofauti tofauti juu ya mambo yasiyokuwa ya kawaida. Mfano fantasia ya utokeaji wa bibi katika sura tofautitofauti,utokeaji wa babu,uwepo wa jiwe la rubi na usafiri uliotumika hujenga taswira ya mambo kama hayo kutokea katika jamii. .Mtoto hujenga taswira juu ya uwepo wa vitu kama hivyo katika maisha ya kila siku ya jamii.

Fantasia huamilisha uwepo wa mambo fulani fulani katika jamii ili kutaka kuthibitisha mambo hayo. Mfano fantasia za utokeaji wa bibi na babu na upinzani kati yao, hutaka kuamilisha kuwa suala la ugomvi kati ya watu waliokufa yanaweza kuwapata watoto au watu wao wa karibu waliobaki duniani kwa namna tofauti tofauti za ajabu. Hivyo tunaweza kupata funzo kuwa ugomvi si kitu chema katika jamii.
Fantasia huibua migogoro : msanii ametumia dhana hii ya fantasia katika kitabu hiki ili kuibua na kukuza migogoro.Hali hii ya kukuza migogoro au kisa ni namna ambayo mtunzi hutumia ili kukifanya kisa chake kiwe na mawanda mapana.Mfano fantasia za upinzani wa babu dhidi ya bibi kwa maumbo tofauti kama vile umbo la vibwengo na umbo la mamba, hali hii imekuza kisa cha msanii na kuwa na mawanda mapana kwani humlazimu msanii kubuni zaidi namna ya kumuepusha muhusika wake asiangamie.Pia fantasia ya usafiri kama vile kutumia ungo,ufagio na nyinginezo, msanii amezitumia ili kujenga na kukuza migogoro katika kazi yake ili uwe na mawanda mapana zaidi.
Fantasia hufanikisha msuko wa vitushi,mfano msanii ameweza  kuhusianisha fantasia kama vile usafiri wa kutumia njia mbalimbali na hadithi mbalimbali alizokuwa akimsimulia Majaliwa na inaonesha wazi kuwa kutokana na kutumia fantasia kumemsaidia kukamilisha msuko wa vitushi kama vile alivyomsimulia majaliwa hadithi tofati wakiwa safarini. Mfano wakiwa juu ya  mlima Kilimanjaro.
Pia fantasia huburudisha, husisimua na kutia watoto hamasa.Mwandishi amefanikiwa kuonesha fantasia tofauti tofauti za kusisimua na kutia hamasa kama vile bibi alivyokuwa akimtokea Majaliwa, bibi na Majaliwa kucheza na wanyama na nyinginezo. Hali hii huburudisha na kumsisimua mtu aisomapo.Pia wasomaji huburudika kutokana na matukio ya ajabu ajabu yaliyojitikeza  na namna yanavyoendelezwa na msanii.
Hivyo tunaweza kuhitimisha kuwa mwandishi wa kitabu cha Marimba ya Majaliwa, amefanikiwa kuonesha jinsi fantasia zinavyojitokeza katika fasihi.Msanii ameonesha fantasia hizo zilivyotumika katika usakaji au utafutaji wa Marimba katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania.Utokeaji wa fantasia katika kazi ya fasihi huwa ni ubunifu wa mtunzi kwa lengo la kuifanya hadhira anayoiandikia, mathalani  ya watoto ihamaki na kufikiri zaidi sababu za uwezekano wa mambo kama hayo katika jamii.
                                         MAREJEO
 Semzaba, E. (2008), Marimba ya Majaliwa. E&D Publishers Limited:Dar es Salaam
Wamitila, K. W. (2003) Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia,Nairobi :English Press

MAANA YA RIWAYA NA AINA ZA RIWAYA


Katika kuandika makala hii hili, sehemu ya kwanza tutaangalia maana ya riwaya kwa mujibu wa wataalamu, historia ya riwaya kwa ufupi na sifa za zake. Sehemu ya pili tutaangalia kiini cha swali yaani aina za riwaya kwa mujibu wa wataalamu wa fasihi. Sehemu ya tatu tutaangalia hitimisho na kumalizia na marejeo.
Riwaya imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwao ni kama vile,
Encyclopedia  Americana (EA), Jz. 20 (1982:510f) wakinukuliwa na Mulokozi (1996) wanasema, riwaya kuwa ni hadithi ya kubuni inayotosha kuwa kitabu. Maelezo haya yanaibua utata kwani hayafafanui kitabu kinapaswa kuwa na urefu kiasi gani. Matharani kwa mujibu wa UNESCO katika Mulokozi (1996) kitabu ni chapisho lolote lenye kurasa 48 au zaidi. Ama urefu wa kitabu hautegemei idadi ya kurasa tu pia unategemea ukubwa wa kurasa (upana na kina) ukubwa wa maandishi na mpangilio wake.
Encyclopedia Britanica EB, Jz.8, (1985:810) wakinukuliwa na Mulokozi (1996) wanaeleza kuwa, riwaya ni masimulizi marefu ya kinathari yaliyochangamana kiasi, yenye kuzungumzia tajriba ya maisha ya binadamu kwa ubunifu. Udhaifu wa hoja hii ni kwamba wamejikita katika kigezo cha urefu, lakini hatujui urefu huo ni wapaswa kuwa kiasi gani. Lakini Mphahelele (1976:45) akinukuliwa  na Mulokozi (1996) anaeleza kuwa riwaya fupi huwa na maneno kati ya (35,000 hadi 50,000) na riwaya ndefu huwa na maneno kati ya (50,000 hadi 75,000).
Pamoja namaelezo hayo ya Mphahelele (1976) imeonekana bado kuna utata katika kigezo cha urefu. Hivyo Wamitila (2002)  Senkoro (2011) na hawakubaliani na  kigezo cha kufasili riwaya kwa kutumia kigezo cha urefu. Mfano Senkoro anaeleza kuwa ,
                               “Ikiwa tutakichukua kipimo cha jumla ya maneno (75,000)
                                 kuwa kielelezo cha riwaya basi itaonekana kuwa tuna
                                 riwaya chache mno katika fasihi kwa hali hii
                                 nadhani sifa ya mchangamano ni nzuri zaidi kuelezea
                                 maana ya riwaya” (uk. 56)

Naye Wamitila anendelea kuelezea kuhusiana na suala urefu kuwa,
                                        Kigezo hiki cha urefu hakifai tunapoziangalia kazi
                                          za fasihi ya Kiswahili...Mfano kazi mbili za E. Kezilahabi,
                                        “Nagona naMizingile” hazina idadi kubwa ya maneno lakini
                                         ni riwaya”.
Hivyo, Wamitila (2002) na Senkoro (2011) wanaelekeana kufanana katika kufasili maana ya riwaya ambapo wanaeleza kuwa, riwaya ni kisa mchangamano ambacho huweza kuchambuliwa kupimwa kwa mapana na marefu kifani na kimaudhui. Riwaya ni kisa au mkusanyiko wa visa, nyenye urefu unaoviruhusu vitambe na kutambaa mahali pengi na kuambaa vizingiti vingi vya maisha kama apendavyo mwandishi wake. Riwaya basi ni hadithi ndefu ya kubuni, yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja, na yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatia kwa undani na upana, maisha ya jamii. Riwaya hutoa picha ya jumla ya maisha ya mtu toka nyumbani hadi katika kiwango cha taifa na dunia nzima. Senkoro (2011).
Hivyo kutokana na fasili za wataalamu hawa tunaweza kufasili riwaya kuwa ni masimulizi ya kubuni ya kinathari yenye msuko au mpangilio fulani wa matukio au ploti inayofungamana na wakati au kusawili wakati na yenye visa vingi vivavyotendeka katika wakati fulani na yenye mawanda mapana yenye mchangamano wa dhamira, visa na wahusika.
Baada ya kutoa fasili mbalimbali za wataalamu wa fasihi kuhusu maana ya riwaya, sasa tuangalie kwa ufupi chimbuko la riwaya;
Riwaya ilizuka kutokana na maendeleo ya mageuzi ya kiutamaduni. Suala la ukoloni  na uvumbuzi pia liliumba hali ambazo zilihitaji kuelezwa kwa mawanda zaidi ya  yale ya ngano na hatithi fupi. Hapo hapo kuzuka kwa miji na viwanda pamoja na maendeleo ya wasomaji yalifanya riwaya nyingi ziandikwe. Uchangamano wa maisha ya jamii kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni  wenyewe ulizusha haja ya kuwa na utanzu wa fasihi ulio na uchangamano kifani na kimaudhui. Kupanuka kwa usomaji, hasa wakati wa mapinduzi ya viwanda huko Ulaya, kuliwafanya waandishi waandike waandiko marefu kwani sasa walikuwapo wasomaji hasa wanawake waliobaki majumbani wakati waume zao walipokwenda viwandani, wasomaji ambao muda wao uliwaruhusu kusoma maandiko marefu marefu ijapokuwa hii lilikuwa jambo la baadaye sana wakati wa kina Charles Dickens. Hii historia fupi ya chimbuko.  Senkoro (2011:55)
Baada ya kuangalia historia fupi ya chimbuko la riwaya ni vyema tukaangalia nduni bainifu za riwaya kwa kuziainisha katika aya moja. Kwa  mujibu wa Wamitila (2002)  sifa hizo ni kama zifuatazo;
Uwazi na uangavu, kazi husika ya fasihi isiwasumbue na kuwatatiza wasomaji kuzielewa, muwala na muumano, kazi ya riwaya lazima iwe na mshikamano au mtiririko mzuri wa visa au matukio kuijenga kazi ya kifasihi, uchangamano wa visa yaani kutokea kisa zaidi kimoja, wingi wa maana kuhusiana na sifa ya uchangamano na ukamilifu ni kule kuwako kwa elemeti zote muhumiu na za kimsingi katika kazi ya fasihi.
Baada ya kuangakulia sifa au nduni bainifu za riwaya tuangalie aina za riwaya kwa mujibu wa watalamu mbalimbali;
Katika uainishaji wa aina za riwaya, wataalamu wametumia vigezo mbalimbali vya uainishaji kama vile msingi wa kidhamira ambao kwa kiasi kikumbwa sifa za kimaudhui, kifani, kihistoria na kiitikadi. Katika uainishaji wa aina za riwaya kwa kutumia vigezo hivyo wataalamu wamefanana kuainisha baadhi ya aina za riwaya. Mfano Mulokozi (1996), Wamitila (2003) na Madumulla (2009)  aina walizofanana kuainisha ni kama zifuatazo;
Riwaya saikolojia ni aina ya riwaya  inayododosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia mawazo, imani, hofu, mashaka, matumaini na athari ya mambo hayo  kwake binafsi na labda kwa  jamii mfano “Kichwa Maji” ya  E.Kezilahabi, “Kipimo cha Mianzi” ya Feud na “Kiu” ya M.S. Mohammed.
Riwaya ya kisosholojia au jamii ni riwaya ambayo inasawiri maisha ya kawaida ya jamii kwa kuchunguza matatizo yake, yawe kifamilia kitabaka, kiuchumi, kisiasa au hata kiutamaduni  mfano “Titi la Mkwe” ya A. Banzi, “Kurwa na Doto” ya M.S. Farsi na “Rosa Mistika” ya  E. Kezilahabi.
Riwaya historia ni aina ya riwaya ambayo msingi wake kuhusu matukio fulani katika jamii ya mwandishi, tukio  hili huwa ni kubwa na la muhimu kijamii, laweza kuwa la kikabila au la  kitaifa  mfano “Uhuru wa Watumwa” ya J. Mbotela, “Miradi Bubu ya Wazalendo” ya Luhumbika na “Zawadi ya Ushindi” ya B. Mtombwa.
Riwaya ya uhalifu ni riwaya ambayo hujihusisha na uhalifu wa aina mbalimbali kama vile ujambazi, uuaji, magendo na utapeli. Mfano “Kwa sababu ya Pesa” ya Simbamwene na “Sanda ya Jambazi” ya H. Jajab.
Riwaya ya upelelezi ni aina ya riwaya ambayo huwa na vitu viwili yaani kosa /uhalifu na upelelezi wa uhalifu huo hadi mhalifu anapopatikana, hivyo wahusika wake ni wahalifu, wadhurumiwa na wapelelezi wakiwemo polisi “Mzimu wa Watu wa Kale” ya M.S. Abdallah na “Duniani kuna Watu” ya M.S. Abdulla.
Baada ya kuonesha aina za riwaya ambazo zimeainishwa na wataalamu hawa wote  sasa tuangalie aina za riwaya  ambazo wanafanana Wamitila na  Mulokozi aina hizo ni kama zifuatazo;
Riwaya  barua ni riwaya ambayo huwa na muundo wa barua kuanzia mwanzo hadi mwisho  mfano “Pamela” ya S.Richardson na “ Barua Ndefu kama Hii”
Riwaya ya vitisho ni riwaya yenye visa vya kusisimua damu na mara nyingi visa hivyo huambatana na matukio  ya ajabu na miujiza mfano “Mirathi ya Hatari” ya Mung’ong’o na  “Vipuli vya Figo” ya E. Mbogo.
Riwaya teti ni riwaya ambayo huathiriwa na kuchimbuka kutegemea jinsi mhusika mkuu anavyosawiriwa. Mhusika huyu huukejeli mfumo wa kiutawala uliopo katika jamii yake. Riwaya hii huonesha vituko ambavyo ni vigumu kukubalika vinavyotokea katika jamii mfano “Unfortune Traveler” ya  Daniel Defoi.
Riwaya ya majaribio, ni riwaya inayojadili mkondo wa nafasi na riwaya kweli. Riwaya ya mjadara nafsi hutungwa bila kuzingatia kanuni za kawaida za uandishi wa riwaya, watunzi wa riwaya hii hudai kuwa kumbo la kawaida ya riwaya hii haitoshelezi mahitaji ya karne hii huwakilisha ukweli wa maisha. Mfano, “Mtunzi wa Hukumu” ya Kasri na “Bina-Adamu” na Musaleo” za Wamitila.
Baada ya kuonesha aina za riwaya ambazo zimeainishwa na Mulokozi pamoja na Wamitila sasa tuangalie aina za riwaya ambazo zimeainishwa na Wamitila na Madumulla. Riwaya hizo ni kama zifuatazo;
Riwaya ya kitawasifu, ni riwaya ambayo ina muundo unafanana na muundo wa tawasifu kwa kuyachunguza maisha ya mtu fulani na kwa nafsi ya kwanza. Mfano riwaya ya “Uhuru wa watumwa” J. Mbotela na “Maisha Yangu baada ya Miaka Hamsini” ya S.Robert.
Riwaya ya wasifu, ni riwaya ambayo mwandishi huandika kwa lengo la kumhusu mtu fulani, mfano “Wasifu wa Siti Binti Saad” ya S. Robert.
Riwaya ya kifalsafa, ni riwaya ambayo inashughulikia masuala ya kifalsafa. Mada ya kifalsafa huchukua sehemu muhimu katika riwaya ya aina hii kuliko wahusika, mandhari, msuko au mtukio. Mfano, “Nagona na Mzingile” ya E kezilahabi na “Umleavyo” ya Haji Gorra Haji.
Baada ya kuonesha aina za riwaya ambazo zimeainishwa na Wamitila na Madumulla, tuangalie zile ambazo zimejadiliwa na Mulokozi na Madumulla ambazo hazijaainishwa na Wamitila.
 Riwaya ya mapenzi ni riwaya yenye kusawiri uhusiano wa kimapenzi kati mvulana na msichana. Mfano “Kweli Unanipenda”  “Mwisho wa Mapenzi” za Simbamwene.
Riwaya ya ujasusi ni wa upelelezi wa kimataifa. Majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na; nchi, serikali au waajiri wao kwenda katika nchi nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za kijeshi, kiuchumi na kisayansi ili taarifa hizo ziwanufaishe wale waliotumwa mfano “The thirty nine steps” ya E. Msiba. “Mzimu wa Watu wa Kale”.
Baada ya kuonesha ufanano wa uainishaji wa aina za riwaya kwa mujibu wataalamu  hawa tuangalie aina za riwaya ambazo zimeainishwa na mtaalamu mmoja mmoja bila wengine kuziainisha aina hizo.Tukianza na Wamitila ameainisha aina za ruiwaya kama zifuatazo;
Riwaya changamano; ni riwaya ambayo ina muundo mgumu na inayohitaji umakini kuielewa. Kwa kawaida msuko wa riwaya hii huwa tata. Inawezekana pakawepo na matumizi mapana ya mbinu rejeshi, upana mkubwa wa wahusika na mandhari, matumizi mengi ya lugha ya kitamathali, mfano; “Mzingile” ya E. kezilahabi, “Zirail na Zirani” ya W.E Mkufya.
Riwaya sahili; ni dhana inayotumiwa kuelezea aina za riwaya ambayo ina muundo rahisi na inaweza kueleweka kwa urahisi. Kwa mfano; riwaya ya “Kaburi Bila Msalaba” ya P . Kureithi.
Riwaya tatizo; ni riwaya ambayo inajishughulisha na tatizo au mgogoro fulani katika jamii. Huweza pia kuelezea aina ya riwaya ambayo inachunguza tasnifu au swala fulani la kisaikolojia. Mfano; “Kuli” ya Shafi A.shafi na “Mafuta” ya K. Mkangi.
Riwaya kampasi; ni riwaya ambayo mandhari yake ni chuo kikuu. Hata hivyo hii imepanuliwa na kuhusishwa na kazi za kuchekesha au zenye mwelemeo wa kitashititi. Kazi za aina hii hukusudia kufichua udhaifu uliopo katika tabia za wanachuo. Mfano; “Small world” ya David Lorge.
Riwaya ya kiambo; ni riwaya ambayo inatilia mkazo kwenye mandhari, usemi au muundo wa kijamii na desturi za mahali maalumu. Mandhari na mahali huathiri njia mbalimbali za kuhisi na kuwaza kwa wahusika wanaopatikana kazi ya aina hii.
Riwaya ya  kidastopia hii husawili jamii isiyokuwa ya kawaida na isiyokuako kwa wakati maalumu bali inafikirika tu. Katika jamii hiyo sheria za kawaida za kijamii zimebadilishwa kwa namna inayowafanya watu wengi waishie kutaabika na kuteseka sana. Mfano wa riwaya hizi ni kama vile “ Kusadikika” ya Shabani Robert na “Walenisi” ya Katama Mkangi.
Riwaya ya kimonolojia  ni riwaya ambayo sauti inayotawala ni moja. Sauti hiyo ni ya mwandishi. Wahusika wanaopatikana katika riwaya hii hudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na sauti ya mwandishi. Mfano “Walenesi” na “Mafula” za Katama Mkangi.
Riwaya ya kipolifoni; ni riwaya ambayo inahusishwa na urejeleaji  ambapo kila wahusika wanapozungumza au kuongea sauti zao mbalimbali zinawakilisha mikabala mbalimbali kiitikadi. Mfano “Dunia mti mkavu” ya S.A Mohamed.
Riwaya ya kisasa; ni riwaya inayohusu wanasiasa na maisha yao wanasiasa. Hudhamiria kuyafichua mambo yanayotendeka kinyume na picha inayoonekakana waziwazi. Mfano; “Nyota ya Huzuni” ya George Liwenga na “Njozi Iliyopotea” ya C.G. Mng’ong’o.
Riwaya ya kitarihi ni riwaya ambayo inajihusisha na mawanda makubwa ya kiwakati na kimandhari.Wahusika wengi walioteuliwa kuakisi hali mbalimbali za kijamii na kiuchumi za wakati maalumu. Mfano;Riwaya ya  “Habari za Wakilindi”
Riwaya ya Kitasnifu ni riwaya inayojihusisha na tatizo fulani la kijamii hasa kwa nia ya kuwahusisha  wasomaji. Katika hali fulani inayowapata wahusika na kwa njia hiyo huwachochea kuwazia njia ya kusuluhisha tatizo hilo Mfano; “Njozi Iliyopotea” ya M.Mng’ong’o na “Nyota ya Huzuni” ya G.Liwenga.
Riwaya ya kiutopia hii ni riwaya ambayo inasawiri jamii anayoiona mwandishi kama jamii kielelezo na aghalabu huhusisha sifa za Kifantasia au kinjozi. Mfano wa riwaya hii ni kama, “Siku ya Watenzi Wote” ya Shaaban Robert
Riwaya ya kiurejelevu hii ni riwaya inayojirejelea. Aghalabu katika usimulizi wake, riwaya  ya aina hii huishia kutoa maoni kuhusu usimulizi wake na njia za kubuni na kutunga riwaya.Tunaweza kusema hii ni riwaya inayofichua mbinu zake za kiutunzi. Mfano “Musaleo” ya K.W.Wamitila
Riwaya kinzani ni riwaya inayotumiwa kuelezea ambayo imekwenda kinyume na matarajio au kaida za uandishi wa riwaya. Mfano, kuwa na muundo wa kimajaribio wahusika kukosa motisha, kuwako kwa matendo yasiyoweza kuungwa kimantiki.
Riwaya ya utetezi  hii hutumiwa kuielezea riwaya ambayo inahusu matatizo ya kijami, kiuchumi pamoja na dhuluma inayowapata wanyonge au wasiokuwa na uwezo katika jamii fulani. Hivyo riwaya hii hukusudia kurekebisha hali iliyopo katika jamii. Mfano “Walenisi” na “Mafuta” ya Katama  Mkangi na “Kuli’ na  “Vuta n’kuvute” za Shafi A.Shafi.
Pia kuna  baadhi ya aina za riwaya ambazo zimejadiliwa  na Mulokozi ambazo hazijajadiliwa na Wamitila na Madumulla. Aina hizo za riwaya ni kama zifuatazo;
Riwaya chuku  ni riwaya ambayo hueleza vituko na masahibu yasiyo kuwa ya kawaida, ni riwaya ambayo haizingatii  uhalisia na mara nyingi masahibu yake huambatanana mapenzi.Mfano “Alfu lela Ulela” ya G. Bocci ccio na “Kusadikika” ya S.Robert”
Riwaya ya kingano, ni riwaya yenye umbo na mtindo wa ngano mathalani huweza kuwa na wahusika wanyama,visa vyenye kutendeka nje ya wakati wa kihistoriA.Mfano “Lila na Fila” ya Longman na  “Adili na Nduguze” ya S.Robert
Riwaya istiara ni riwaya mafumbo ambayo umbo lake la nje ni ishara au kiwakilishi tu cha jambo jingine. Mfano “Kusadikika”  ya S.Robert ambayo inasawili  utwala wa mabavu na “Shamba la Wanyama”  ya Kawegere.
Riwaya tendi ni riwaya yenye mawanda mapana kama tendi aghalabu riwaya hii husawili matendo ya ushujaa na masuala mazito ya kijamii yenye kuathiri historia ya taifa husika. Mfano “Vita na Amani” ya Leo Tolstoi na “Chaka Mtemi wa Wazuru” ya Thomas M.
Riwaya ya kisayansi ni riwaya inayotumia taaluma  ya sayansi kama msingi wa matukio, masahibu na maudhui, mathalani riwaya hii hubashiri namna sayansi itakavyo athiri maendeeo ya mwanadamu katika karne zijazo. Mfano “Safari Kiini cha Dunia” ya Jules Vernes.
Kuna baadhi ya aina ya riwaya ambazo zimejadiliwa na Madumulla ambazo hazijadiliwa na Mulokozi na Wamitila. Ambazo ni kama zifuatazo;
Riwaya ya kimaadili ni riwaya ambayo ina nia ya kufundisha maadili fulani mfano “Kufikirika” ya S Robert.   Ni riwaya inayotoa maadili kwa jamii.
Riwaya ya kimapinduzi ni riwaya ambayo inajadili migogoro na maisha ya binadamu kwa kutafakari kwa mantiki na kina kuhusu mambo ambayo urazini wake hauonekani kwa urahisi. Mfano “Umleavyo” ya Haji na Kichwa Maji” ya E.Kezilahabi.
Hivyo kutokana na uainishaji huu wa aina mbalimbali za riwaya kutoka kwa wataalamu hawa tumeona kuwa wanatofautiana katika vigezo vya uainishaji ambapo tunaona wanaainisha aina mbambali za riwaya. Kutokana na uainishaji huo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa aina hizo zote za riwaya zinaweza kuangukia katika aina kuu mbili za riwaya ambazo ni riwaya ya dhati na riwaya pendwa. Riwaya pendwa ni riwaya ni riwaya ambazo hutungwa kwa lengo la kuburudisha na kumstarehesha msomaji mfano, riwaya za kimapenzi, kimahaba, kiuharifu, kiupelelezi na kijasusi. Wakati riwaya ya dhati ni riwaya ambazo huchimbua na kuchambua masuala mbalimbali ya kijamii, yaani hutafuta chanzo chake sababu zake mpaka kikatokea athari na suluhisho lake. Hivyo tunaweza kusema kuwa aina za riwaya ambazo hukosekana katika aina mojawapo ya riwaya dhati huwa katika  riwaya pendwa.

MALEJEO.
Madumulla, S.J.  (2009) Riwaya ya Kiswahili: Nadharia Historia na Misingi ya Uchambuzi.
                              Dar es Salaam: Mture Educational Publishers Ltd.
Mulokozi, M.M. (1996) Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.
Senkoro, F.E.M.K. (2011) Fasihi. Dar es Salaam: KAUTTU.
Wamitila, K.W. (2002) Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix
                             Publishers Ltd.
Wamitila, K.W. (2003)  Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publicatins Ltd.


MTINDO WA MWINGILIANOMATINI KWENYE KAZI ZA FASIHI.

UCHAMBUZI WA TENDI.

Makala  hii ina lengo la kutaka kujua kama tendi za Kiswahili huwa na mwingiliano matini  na  kubainisha  vipengele  vilivyoingiliana katika utanzu huu na dhima zake. Waandishi wa tendi mbalimbali za Kiswahili, wamekuwa wakitumia mtindo wa kuchanganya vipengele mbalimbali vya kisanaa katika kazi moja. Mbinu hii inatazamwa na makala haya kuwa ni mwingilianomatini katika tendi za Kiswahili. Mathalani, mwandishi  anayeandika  au simulia tendi za Kiswahili, hujikuta akichanganya matini za nyimbo, semi, hadithi  ndani  ya  hadithi,  maigizo,  matumizi  ya  ishara, ngoma  na  kadhalika.  Kuchanganya  huko  kwa vipengele  tofauti  katika  kazi  moja  ni  kitu  ambacho  kimezoeleka  sana  miongoni  mwa wanafasihi. Kipengele hiki kinahitaji kuandikiwa ili kuweza kuweka bayana kuwa katika tendi kunaweza kuwa na sifa mbalimbali  za tanzu nyingine na kuziorodhesha ili zijulikane wazi. Hivyo makala haya yatakuwa na lengo la kuthibitisha uwepo wa mwingiliano huo.
Utangulizi
Mwingilianomatini  katika kazi za fasihi  ni  dhana  ambayo  imekuwa  ikijitokeza  sana kwa  sababu  mbalimbali  za  kifasihi. Wakati  mwingine  mwingiliano huu hubainishwa kabisa  na wataalamu wa  fasihi  simulizi kama  mtindo wa kawaida katika kumbo za fasihi. Kwa mfano, Mulokozi (1989)  anasema  kwamba mojawapo  ya  sifa  kuu  ya  fasihi  simulizi  ni  vipera  vyake  kuingiliana  katika utendaji.  Pamoja  na  mtindo  huo  kuwa  wa  kawaida  katika  fasihi,  bado  sababu zake hazijabainishwa wazi katika uhakiki wa kazi za fasihi. Kwa  mantiki  hiyo, kuna  haja  ya  kuchunguza  sababu  zake  ili  kupanua  uelewa  katika  taaluma  ya fasihi. Makala haya yana lengo la kuzionesha sababu hizo za kuingiza vipengele mbalimbali vya kisanaa katika fasihi kwa kuchunguza tendi.
Pengine, tuanze kwa kujiuliza swali, mtindo ni nini? kisha tutafasili dhana ya mwingiliano matini, tendi, kisha tutaangalia vipengele ambavyo vimeingiliana katika tendi za Kiswahili na dhima zake na mwisho ni hitimisho.
Tukianza na fasili ya mtindo; Senkoro (2011) anasema mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kaida zilizofuatwa kama ni(za kimapokeo) au ni za kipekee. Wamitila  K.W (2008) anasema mtindo ni sifa ya upekee ambayo huitambulisha kazi ya mtunzi au msanii fulani.
Kwa ujumla fasili hizi hazipishani sana, ukizichunguza utagundua kuwa mtindo hujihusisha na namna ambayo msanii huitunga kazi yake ambayo huwa na upekee wa namna fulani; upekee huu ndio unaoweza kuwatofautisha  waandishi. Hivyo basi kwa kutumia mtazamo wa kimtindo tunaweza kufasili mwingilianomatini kama alivyofasili Senkoro (2011) kuwa ni  mbinu ambayo huonyesha kutumiwa kwa utanzu mmoja wa fasihi katika kutolea au kuwasilisha utanzu mwingine. Kwa mfano si jambo geni kukuta wimbo au kipande cha wimbo ndani ya ngano au hadithi. Hivyo basi tunaweza kusema kuwa mwingilianomatini ni ule uwepo wa sifa mbalimbali za matini moja au zaidi katika kazi fulani ya fasihi kama vile matumizi ya nyimbo, matumizi ya barua, ngoma, masimulizi ya hadithi ndani ya hadithi, misemo, nahau, majibizano, vicheko, picha na michoro na kadhalika. Baada ya hapo tuangalie tendi ni nini? Jibu la swali hili ni muhimu ili kupata uelewa wa awali  katika hoja  za makala haya. Zipo maana  kadhaa zinazotolewa  na wanafasihi  mbalimbali  kuhusu dhana ya tendi.
Mulokozi (1996) anafafanua tendi kuwa, ni utungo wenye kusimulia matukio ya kishujaa yenye uzito wa kijamii au kitaifa. Matukio haya yaweza kuwa ya kihistoria lakini tendi nyingi huchanganya historia  na visakale au visasili. TUKI  (2004) wanasema tendi ni utanzu unafaa kusherekewa kishujaa. Hii inaonyesha kuwa tendi zinahusu matukio ya kishujaa yaweza kuwa ya  kweli  au ya kubuni, na yenye funzo fulani kwa jamii.
Kutokana na fasili ya tendi tunayopata kupitia maoni ya wataalamu hawa tunabaini kuwa utendi ni mojawapo ya tanzu za kazi za kifasihi. Utanzu huu unaweza kuwa katika umbom la kiusimulizi au la kiuandihi. Kwa mantiki hiyo, tendi kama zilivyo tanzu nyinginezo za kifasihi huwa na mitindo anuai. Mojawapo ya mittindo yake ni suala la mwingiliano matini.
Data  ya  makala  haya  imepatikana  kutoka  katika  sampuli  ya kitabu  cha Utenzi wa Nyakiiru Kibi kilichoandikwa na Mulokozi (1997). Uteuzi  wa  kitabu hicho  kama sampuli umefanyika kwa nasibu. Unasibu huo umetokana na imani kuwa mbinu hii ya mwingilianomatini hujitokeza katika tendi zote. Hivyo  hakukuwa  na haja  ya  kuweka  vigezo  vingi  vya  uteuzi.  Lakini,  kwa  ujumla  makala  imeteua kitabu  hicho  kwa  kuzingatia  kigezo cha matukio yake  kuwa  na  ujumbe kwa jamii, lugha rahisi, muundo sahili, na kadhalika. Utenzi huu unasimulia historia ya kuanzishwa kwa utawala wa ukoo wa Babito katika nchi ya Kiziba, wilaya ya Bukoba, karne ya 15. Babito walikua ni wahamiaji wa Kiluo kutoka Uganda.Walifika Kiziba kutokea Bunyoro nchini Uganda, ambako walikuwa tayari ni watawala. Historia ya Babito katika maeneo haya inaonyesha namna watu wa jamii na lugha mbalimbali hapo kale walivyokua na ushirikiano mzuri katika kujenga utaifa na ustawi wao. Siasa za ukabila na ubaguzi hazikua na nguvu. Mhusika mkuu katika andiko hili ni Nyakiiru. Huyu anasimuliwa kama mhusika shujaa. Nyakiiru alikua ni kiongozi wa kundi la Babito lilofika Kiziba kama mwaka 1945; ambapo alishirikiana na Kanyamaishwa, ambaye alikuwa ni mototo wa mfalme wa Kiziba aliyeitwa Ntumwa, kumwua mfalme huyo na hivyo kujichukulia madaraka ya utawala.
Hadithi ya utenzi huu imetokana na masimulizi ya wazee ambayo yamehifadhiwa katika vichwa vya watu na kupokezwa kwa mdomo tangu karne ya 15. Hata hivyo yako mambo kadha ya msingi ambayo yanajitokeza takribani katika masimulizi yote. Mambo hayo ndiyo mwandishi amejaribu kuyatumia kama kiini cha utenzi huu na amejaribu kuyapanga kisanaa ili kupata hadithi nzuri na yenye mshikamano na mtiririko mzuri unaofaa, na wenye mafunzo fulani kwa vizazi vya leo. Hivyo utenzi huu hausimulii historia kavu, bali unasimulia hadithi ya kusisimua inayotokana na historia iliyochanganyika na visakale ambayo ni masimulizi yanayohusu mashujaa wa kale ambayo yamechanganya ubunifu ndani yake na yaweza kuwa ya kweli au ya kubuni. Utenzi huu umekusudiwa usomwe na vijana. Hivyo lugha yake imerahisishwa kidogo ili ieleweke vizuri kwa walengwa.
Mwega wa Kinadharia
Makala  haya  yataongozwa  na mwega wa kinadharia wa  mwingilianomatini. Ili hadhira ya fasihi ielewe kazi yoyote ya fasihi lazima ihusishe vipengele vingine nje  ya  muktadha  wa  usomaji  au  usimulizi  ule  (Mshengyezi,  2003).  Dhana ya kuingiza  vipengele  hivi  ndiyo  huitwa  mwingilianomatini.  Wataalamu
wanaounga mkono mawazo ya nadharia hii wanamtaja mwasisi wa nadharia hii kuwa ni Mikhail M. Bakhtin ambaye alikuwa mwanaisimu na mhakiki wa kazi za fasihi aliyeishi kati ya mwaka 1895-1975 (Njogu na Wafula, 2007). Njogu na Wafula  wanazidi  kusema  kuwa  Bakhtin  aliamini  kwamba  kazi  ya fasihi ina sauti mbalimbali  zinazoingiliana  na kupiga  mwangwi  katika  kazi  nyingine zilizotangulia,  zilizopo au  zitakazokuja  baadaye. Ufafanuzi  huo pia  uliwahi kutolewa  na  Wamitila  (2006)  aliposema  kuwa  Bakhtin  anaamini  kuwa  utanzu wa riwaya una uwezo wa kuingiza vipengele vya tanzu nyingine lakini ukabakia na  sifa  zake  kama  utanzu.  Hali  hiyo  ndiyo  pia  hujitokeza  katika  tendi mbalimbali  za  Kiswahili  ambazo  zina  mwingiliano  na  vipengele  vingi  sana katika  kazi  moja.  Kwa  ufafanuzi  wa  Wamitila,  utanzu  wa  fasihi  kuwa  na vipengele  vingine  ndani  yake  hakuondoi  hadhi  ya  utanzu  huo.  Kwa  ujumla, tunaposema  kuingiliana  kwa  matini  katika  kazi  za  fasihi  tunamaanisha  kazi moja ya kifasihi kuwa na sifa za tanzu nyingine ndani yake. Kabla hatujaenda kuona vipengele hivyo vilivyojitokeza katika tendi hebu tuangalie kwanza sifa za tendi za Kiswahili.
 
Sifa za Tendi za Kiswahili
Molukozi (1996) kama alivyomnukuu  Finnegan (1970:108) anasema kuwa utanzu huu hautokei sana katika  Afrika, pamekua na mjadala mrefu kuhusu fani hii. Wataalamu kama  Okpewho (1979) Johnson (1986) Mulokozi (1987) na wengine wamethibitisha kuwa utendi ni fani iliyoenea sana katika Afrika, na wamejeribu kuonyesha baadhi ya sifa zake. Finnegan alibainisha sifa nne za tendi simulizi:
Ø    Nudhumu: Utendi aghalabu ni utungo wa kishairi.
Ø    Urefu: Anasema ni utungo mrefu.
Ø    Upatanifu:  Anasema ni utungo ambao una visa vilivyounganika kimantiki.
Aidha Mulokozi  anaendelea  kusema kuwa zaidi ya sifa za utendi alizoelezea Finnegan, ambazo wengi wanaona hazitoshelezi, uchunguzi wao umedhihirisha kuwa utendi una sifa zifuatazo:
Ø    Hutolewa kishairi
Ø    Huhusu matukio muhimu ya kihistoria au kijamii;
Ø    Huelezea habari za ushujaa na mashujaa; hii inamaanisha kuwa husimulia juu ya maisha na matendo ya kishujaa ya mbabe wa utendi, kwa mfano kuzaliwa kwake, maswaibu yake, safari zake, uongozi wake kwa watu wake, na kifo chake.
Ø    Matini (maneno) yake kwa kawaida hutungwa papo kwa papo (utendi hautungwi kabla ya kuhifadhiwa kichwani kwanza ili badaye utolewe kwa ghibu).
Ø    Hivyo, hutawaliwa na muktadha wa utungaji na uwasilishaji  wake kwa jamii.
Baadhi ya tendi muhimu za Kiafrika ni Sundiata (au Sunjata) (Mali, Gambia, na) Mwindo (Zaire), Silamaka (Mali) na Mvet (Gabon). Katika Afrika Mashariki, tunao ushahidi kuwa tendi ziko au zilikwepo katika jamii zifuatazo: Wachaga (Mlire); Wahehe (Mukwavinyika); Wanyambo na Wahaya (Kachwenjanja, Mugasha); Wakwere na Wazinza. Anasema hata hivyo, uchunguzi bado hujakamilika, na huenda zipo jaamii nyingine zenye utanzu huu. Hatuwezi kupinga hoja za mtaalamu huyu wa fasihi kwani hoja zake zinaonekana kuwa na ushawishi kuwa tendi zilikwepo na pia zina sifa kama hizo alizobainisha hususani kuhusu mashujaa  na matukio ya kishujaa;  yaweza kuwa ya kweli au ya kubuni au ya kihistoria. Hii ni kwa sababu tendi ni sanaa inayoambatana na hali fulani ya kijamii, hasa ile hali yenye vuguvugu la mapambano, na yenye asasi (kama vile ufalme)  zinazoweza kuidhamini sanaa ya utendi. Hii ni sanaa ambayo hufa, kwa vile mazingira yanayoilea na kuirutubisha hayapo  tena, hivyo ni muhimu kuzirekodi na kuzihifadhi zile tendi chache tulizo nazo kabla hazijatoweka au kusahaulika kabisa na kupotea katika jamii. Baada ya kuona sifa hizo za tendi za Kiswahili sasa tuangalie  vipengele vilivyojitokeza katika utanzu huu.
Tanzu Zinazojitokeza katika Tendi za Kiswahili
Tanzu  zinazojitokeza  katika  tendi  ni  nyingi, lakini  hapa  tutatumia  vipengele vichache tu vinavyojitokeza katika tendi za Kiswahili. Katika Utenzi wa Nyakiiru Kibi kuna vipengele au sifa mbalimbali  za tanzu  nyingine ambazo mwandishi ameziingiza katika  utanzu huu, tanzu hizo ni kama hizi  zifuatazo:
Picha au Michoro mbalimbali
Makala yanatumia dhana ya picha na mchoro yakimaanisha uwakilishi wa sura ya  mtu/watu  au  kitu/vitu au mahali  kwenye  karatasi  au  kitu  chochote  kinachoweza kuandikwa  juu  yake. Sura  hiyo  inaweza  kuwa  imechorwa, imechongwa au tengenezwa. Katika utanzu huu picha zinaonekana katika jalada, pia katika ukurasa wa 1,2, 3, 7,8, 9,10,11, 12, 15 19, 20, 23, 24,25, 26, 28, 30, 33,39,44,50,54, 55, 60, 61, 64, 65,66, 69,75,83,87, 88,90 na 91. Mwandishi amejaribu kutumia michoro na picha katika utanzu huu ambako inasaidia kutoa ufafanuzi wa kina juu ya matukio yaliyojitokeza katika utenzi huu na vile vitu vilivyotumika katika utenzi huu na maeneo mbalimbali yaliyohusika au husishwa katika kukamilisha matukio au utendekaji wa matukio mbalimbali  na picha za watu mbalimbali. Kwa mfano katika jalada la kitabu mwandishi ameonesha mchoro wa ngoma ikimaanisha ngoma ni chombo muhimu cha kijadi katika jamii na picha za vibuyu hii ikidhihirisha kuwa kuna mambo ya kijadi yaliyokua yakitendeka katika jamii zetu na hii inaonesha uzalendo kwa kuenzi utamaduni wetu; pia katika kurasa za mwanzoni kabisa kunaonekana picha za watoto wamekaa wanasoma vitabu ikionesha kuwa ni ishara ya kuhamasisha watoto wajijengee utamaduni wa kujisomea vitabu, bado katika kurasa hizo kuna michoro ya ramani ambazo zinaonyesha maeneo yaliyozungumziwa katika utenzi huu; hii inasaidia wasomaji kuelewa kwa urahisi kile kilichozungumziwa katika kazi hii na kuweza kuvuta hisia zaidi na kujijengea taswira za ulimwengu mpya. Aidha tukiangalia katika ukurasa wa 10,25,44,50 na 88 tunaweza tukaona jinsi mwandishi ameonesha picha za baadhi ya matukio yaliyokua yanatendeka mfano upigaji wa ngoma, Nyakiiru akipambana na chui, mapambano katika ukurasa wa 88 ambako Nyakiiru alitoka na jeshi lake akaenda kushambulia maadui Bugandika na watu wakauana sana; kwa kuangalia picha hizo zinavuta hisia za huzuni na wakati mwingine zinatujengea ujasiri kutokana na matukio ya kishujaa yaliyotokea. Katika tendi simulizi, dhana ya picha hujitokeza kwa sifa kadhaa za mwonekano wa wahusika wa tendi  zinazofafanuliwa  na  msimulizi  mbele  ya hadhira. Kwa  mfano, wadudu  watapewa  sifa ya jitu  kubwa  lenye  uwezo  wa kufanya maajabu makubwa kijiji  kizima, kwa mfano katika ukurasa wa 75  katika ubeti wa 724 na725 mwandishi amechora picha zinazoonesha jinsi senene walivyoweza kutishia kijiji kizima cha Baziba.
              724     Senene kwenye mashamba                     725     Senene miti kishika
                        Matawi yanavunjika                                          Senene kwenye miamba
                        Kwenye mapaa ya nyumba                                Matunda yanaanguka
                        Na mashina kupembea!                                    Senene wakatambaa!
Hivyo kipengele hiki cha michoro na picha mbalimbali ni moja ya sifa za utanzu mwingine ambazo tunaweza kusema zimeingizwa katika tendi, na michoro hii imesaidia kufanya matukio yaweze kueleweka kwa urahisi pale ambako hayakueleweka vizuri aidha yamepelekea kuleta uhalisia wa matukio na visa hivyo kwa  hadhira na jamii nzima. Hivyo michoro hukazia uelewa na kufikisha ujumbe kwa urahisi na kuimarisha maudhui, uhalisia wa jambo na huleta mvuto kwa wasomaji na kuchochea udadisi kwa hadhira.
Hadithi ndani ya Hadithi
Hadithi ndani ya hadithi  ni  dhana  inayomaanisha  simulizi  moja  kuingiliwa  na nyingine. Kwa  mfano, mwandishi kama msimulizi mkuu wa hadithi  anampa nafasi  mhusika  katika  hadithi kusimulia hadithi  nyingine. Katika  dhana  hii  kunakuwa  na  hadhira  tofauti  kutokana  na idadi  ya  usimulizi.  Mathalani, tunaposoma  hadithi  halafu  ndani  ya  hadithi  hiyo  tukakuta  mhusika  mwingine ndani ya hadithi hiyo akiwasimulia  wengine, hapo tunakuwa  na hadhira ya aina mbili. Sisi kama wasomaji  tunakuwa  hadhira,  na  wale  wanaosimuliwa  na mhusika  katika  hadithi  nao  pia  ni  hadhira  nyingine.  Kwa  mfano, ndani ya hadithi ya kitabu cha Nyakiiru Kibi kuna wasimulizi wawili. Mmoja  ni mwandishi  mwenyewe  akisimulia historia ya kuanzishwa kwa utawala wa ukoo wa Babito katika nchi ya Kiziba ambapo naye anasema hadithi hii imetokana na masimulizi ya wazee yaliyohifadhiwa kwenye vichwa vya watu. Msimulizi  mwingine ni Nyakiiru  wa hadithini  na Kanyamaishwa  wakimsimulia Mtukufu wa Omukama wa Jamala kuhusu maisha yao na walikotokea na jinsi walivyokua wanaishi na kazi waliyokua wanaifanya toka utotoni, ujuzi  walionao  na nasaba yao kwa ujumla. Hapa tunaona jinsi kipengele hiki kilivyojitokeza katika tendi hii na Nyakiiru na Kanyamaishwa wamekua kama wasimulizi na Mtukufu Omukama kawa kama hadhira katika ukurasa wa 67 ubeti wa 634 hadi 641.
Pia usimulizi mwingine unaonekana ukurasa katika  wa 80 ubeti wa 775 hadi 780 ambako kuna masimulizi juu ya safari ya Nyakiiru na Kanyamaishwa wanaelekea Ikulu kwa Sulutani. Hata katika ukurasa wa 6 mwandishi amejaribu kuingiza masimulizi katika ubeti wa 55 ambako inaelezwa habari za kuwepo kwa Sulutani enzi za zamani ambaye ilikuwa mkali kupindukia. Hivyo masimulizi haya yanasaidia kuingiza vionjo mbalimbali katika  tendi na kuendeleza uwepo wa matukio mbalimbali katika tendi hii huwafanya hadhira wasichoke kufuatilia matukio yanayoelezwa katika tendi na  kuongezea ufahamu wa mambo mbalimbali na kuyahusianisha na mazingira yao ya kila siku. Hiki nacho ni kipengele ambacho pia kinajitokeza  katika kazi za kifasihi kama vile tendi kwa sababu katika kila tukio huenda kukawa na tukio jingine ndani yake au kinachohusiana na tukio hilo,hivyo mwingiliano wa matukio hayo ndiyo unaopelekea uwepo wa mtindo wa mwingiliano matini katika  tendi za Kiswahili.
Maigizo
Maigizo  ni  matendo  ya  kumithilisha  kitu  au  tabia  fulani  kwa  nia  ya  kufikisha ujumbe  kwa  jamii. Matendo yanayoweza kuigizwa ni kama vile uchawi, ulevi,  ugomvi, matambiko, uganga, michezo ya ngoma, kusalia miungu, mapambano,  uwindaji, unyanyasaji, kuzaliwa kwa mtoto na  kadhalika.  Mambo  hayo hufanywa  na wahusika wa kimaigizo  mbele  ya  hadhira  ili  kufikisha ujumbe. Matendo  yanayofanywa  na  wahusika  wa  kimaigizo  siyo  halisi  kwa  kuwa wahusika wa kifasihi sio watendaji wake halisi, bali wahusika huvaa tu uhusika kama  nguo kwa  muda  ili kuwakilisha watendaji  halisi  katika  jamii.
Aidha, maigizo  ni kipengele  mojawapo  cha  sanaa  za  maonesho  chenye  sifa  zifuatazo:  dhana inayotendeka,  uwanja  unaotendewa, watendaji, hadhira (watazamaji), kusudio la kisanaa, muktadha wa kisanaa na ubunifu (Mulokozi, 1996). Katika tendi  mara nyingi fanani hulazimika  kuingiza  matini  ya  maigizo  katika  usanii  wake.  Endapo  matukio  yanayotokea  katika  kisa  chake  yanaweza  kuigizika  basi  anayehadithia  hulazimika  kuigiza.  Kwa  mfano,  msimuliaji  wa hadithi  akisimulia  hadithi  yake  yenye  mhusika au wahusika  wanaoimba basi  msimuliaji  huyo  hujikuta  akiimba   mbele  ya  hadhira.  Huu  ni  uigizaji.  Kuna  matendo   mbalimbali ambayo yameigizwa katika utenzi huu ambayo yanatokea katika jamii kama vile uwindaji, mambo ya uganga au matumizi ya waganga jadi, wazee wa jadi na imani za kishirikina mfano katika ukurasa wa 18 katika ubeti wa 156 mwandishi anaonyesha jinsi jamii ya Kiziba ilivyokuwa inaamini kutokana na maajabu yanayotokea katika jamii mfano Mtoto wa Malikia alivyotangulia kuota meno ya juu, waliamini kuwa  ile ni ishara ya  kutokea kwa balaa badae; Pia kuna maigizo ya matambiko ambako familia ya Mfalme iliamua kutambikia baada ya kuona mwanao ameanza kuota meno ya juu wakahisi huu ni mkosi au kisirani katika familia yao kwa mfano katika ukurasa wa 47 ubeti wa 439 mwandishi anasema;  
            439       Sala wakazitongoa
                        Tambiko wakazitoa
                        Zipate kuwafikia
                        Miungu  wenye afua.
Aidha uigizaji   uliendelea katika mambo mengine yanatokea katika jamii kama vile unywaji wa pombe (ulevi) ambapo inaoeshwa kuwa jamii ilikua inakunywa pombe ili kupunguza mawazo au kusahau maswaibu yanayowakumba  na wakati mwingine kuongeza ujasiri wa kutenda jambo fulani kwa mfano katika  ukurasa wa  409 na 412 anaonyesha akina Nyakiiru  na Kanyamaishwa  walivyokuwa wanakunywa pombe mpaka  wanalewa kisha wanachukua silaha zao wanaenda mawindoni.                                                             
            409       Wote wamekwishalewa                         
                        Na hawakujitambuwa
                         Mutalala  kazidiwa
                        Wengine  kuwapitia.
Maigizo mengine ya sherehe ambako tunaona familia ya mfalme ilikuwa inasherekea kuzaliwa kwa mtoto wa Malkia. Haya tunayaona katika ukurasa wa 9 ubeti wa 75 na 76 wanajamii wakihamasishwa kusherekea kwa kupita ngomezi (la mgambo).
              75     Likipigwa la mgambo                 76   “Malkia   mtukufu
                       Likilia lina jambo                               Kazaa mwana nadhifu
                    “Ikuluni kuna mambo                           Mwingine hafui dafu
                      Kajifungua malkia                             Kunawiri kazidia.”
Kipengele hiki cha maigizo huwa kinajitokeza sana katika kazi za kifasihi ikiwemo tendi kwa lengo la  kuweka msisitizo wa yale matukio yanayotendeka  katika jamii na kuleta uhalisia aidha wakati mwingine kuifanya jamii iamini kuwa matukio hayo yapo na bado yanatokea katika jamii na kujifunza kupitia matukio hayo. Hivyo kuwepo kwa kipengele hicho kinawakilisha mwingilianomatini katika tendi.
Semi
Semi  ni  tungo  au  kauli  fupifupi  za  kisanaa  zenye  kubeba  maana  au  mafunzo muhimu  ya  kijamii.  Semi  zinajumuisha  tanzu  kama  vile  methali,  vitendawili, mafumbo,  misimu,  lakabu  na  kauli-tauria  (Mulokozi,  1996). Fasili  hii ya Mulokozi haitofautiani sana na ile ya M’Ngaruti  (2008) anayesema kuwa  semi ni  tungo  au  kauli  fupi  za  kisanaa  zinazobeba  maana  au  mafunzo ya kijamii. Katika tendi watunzi wengi huingiza semi mbalimbali kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii fulani au wakati mwingine hutumika katika kuonya au kukataza jambo na kutoa tahadhari. Katika utenzi huu pia tunaona mwandishi ameingiza semi mbalimbali kama tunavyoziona katika  kurasa zifuatazo 35, 37, 38, 48, 58  na 68. Semi hizo ni kama zifuatazo;
Ø  Misuli ya dume  katika ukurasa wa  35 ubeti wa 307.
Ø  Usiku wa kiza  katika ukurasa wa 35 ubeti wa 310.
Ø  Wakata nguu na nyanda katika ukurasa wa 36 ubeti wa 320.
Ø  Giza ni mama wa nuru katika ukurasa wa 37  ubeti wa 331.
Ø  Uongozi si udhuru katika ukurasa wa 37 ubeti wa 333.
Ø  Penye mamba pana mto katika ukurasa wa 38 ubeti wa 345.
Ø  Penye moshi pana moto katika ukurasa wa 38 ubeti wa 345.
Ø  Maisha yangu ni yako katika ukurasa wa 58 ubeti wa 554.
Ø  Adui zako ni zetu katika ukurasa wa 68 ubeti wa 648.
Hizo ni baadhi ya semi ambazo zimejitokeza katika utenzi huu, hii ni dhahiri kuwa semi hizi hutumiwa katika kazi za kifasihi kwa lengo la kutoa ujumbe fulani, kuhamasisha suala fulani, kulinganisha vitu fulani na kutahadharisha jambo fulani. Mbali na hayo baadhi ya semi hukusudia kuleta mtiririko wa matukio utakaounganisha sehemu katika visa vyao.
Matumizi ya Nahau
Katika utenzi huu pia matumizi ya nahau nayo yamejitokeza, ambako ni moja ya sifa za tanzu nyingine zilizoingizwa katika tendi. Nahau  ni moja ya semi ambazo zina mafumbo ndani yake na zina lengo la kutoa ujumbe filani kwa njia ya kutumia maneno mengine tofauti na kitu kinachozungumziwa. Hivyo jamii hutumia nahau kwa lengo la kukosoa au kuelezea kitu au sifa na tabia za mtu kwa namna ya tofauti. Mara nyingi si rahisi kuweza kutambua maana ya hizo nahau kama miongoni mwa wanajamii wanaotumia nahau hizo. Hivyo wakati mwingine huwa ni vigumu  kupata maana zake kwa haraka. Katika tendi nahau nazo zinatumika katika kukamilisha maudhui na kuongeza sifa za wahusika waliotumika. Miongoni mwa nahau hizo tunaziona katika kurasa na beti mbalimbali kwa mfano “Kaingia kwa mabavu” katika ukurasa wa 6 ubeti wa 60, “Mashavu yamemtuna” katika ukurasa wa 34 ubeti wa 297, “Damu inatuchemka” katika ukurasa wa 34 ubeti  wa 303, “kukata maini, kubwaga moyo, kumtia mtu simanzi”, “ana mguu mmoja” katika ukurasa wa 4 ubeti wa 33, “jicho lake ni jua” katika ukurasa wa 24 ubeti wa 17, “sauti yake ni radi” katika ukurasa wa 2 ubeti wa 27. Nahau hizi zimebeba mengi ndani yake ambayo yanalenga kufikisha ujumbe kwa jamii na pia zinasaidia kuweza kutambua muonekano wa kitu fulani  na kufikirisha jamii.
Matumizi ya vilio na vicheko
Halikadhalika katika katika tendi huwa kuna maswaibu mbalimbali ambayo huibua hisia kwa wahusika ambazo zaweza kuwa za furaha au huzuni  na kupelekea vilio au vicheko. Vicheko huwa vinaweza kuashiria mambo mengi katika jamii kama yafuatayo: furaha, kebehi au kejeli, mzaha au dharau. Kwa upande wa vilio navyo vyaweza kuashiria furaha, huzuni au majonzi, matatizo au mikosi, maumivu, uchungu na hasira. Katika utenzi huu vilio na vicheko vimetumika kwa mfano katika ukurasa wa 18, 20, 23, 25 na 34. Katika ubeti  wa 34 ukurasa wa 820 mwandishi anaonesha vijakazi walivyokua wanalia Mukama alipouwawa.
                        820  Nao vijakazihao
                               Wakatoka mbiombio
                               Wakalia “Yoo! Yoo!
                               Mukama  wamemuua!”
Hivyo vilio na vicheko navyo vinadhihirisha kuwepo kwa mtindo wa mwingilianomatini katika tendi  na dhima nyingi kwa jamii kama vile kuonyesha hali aliyo nayo mtu kutokana na jambo fulani lililompata mfano furaha au huzuni na kadhalika.
Matumizi ya Taharuki
Taharuki ni ile hali ya kutamani kujua kuwa tukio fulani au jambo fulani linaishiaje au nini hatima yake. Ni hali ya kutaka kujua nini kitakachofuatia au kitakachotokea baada ya tukio fulani kuisha.Watunzi wengi wa kazi za kifasihi huunda kazi zao kwa kuingiza matukio yanayopelekea taharuki kwa hadhira. Hii huongezea ari kwa hadhira ya kutaka kujua ni nini kitakachofwatia mwishoni na kufwatilia kwa umakini mkubwa kisa au hadithi nzima. Haya yamejidhihirisha katika utenzi huu pale Malkia anataharuki ni nini kitakachofwatia baada ya kuona mwanae kaanza kuota meno ya juu. Kwa mfano katika ukurasa wa 17 ubeti wa 153, 154 na 155. Hivyo tendi nyingi za Kiswahili huusisha matumizi ya taharuki; hii huleta hamu ya kuendelea kufwatilia hatima ya kisa fulani.
Matumizi ya Majigambo au Vivugo
Hizi ni ghani za kujisifia. Kwa kawaida hutungwa na kughanwa na mhusika mwenyewe. Kivugo hutungwa kwa ufundi mkubwa, kwa kutumia mbinu kama sitiari, vidokezi, ishara, takiriri na wakati mwingine hata vina ( Mulokozi 1996:81). Mara nyingi hufanywa na wanaume yakifungamana na tukio maalumu katika maisha yake, kwa mfano kuingia vitani, kupambana na maadui kama vile wanyama wakali, kushinda jambo na kadhalika. Kipengele hiki halikadhalika hakijaachwa nyuma kwani katika tendi lazima pawepo na matukio mengi ya kishujaa waliyoyafanya watu na hivyo hujigamba mbele za watu kudhihirisha ushujaa wao, kwa mfano katika ukurasa wa 6 ubeti wa 57  hadi wa 61, 68, 75, 76, 109, 386 hadi 390, na 639 hadi 641. Katika beti hizi zote mtunzi ameonesha majigambo mbalimbali yaliyokua yanafanywa na wahusika, mfano ubeti wa 396 na 397 Nyakiiru na Kanyamaishwa wanajigamba mbele ya Sultani.
                       
                        396     “Ni vyema kuyasikia                        397    “Nimezoea vita
                                    Maneno ya ushujaa                                    Hupiga bila kusita
                                    Mimi pia nakwambia                                  Kazi yangu ni kuteta
                                    Si mzembe kwa kuua.                               Mateto nina yajua.

                       
Ngomezi
Baadhi ya makabila huweza kupeleka habari kwa njia ya ngoma. Midundo fulani ya ngoma huwakilisha kauli fulani katika lugha ya kabila hilo. Mara nyingi kauli hizo huwa ni za kishairi au kimafumbo (Mulokozi 1996:87). Anaendelea kusema kuwa hii ni fasihi simulizi inayowasilishwa kwa kutumia mlio wa ngoma badala ya mdomo; tunaziweka katika kundi la fasihi simulizi  kwa vile ishara za ngoma zinazotumika huiga misemo, tamathali na viimbo vya usemaji wa lugha inayohusika. Halikadhalika ngoma imetumika katika utenzi huu ambako mtunzi anaonyesha katika ukurasa wa 19 amechora picha ya mtu akipiga ngoma kwa lengo la kutoa taarifa mbalimbali za kijamii kwa mfano kuzaliwa kwa mtoto wa Malkia, Kichwankizi ilitumika kutoa taarifa  kwa wanakijiji wa Saza kuwa Nyakiiru atadhuru kijijini hapo, pia ilitumika kuashiria jambo au tukio fulani, kwa mfano katika ukurasa wa 56 ubeti wa 528 ngoma ilipigwa kuashira kuwa Nyakiiru ametawala. Hii bado ni ushahidi kuwa tendi za Kiswahili zina kaida ya kuwa na sifa za tanzu nyingine ndani yake.
Mianzo na miishio ya kifomula
Huu ni mtindo maalumu ambao hutumika sana katika usimuliaji wa kisa fulani ambapo fanani na hadhira  wengi  hutumia katika kuanza na kumalizia kusimulia kisa. Mtindo huu hutumiwa kwa lengo la kutaka kuvuta usikivu kwa hadhira, umakini na kuwajulisha kuwa huo ndiyo mwanzo wa usimulizi wa kisa fulani; au ndiyo mwisho wa hadithi au kisa kinachoelezewa. Mianzo hiyo yaweza kuanza hivi; hapo zamani za kale, paukwa.., Siku moja.. pia huwa na miisho maalumu, kwa mfano, Wakaishi kwa raha mustarehe au hadithi yangu imeishia hapo… Katika utenzi huu mianzo na miisho hiyo ya kifomula imejitokeza katika ukurasa wa 6 ubeti wa 55 anaanza hivi; “ Huko zama za zamani mwa… Na katika ukurasa wa 76 ubeti wa 729 anamalizia hivi; “ Pia tangu siku hio….Matumizi ya kanuni hizi hutusaidia kubaini mwanzo na mwisho wa kisa fulani. Hivi navyo ni miongoni mwa vipengele vinanyojitokeza katika tendi za Kiswahili kama mwingilianomatini.
Hitimisho
Makala  haya  yanahitimisha  kwa  kusisitiza  kuwa tendi za Kiswahili  ni fani ambayo inahitaji  ubunifu  mkubwa wa fanani kulingana na muktadha  husika. Hali  hii  ndiyo  inayofanya  fani  hii  hasa  inapoigusa  hadhira ya tendi kuingiza dhana ya mwingilianomatini. Kama  ilivyokwishaelezwa  hapo  awali kuwa uchanganyaji huu wa matini ni kitu cha kawaida na tendi za Kiswahili zina mwingiliano huo, lakini sababu za uchanganyaji huo zilikuwa bado  hazijabainishwa wazi katika tendi za Kiswahili. Makala yameweza kufafanua dhana ya mwingilianomatini katika tendi za Kiswahili na umuhimu wake kifasihi. Ili kukamilisha malengo  mbalimbali  kisanaa, mwandishi hana budi kuhusisha matini mbalimbali katika kazi yake.

Marejeo
M’Ngaruti.  (2008)  Fasihi  Simulizi  na  Utamaduni. Jomo  Kenyatta
                   Foundation: Nairobi. 
Mulokozi,  M.M.  (1989) “Tanzu za Fasihi Simulizi.” Katika, Mulika.  Na.  21.
                  Dar es Saalaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, kur. 1-24.
Mulokozi, M. M. (1996) Utangulizi  wa Fasihi ya Kiswahili. OSW 105: Fasihi
                  ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Mulokozi, M. M. (1997) Utenzi wa Nyakiiru Kibi. ECOL Publicitions: Morogoro.
Mushengyezi,  A.  (2003) Twentieth  Century  Literary  Theory.  LIT.  224:
                  Literature. Kampala: Makerere University.
Njogu, K. na R. M. Wafula. (2007)  Nadharia  za  Uhakiki  wa  Fasihi.Jomo Kenyatta Foundation:                 
                   Nairobi.
Senkoro, F.E.M.K. (2011) Fasihi: Mfululizo wa Lugha na Fasihi  KAUTTU: Dar es Salaam.
TUKI, 2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TUKI: Dar es Salaam.
Wamitila, K.W. (2006)  Uhakiki  wa  Fasihi:  Misingi  na  Vipengele  Vyake.
                  Phoenix Publishers Ltd: Nairobi.
Wamitila, K.W. (2008) Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Vide-Muwa         
                  Publishers Ltd: Nairobi.   


FANTASIA NA DHIMA YAKE KATIKA TENDI.

Na Charles Timotheo.
Ikisiri
Fasihi simulizi na andishi kwa pamoja huchangia sifa moja ya kuwa sanaa ya lugha katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii husika. Hii ndiyo ithibati ya sanaa yoyote kuwa fasihi. Kama uwasilishaji wa mawazo katika jamii utafanyika bila kutumia lugha kisanaa basi hapo hakuna fasihi. Katika kutumia lugha na mbinu nyingine za kisanaa katika kufikisha ujumbe kwa jamii, wakati mwingine kuna kuvuka mipaka ya uhalisia kwa kuhusisha wahusika na mambo ya kinjozinjozi au fantasia kwa makusudi. Mtindo huu wa kutumia fantasia katika kazi za kifasihi ni kinyume kabisa na wanataaluma wanao amini katika ukweli na uhalisia. Wafuasi wa nadharia ya uhalisia wanadai kuwa mwandishi au msanii wa kazi za fasihi anapaswa kuitoa picha ya jamii bila kuidunisha wala kuipigia chuku. (Wafula na njogu, 2007 wanaeleza hayo). Kwa kuwa fantasia inakimbia ukweli wa uhalisia katika kazi za fasihi je mbinu hiyo ina dhima gani kifasihi? Makala hii yatahusu dhima ya fantasia katika tendi.
Utangulizi
Wamitila (2003) anaeleza kuwa fantasia ni sawa na njozi, njozi ni dhana inayotumiwa kuelezea kazi ya fasihi ambayo ina sifa ambazo zinakiuka uhalisi.Anaendelea kufafanua kuwa ni kazi yenye sifa za kindotondoto au kutaka kuamilisha hali isiyo ya kawaida. Njozi hupatikana sana katika maandishi yanayolenga hadhira ya watoto.Sifa za kinjozi huweza kupatikana katika fasihi inayohusishwa na matapo mbalimbali ya kifasihi.Hutumiwa kueleza kazi za kinathari ambazo huwa na mandhari ya ajabu, matukio magumu kukubalika katika hali ya kawaida na hata wahusika wasioweza kupatikana katika uhalisi. Kutokana na fasili hiyo ya Wamitila tunaweza kusema kuwa wahusika katika kazi zenye fantasia ni wahusika kama vile mazimwi,mashetani ,majini na vitu vingine ambavyo havidhaniwi kuwepo katika jamii, yaani haviwezi kupatikana katika uhalisia .Fantasia nyingi huwa na motifu za zafari, au msako wa utafutaji au ufumbuzi wa kitu falani. Fantasia pi inatumika katika kazi nyingine za kifasihi kama vile riwaya, tamthiliya na hadithi fupi. Kwa mfano riwaya ya marimba ya majaliwa ya E. MBOGO.
Matumizi ya fantasia katika tendi ni suala la kawaida katika tendi. Matumizi ya fantasia yanapojitokeza katika fasihi, huleta upya  ambao unakuwa haujazoeleka na hivyo kuwashutua wahakiki wa fasihi. Mshtuko huu ndio uliozaa istlahi ya uhalisiamazingaombwe kama inavyotumiwa zaidi na Senkoro (2006). Dhana hii inatumika kuzieleza zile kazi za kifasihi zinazounganisha uhalisi na uajabuajabu.
Makala haya yatahusu dhima ya matumizi ya fantasia katika tendi. Hili linatokana na ujitokezaji wa mara kwa mara wa sifa hii katika kazi nyingi za tendi hali ambayo inakiuka uhalisia unaoamini kuwa fasihi ni kioo cha jamii. Fasihi kama kioo cha jamii inapaswa kuakisi kile kinachotokea bila kukipotosha kwa kuingiza mambo yasiyo halisi. Kwa kuwa mbinu hii ya kifani inajitokeza katika kazi nyingi za tendi hasa zile za visasili, makala haya yatatumia kisasili kimoja cha kidini kutoka katika maandiko matakatifu yaani Biblia katika Agano la kale katika kitabu cha Waamuzi. Kisasili hicho ni Kisasili cha Samson. Kwa kuwa makala haya ni ya kitendi basi tuangalie kwa ufupi maana ya tendi kama inavyofasiliwa na wataalamu mbalimbali.
Maana ya tendi
Wataalamu mbalimbali wameelezea dhana ya utendi, miongoni mwao ni Wamitila (2003), anaeleza utendi ni shairi refu la kisimulizi linalozungumzia kwa mapana mtindo wa hali ya juu  matendo ya mashujaa au shujaa mmoja. Kimsingi utendi huwa na sifa nyingi na huweza kuleta pamoja hadithi ya kishujaa, mugani, visasili, historia pamoja na ndoto za taifa Fulani. Wamitila  anaendelea kusema kwamba kuna aina mbili za tendi ambazo ni tendi zinazohusisha fasihi simulizi na tendi zafasihi andishi. Pia anasema tendi ni tungo ndefu ambazo huimbwa na mafundi fulani na huwahusu mashujaa, walioishi katika jamii fulani. Nyimbo hizi zinagusia maisha ya mashujaa hao, kuzaliwa kwao, kuishi kwao, shida zao, vita, matendo yao ya kishujaa na vifo vyao.
Mulokozi (1996), anaeleza kuwa utendi (epic) ni utanzu mashuhuri sana katika kundi la ghani-masimulizi. Utendi ni ushairi wa matendo ni tungo mrefu wenye kusimulia matukio ya kishujaa yenye uzito wa kijamii au kitaifa. Matukio huweza kuwa ya kihistoria na visakale/ visasili.
Kutokana na maelezo hayo, Wamitila na Mulokozi wanaelekea kufanana katika kufafanua dhana ya tendi, wote wanazungumzia juu ya ushairi mrefu unaoelezea matendo ya mashujaa yenye uzito kijamii na wanaeleza kuwa tendi huweza kuwa historia au visasili. Hivyo kutokana na maelezo hayo tunaona kuwa tunaweza kupata tendi katika umbo la visasili ambapo huwa na matukio yamhusuyo shujaa yaani maisha yake kwa ujumla na matendo ya kishujaa anayoyafanya, kisasili cha Samsoni kinakidhi sifa hii hivyo inadhihirisha kuwa ni tendi ingawa matini, maudhui yake na vipengele vyake vimeegemea katika umbo la kisasili
Sifa za tendi (epic)
Tunaweza kuainisha sifa za tendi kwa kifupi kama ifuatavyo;
Tendi zina dhima mbalimbali. Dhima hizi zaweza kuwa za kutunza historia, kutunza  lugha, kuelimisha, dhima za kijamii na hata kuburudisha. Wakati mwingine tendi huwa na dhima ya kuhamasisha na kutambulisha jamii. Mulokozi anakubaliana na tendi kuwa na kazi nyingi na msingi wa tendi kuwa na kazi hizo unatofautiana kati ya jamii na jamii.
Sifa ya urefu, ama kuhusu suala la urefu ni suala linalobadilikabadilika. Hivyo kile kinachoitwa kirefu katika tendi sio ile  hadithi au simulizi la utendi bali ule urefu wa utendaji, hii ni kwa mujibu wa Mulokozi 1996.
Sifa zinazohusu maudhui, katika sifa hii kuna maudhui  yanayohusu shujaa, matatizo, maisha yake, au masuala  jamii anamoishi shujaa husika.
Muhtasari wa kisasili teule na fantsia inavyojitokeza
 Kisasili cha Samsoni
Hiki ni kisasili kinachotoka katika Biblia, Agano la kale kitabu cha Waamuzi sura ya 13-16. Kisa kilieleza kuzaliwa kwa shujaa Samsoni hadi kufa kwake. Kisasili kilianza kwa kueleza jinsi Manoa ambaye alikuwa akiishi na mkewe aliyekuwa tasa yaani alikuwa hana uwezo wa kuzaa mtoto. Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke na kumweleza kuwa atachukua mimba naya atazaa mtoto mwanamume hivyo alikatazwa asitumie vileo wala divai kwani huyo mtoto atakuwa mnadhiri wa Mungu pia alikatazwa asimnyoe nywele hata siku moja. Basi mwanamke alimweleza mumewe na baadaye Manoa alimwomba Mungu amwelekeze namna ya kumlea huyo mtoto. Kisa kinaendelea kutueleza juu ya yule malaika kwani alitokea tena na kuwaelekeza cha kufanya na mwishowe mtoto mwanamume alizaliwa na kupewa jina la Samsoni.
Mtoto akakua na Bwana akam’barikia Samsoni. Muda wa kuoa ulipowadia Samsoni alienda kuoa mwanamake wa Timna mojawapo wa binti wakifilisti na wakati huo Israeli walikuwa wanatawaliwa na Wafilisti. Wakati Samsoni alipokuwa anaenda Timna alikutana na simba lakini alimuua kwa mikono yake mwenyewe kwa kumpasua kama mwanambuzi. Basi kisasili hiki kinaendelea kutueleza mambo yaliyokuwa ya ajabu ajabu yenye nguvu za ziada kama vile kuwaua wanaume thelathini na kuzitwaa nyara zao ili kuwapa wale ambao walitegua kitendawili chake. Aliweza kuwakamata mbweha mia tatu na kuwafunga wawili wawili vienge kisha kuwasha moto na kuwaachia na waliweza kuteketeza mashamba ya ngano na mizeituni ya Wafilisti.
Kisa hiki pia kinaeleza anguko la shujaa huyu aliyeweza kunaswa na Delila mwanamke kahaba  wakifilisti aliyeweza kumshawishi amjulishe siri ya nguvu zake na baada ya upelelezi mwingi shujaa huyu alijikuta akimweleza kuwa tangu kuzaliwa wembe hukupita kichwani mwake na ndipo Delila alipomnyoa nywele zake zote na Wafilisti waliweza kumkamata nakumng’oa macho yake mawili.
Siku ya kifo chake ilikuwa ni sherehe ya Wafilisti ya kumshukuru mungu wao Dagoni kwa kuwawezesha kumkamata adui yao Samsoni hivyo walimleta mbele ya wakuu na viongozi mbalimbali pamoja na watu wengi sana. Hapo Samsoni nywele zake zilishaanza kuota hivyo  alishikilia nguzo mbili zilizokuwa zimeshikilia jengo lile nakuanza kuzisukuma na jengo lile lilianguka akafa na watu wengi kuliko aliowahi kuwaua enzi za uhai wake. Mwisho mwandishi anaeleza kuwa Samsoni alikuwa mwamuzi wa taifa la Israeli kwa muda wa miaka 20.
Fantansia zilivyojitokeza katika tendi.
Katika kisasili hiki kuna mambo kadhaaa yanaelezwa ambayo katika ulimwengu hayawezi kutokea bila uwezo wa nguvu za ziada. Zifuatazo ni fantasia zilizojitokeza katika Kisasili cha Samsoni.
Kwanza fantasia ya kwanza ipo katika hali ya kuzaliwa kwa Samsoni au kutabiriwa kuzaliwa kwake. Katika simulizi hii mama yake Samsoni alikuwa Tasa yaani hawezi yaani asiyeweza kuzaa lakini wakati huo huo malaika anamtokea mama yule na kumueleza kuwa atachukua mimba na kumzaa mtoto wa kiume (Amu 13:3-5) “Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akauwambia, Tazama wewe u tasa huzai; lakini utachukua mimba...”
Pili, kitendo cha Samsoni kutonyolewa tangu kuzaliwa kwake ambalo ni agizo alilopewa mama yake na malaika wa bwana, jambo ambalo si la kawaida katika ulimwengu wa kawaida kwani si rahisi kumkuta mtu ambaye hakuwahi kunyolewa tangu kuzaliwa kwake hadi kuwa mtu mzima kabisa kama Samsoni (Amu 13:5) “Kwani tazama utachukua mimba nawe utamzaa mtoto mwanamume na wembe usipite juu ya kichwa chake....”
Pia kitendo cha malaika kumtokea mke wa Manoa.  Mwanamke huyu alitokewa na malaika mara kadhaa kuelezwa kuhusu kuzaliwa na mambo yanayompasa kuyafanya kipindi cha ujauzito wa Samsoni. Hili pia ni jambo ambalo si la kawaida labda linaweza kutokea kwa kufikirika tu, kwa imani na si kwa kulithibititisha hasa kisayansi. Katika (Amu 13:2) “Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke....:”
Fantasia nyingine ni Samsoni kumuua simba kama mbuzi. Hili ni jambo ambalo si la kawaida sana kwani mwandishi ameeleza hili pale Samsoni na wazazi wake walipokuwa wakielekea Timna kwenda kuoa. Samsoni alingurumiwa na simba katika mashamba ya mizabibu na yeye alimpasua kana kwamba anampasua mbuzi na wala hakuwa na kitu chochote mkono mwake. Hili limeoneshwa katika (Amu 14:6) “Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana mbuzi wala hakuwa na kitu chochote mkononi...”
Kitendo cha Samsoni kuwapiga wanaume thelathini. Baada ya kitendawili cha Samsoni kuteguliwa ilimpasa  awalipe wale vijana waliotegua kitendawili chake, hivyo ilim’bidi awapige wanaume thelathini huko Ashkeloni ili achukue nyara na kwenda kulipa. Hili limeoneshwa katika (Amu 14:19) “Roho wa Bwana ikamjilia juu yake kwa nguvu, naye akatelemkia Ashkelani akapiga watu waume thelathini katika watu hao na kuzitwa nyara zao na kuwapa hao.....”
Tukio ligine lisilo la kawaida  ni  Samsoni kuwakamata mbweha mia tatu na kuwafunga vienge katika mikia yao. Hili Samsoni alilifanya baada ya kwenda kwa mke wake na kukuta ameozwa kwa mtu mwingine hivyo aliona hakuna kinachomfanya kumzuia kuwadhuru wafilisti kwani tayari alikuwa ameshanyang’anywa mke. Samsoni aliwakamata mbweha mia tatu  na kuwafunga vienge vya moto katika mikia yao na kisha kuvitia moto na kuwaachia wakimbilie katika mashamba ya ngano na kutekeleza matita na ngano na  mashamba ya mizeituni hili limeoneshwa (Amu 15:4-5).
Pia Samsoni  kuwaua watu elfu wa mfupa wa taya la punda. Watu wa Yuda walimfunga Samsoni kamba ili kumtia mikononi mwa wafilisti, Samsoni alikubali na walipofika kwa wafilisti Samsoni alizikata zile kamba mbili mpya alizofungwa nazo kama kitani iliyoteketezwa kwa moto  na hapo ndipo alipochukua mfupa mbichi wa taya ya panda, akawapiga watu elfu kwa mfupa huo (Amu 15:14-15).
Samsoni kuzikata kamba saba mbichi alizofungwa nazo. Delila alikuwa akimpeleleza Samson kuhusu asili ya Nguvu zake hivyo Samsoni akamwambia wakinifunga kamba mbichi saba ambazo hazijakauka bado hapo ndipo nitakuwa dhaifu. Basi Delila akaletewa kamba mbichi saba na kumfunga nazo Samsoni  mwandishi anasema Samsoni alizikata kama vile uzi wa pamba ukatavyo ukiguswa na moto. Katika (AMU 16:9) “Na yule mwanamke... Ndipo akazikata zile kamba kama vile uzi wa pamba ukatavyo ukiguswa na moto, basi hiyo asili ya Nguvu zake haukujulikana.”
Fantasia nyingine ni  Kuangusha Nyumba kubwa kwa kushikilia nguzo mbili kubwa zilizokuwa katika nyumba ile. Hili lilikuwa ni jambo la mwisho Samsoni kulifanya katika uhai wake kabla ya kifo chake ambacho ndio lilikuwa anguko lake. Baada ya Wafilisti kumtesa sana nywele zake zilianza kuota na alipoitwa kwenda kucheza alizishika nguzo za ile nyumba iliyokuwa na watu wengi waume kwa wake, wakuu wote wa Wajilisti na kuiangusha kitu kilichosababisha kifo chake na cha wote waliokuwamo ndani.
Hivyo basi tunaweza kusema kwamba mambo hayo hapo juu yanaweza kutokea katika ulimwengu wa kufikirika tu, katika ulimwengu wa kiuhalisia hayapo na wala hayawezi kuthibitishwa kisayansi.
Dhima ya Fantansia katika Tendi
Baada ya kuangalia muhtasari wa kisasili cha Samsoni pamoja na fantansia inavyojitokeza basi  tuangalie sababu za kuwepo kwa fantasia hizo. Kwa kuwa mambo hayo ya kindotondoto si halisi je yaepukwe? Tunapojibu swali hilo ndio tunapata sababu za waandishi kutumia fantasia na mchango wa mbinu hiyo kifasihi. Dhima kuu za fantasia katika tendi ni pamoja na;
                    
Kumwibua  na kumwonyesho kwa uwazi mhusika Shujaa.
Hii ni mojawapo ya dhima kuu ya matumizi ya fantansia katika tendi. Mara nyingi mhusika shujaa wa kitendi ni lazima awe na ruwaza fulani ya maisha ambayo kwa asilimia kubwa au karibia maisha yake yote yanajawa na mambo ya kinjozinjozi au kindotondoto. Wataalamu wengine husema anatumia nguvu za sihiri. Mara nyingi mhusika shujaa wa kitendi kuzaliwa kwake huwa ni kwa ajabuajabu na pengine hukataliwa na jamii yake. Lakini kukua kwake na mambo anayoyapitia huwa ni ya ajabuajabu na hiyo ndiyo fantansia yenyewe. Mfano katika kisasili cha Samsoni. Samsoni anazaliwa na mama tasa aliyetokewa na malaika lakini katika kukua kwake Samsoni hakuwahi kunyolewa nywele na zaidi alifanya mambo ya ajabuajabu. Mfano katika katika aya 14:6.

Kujenga msuko wa matukio katika Tendi.
Mohamed (1995) anauita msuko huu ni Ploti. Anaifafanua ploti kuwa ni msukumo wa hadithi katika mpangilio fulani. Anazidi kufafanua kuwa msukumo huu hujengwa na wahusika wanaotenda na kutendana na kuathiriana kusababisha matukio, mwendo na kasi ya kwenda kiwakati na pahala. Ufafanuzi huu unafanana na ule wa Wamitila (2011) unaodai kuwa msuko ni mpangilio wa matukio katika kazi ya kifashi.
Hivyo basi dhima mojawapo ya kutumia fantansia katika tendi ni hiyo ya kuibua matukio ili kufanikisha msuko. Katika kisa cha Samsoni kuzaliwa kwake kule kwa ajabuajabu na kutokunyolewa kwake nywele kumesaidia kusukuma mbele na kufanikisha usimulizi wa kisasili hiki. Mwandishi anaeleza kuwa Samsoni alizaliwa na mwanamke tasa ambaye alitokewa na malaika wa bwana na pia sio tu kuzaliwa bali anaeleza kuwa hakuwahi kunyolewa mpaka Delila alipoamua kumpeleleza na kujua siri hiyo na kumnyoa jambo lililosababisha kuishiwa nguvu. Kuwepo kwa nguvu za Ajabu za Samsoni iliwezesha simulizi nzima kunoga na kuzua taharuki nyingi katika sura mbalimbali. Aidha kisasili hiki matukio yake yote kwa kiasi kikubwa yamefanikishwa kwa fantansia mbalimbali hasa ya nguvu za ajabu za Samsoni.

Kujenga Taharuki kwa wasomaji au wasikilizaji.
Madumulla (2009) anamueleza msanii mzuri kuwa ni yule anayepanga kazi yake kiasi kwamba tukio moja linasababisha lingine na kusababisha kujenga hamu msomaji ya kutaka kujua kulikoni, nini kitatokea hii ndiyo huitwa taharuki. Matumizi ya fantasia katika tendi inasaidia sana kujenga taharuki na hii humfanya msomaji atake kujua zaidi kujua nini kinaendelea katika simulizi baada ya tukio fulani. Mfano katika kisasili cha Samsoni Delila anampeleleza Samsoni kuhusu asili ya nguvu zake basi Samsoni anamueleza mara ya kwanza kitu kinachomfanya msomaji anakuwa na hamu ya kujua ni nini kitatokea baada ya kutoa siri na hivyo hivyo kwa mara ya pili na tatu na hata mara ya mwisho alipotoa siri yake lazima mtu ajiulize hivi itakuwaje je atakufa? Hivyo fantansia husaidia msomaji kupata hamu ya kuendelea kujua kitakachotokea na kufanya kazi ivutie zaidi.

Kuibua dhamira mbalimbali kwani kila fantasia ina maudhui fulani.
Dhamira huweza kuibuliwa kwa kupitia fantansia mbalimbali zinazojitokeza katika tendi. Masuala kadhaa huibuliwa kupitia mambo ya kiajabuajabu yanayojitokeza. Katika kisasili hiki cha Samsoni dhamira nyingi zimeibuliwa katika matumizi ya fantansia, mfano siri ya Samsoni kuwa na nguvu nyingi inaweza kuwa na dhamira mbalimbali kama vile, kujua kutunza siri, kwani Samsoni alimwambia Delila siri yake na hivyo kusababisha kuanguka kwake, pia dhamira ya kuwa msaada kwa taifa lako, kupambana na adui na pia kuacha uonevu kwa wengine kama ambavyo Wafilisti walivyokuwa wanawapiga na kuwatawala  waisraeli.
Lakini pia agizo alilotoa malaika kwa wazazi wa Samsoni la kutokumnyoa nywele nalo pia huibua dhamira ya kuwa tunapaswa kuwa watiifu tunapopewa maagizo na wakubwa zetu kwani wazazi wa Samsoni hawakumnyoa na walitii maagizo yote.

Mgogoro husaidia sana kumvutia msomaji kutaka kujua ni nini hatima ya mgogoro fulani kitu ambacho huipa uzito kazi ya fasihi, na matumizi ya fantansia kwa ujumla yanasaidia sana katika ujenzi wa migogoro ya kiusimulizi.

Kutimiza matamanio ya Binadamu
Kupitia matumizi ya fantansia, mambo yote hata yale yasiyowezekana kwa binadamu huwezekana, hii ni kutokana na kuwa binadamu ana uwezo wa kufanya mambo mengi sana katika ulimwengu wa kihalisia, kwa upande mwingine, yapo mambo mengine ambayo binadamu hutamani kufanya lakini hana uwezo nayo. Mambo yale yanayobanwa na mikatale ya kijamii  huwezekana kuyasema kupitia kazi za kifasihi kupitia fantansia.
Sigmund Frend katika nadharia yake ya Saiko-changanuzi anaifananisha kazi ya fasihi na ndoto, anasema kazi za fasihi ni kazi za ubunifu, kazi hizi ni sawa na ndoto tu ya mtunzi. Hata wahusika wanaopatikana ni wanadamu wanaoishi katika ndoto na njozi za mwandishi (Wafula na Njogu, 2007).
Hivyo matumizi ya fantansia huonesha matamanio ya mtunzi mfano katika kisa cha Samsoni. Suala la Wafilisti kuwatawala Waisraeli mwandishi alikuwa anatamani kulipinga kupitia mambo mbalimbali ya kiajabuajabu, pia kufanya mambo makubwa na yanayohitaji nguvu kwa urahisi mfano. Kumuua simba kirahisi jambo ambalo kwa kawaida ni gumu lakini pia kuangusha nyumba kubwa kwa urahisi nyumba iliyokuwa imara na yenye nguzo mbili. Hivyo kwa kutumia fantansia mtunzi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza matamanio yake.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema makala hii inasisitiza kuwa fantasia ni mbinu muhimu katika kazi za kitendi kwani huwa na mchango/dhima nyingi katika kazi hizi ambayo kwa kiasi kikubwa husaidia kukidhi sifa za kazi fulani kuwa tendi na fasihi kwa ujumla. Kutokana na uwepo wa fantasia nyingi katika kazi mbalimbali za fasihi bado waandishi na wahakiki wanapaswa kufanya utafiti zaidi juu ya umuhimu wa fantasia katika kazi za fasihi.
                                                            
Marejeo
Madummulla, J. S (2009). Riwaya ya Kiswahili; Nadharia, Historia, na Misingi ya Uchambuzi.
                            Dar es Salaam: Mture Educational Publishers Limited.
Mohamed, S. A (1995), Kunga za Nathari ya Kiswahili; Riwaya, Tamthilia na Hadithi Fupi,
                            Nairobi; English Press Limited.
Mulokozi, M. M (1996), Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili,Dar es Salaam; Chuo kikuu Huria.
Njogu, K na R. M. Wafula (2007), Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyata
                              Foundation.
Senkoro, F.E.M.K (2006) Fasihi. Dar es salaam: Kauttu
The Bible Societies of Kenya and Tanzania (1997) Biblia; Maandiko Matakatifu. Kenya na  
                              Tanzania.
Wamitila. K.W (2003), Kamusi ya fasihi; Istilahi na Nadharia. Nairobi. Focus publication Ltd.
Wamitila K. W. (2011) Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Nairobi English press.
                                    


FASIHI LINGANISHI NA TAFSIRI
TIMOTHEO  CHARLES
 UTANGULIZI.
Makala hii inalenga kueleza juu ya suala zima la tafsiri na mchango wake katika kukuza fasihi linganishi ya Kiswahili. Makala hii itaanza kwa kueleza maana ya fasihi linganishi na maana ya tafsiri kama ilivyofafanuliwa na wataalamu mbalimbali. Baada ya tafsiri hizo makala hii itaendelea kuchambua tafsiri katika fasihi linganishi  ya Kiswahili mkazo ukitiliwa zaidi mchango wa tafsiri na kuonyesha kuwa tafsiri ni nyenzo muhimu katika kukuza fasihi. Data hizi zitaonyesha jina la kazi husika, jina la mfasiri, wakati au kipindi ambacho kazi hiyo imefasiriwa na lugha iliyotumika kufanya tafsiri. Pia makala hii itaonyesha utanzu ulioingiza kazi za fasihi za kigeni kwa njia ya tafsiri, utanzu unaokabiliwa na changamoto nyingi wakati wa kutafsiri na namna ya kukabiliana na changamoto hizo. Sehemu inayofuata ya makala hii itaonyesha kwa kina utanzu mmoja kati ya zilizopo kwenye jedwali kama kielelezo cha kueleza ama tafsiri ni mbovu au ni bora katika kazi za fasihi na kisha utafuata uchambuzi wa kazi mojawapo ya fasihi msisitizo ukiwa hasa kwenye mchango wa tafsiri katika fasihi linganishi ya Kiswahili pamoja na changamoto zitokanazo na mchakato wa tafsiri katika kufasiri matini za kifasihi.
Tukianza na maana ya fasihi linganishi na maana ya tafsiri kama zilivyoelezwa na wataalamu mbalimbali. Maana ya fasihi linganishi,
Wamitila (2003) anaeleza kuwa fasihi linganishi  inahusu uchambuzi wa maandishi ya wakati mmoja na aina moja na katika lugha mbalimbali kwa  nia ya kumiliki sifa zinazoyahusisha  kama athari, vyanzo, sifa zinazofanana na tofauti za kiutamaduni. Anaendelea kueleza kuwa inawezekana kufanya hivi kwa nia ya kuangalia matapo mbalimbali, maendeleo au hata nadharia za kiuhakiki. Fasihi ya namna hii iliweka misingi na juhudi za wanaisimu kuanza kuilinganisha lugha mbalimbali katika karne ya kumi na tisa. Hivyo tunaweza kusema kuwa faasihi linganishi inajikita zaidi kutumia mbinu za kiulinganishi baina ya kazi mbili za kifasihi ili kujua sifa fulani fulani kama vile kufanana kwa kazi hizo, tofauti za kiutamaduni katika kazi hizo, kujua ulinganishi katika lugha yaani sarufi ya lugha katika kazi hizo za kifasihi.
Baada ya kueleza maana ya fasihi linganishi kwa kifupi ufuatao ni ufafanuzi wa tafsiri kama ulivyoelezwa na wataalamu mbalimbali.  
Kwa mujibu wa Mwansoko na wenzake (2006) wanaeleza kuwa tafsiri ni zoezi la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi nyingine. Woa wanatilia mkazo katika zoezi la uhawilishaji na kinachohawilishwa ni mawazo katika maandishi. Pia wakimnukuu Catford (1965) yeye anaeleza kuwa kufasiri ni kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha mmoja yaani lugha chanzi na kuweka badala yake mawazo yanayolingana kutoka katika lugha nyingine yaani lugha lengwa. Hapa msisitizo upo katika matini zilizoandikwa na kuzingatia zaidi ujumbe au wazo lililopo katika matini chanzi lijitokeze vile vile katika matini lengwa. Mawazo haya hayawezi kuwa sawa kabisa na ya matini chanzi bali ni mawazo yanayolingana toka matini chanzi na matini lengwa, hii ni kutokana na sababu tofauti kama vile utamaduni, historia, kiisimu na mazingira.
Naye Newmark (1982) anaeleza kuwa tafsiri ni mchakato wa uhawilishaji wa maneno kutoka matini chanzi kwenda matini lengwa.
Pia Nida na Taber (1969) wanaeleza kuwa tafsiri hujumuisha kuzalisha upya ujumbe wa lugha chanzi kwa kutumia visawe vya asili vya lugha lengwa vinavyo karibiana zaidi na lugha chanzi kimaana na kimtindo. Wao wanatilia mkazo uzalishaji upya wa kwa kutumia visawe asili vinavyokaribiana na matini chanzi kimaana na kimtindo. Kutokana na maana hizi tunaweza kusema kuwa tafsiri hufanywa katika ujumbe uliopo katika maandishi, ni jaribio la kiuhawilishaji, na wazo linalatafsiriwa huwa na visawe vinavyokaribiana na sio sawa kutokana na tofauti za kiisimu, kihistoria, kiutamaduni na mazingira.
Kwa kiasi kikubwa tafsiri ni nyenzo muhimu sana ya kukuza fasihi ya Kiswahili kwani husaidia katika ukuzaji wa msamiati. Kwa mfano katika makala ya G. Ruhumbika katika Makala za semina ya kimataifa ya waandishi wa Kiswahili (ii) anaeleza kwa upande wa lugha ya Kingereza inasemekana maneno mapya 12000 yaliingizwa miaka 1500 na 1650. Mfano huu unajidhihirisha hata lugha ya Kiswahili kuna maneno ambayo yameingizwa kutoka lugha za kigeni ambayo ni ya kawaida kwa sasa na yanatumika mfano neno data, drama, thieta na kathalika.
Pia tafsiri husaidia jamii lengwa kujifunza utamaduni wa jamii chazi ambapo tunaweza kujifunza mwenendo bora wa kiutamaduni, kihistoria, kiuchumi na kijamii.
Tafsiri husaidia kuchambua viepengele na mbinu za matini chanzi kama vile mtindo, muundo ujenzi wa wahusika na mandhari. Kwani tukizingatia kazi za kifasihi lazima ziwe na uwezo wa kuathiri na kuathiriwa kwa baadhi ya vipengele vya kazi zingine. Hivyo tafsiri ni nyenzo ya mawasiliano ambapo ujumbe wa lugha chanzi huwafikia jamii lengwa wakapata itikadi, tamaduni na histiria za jamii chanzi.
MAPITIO YA KAZI ZA FASIHI YA KISWAHILI ZILIZOTAFSIRIWA.

NA
JINA LA KAZI
UTANZU WAKE
JINA LA MFASIRI
KIPINDI
LUGHA ILIYOFASIRIWA

1.
Sundiata
Tamthiliya
E. Mbogo
2011
Kingereza - Kiswahili.

2.
Safari za Guiliver
Hadithi fupi
Genesis press  Kiswahili
2010
Kingereza - Kiswahili.

3.
Bwana Myombokere na Bwana bugonyoka
Riwaya
Aniceti Kitereza
1980
Kikerewe - Kiswahili

4.
Wimbo wa lawino
Ushairi
Paul Sozigwa
1975
Kingereza - Kiswahili.

5.
Mabepari wa venisi
Tamthiliya
Mwl. J.K.Nyerere
1969
Kingereza - Kiswahili

6.
Juliasi kaizari
Tamthiliya
Mwl. J. K. Nyerere
1964
Kingereza - Kiswahili.

7.
Hekaya za abuniasi
Hadithi fupi
S. Chiponde
1928
Kingereza - Kiswahili

8.
Alfu lela ulela. Kitabu 4.
Hadithi fupi.
Edwin W. Brenn
1994
Kingereza - Kiswahili

9.
Nitaolewa nikipenda
Tamthiliya
C.M. Kabugi
2010
Kingereza - Kiswahili

10.
Barua  ndefu kama hii
Riwaya
C. Mganga
1994
Kingereza - Kiswahili.

11.
Mfalme edpod
Tamthiliya
S.S. Mushi
1971
Kingereza - Kiswahili

12.
Wema hawajazaliwa
Riwaya
Abdilatif Abdallah
1976
Kingereza - Kiswahili.

13.
Mtawa mweusi
Tamthiliya
EAEP LTD
2008
Kingereza - Kiswahili.

14.
Aliyeonja pepo
Tamthiliya
Maritin Mkombo
1980
Kiswahili - Kingereza.

15.
Alfu lela ulela. Kitabu 2.
Hadithi fupi
Hassan Adam
2004
Kijerumani -Kiswahili.

16.
Makbeth
Tamthiliya
S.S. Mushi
1969
Kingereza -Kiswahiki.

17.
Mchuuzi muungwana
Tamthiliya
A. Morrises
1961
Kingereza - Kiswahili.

18.
Kisima chenye hazina
Hadithi fupi
F. Jameson
1928
Kingereza - Kiswahili

19.
Robinson crusoe
Hadithi fupi
Genesis press Kiswahili
2010
Kingereza - Kiswahili.

20.
Masaibu ya ndugu jero
Tamthiliya
A .S. Yahya 
1974
Kingereza - Kiswahili
21.
Mkaguzi mkuu wa serikali
Tamthiliya
C. Mwakasaka
1979
Kingereza - Kiswahili.
22.
Mnafiki
Tamhiliya
L. Taguaba
1973
Kingereza - Kiswahili.
23.
Orodha
Tamthiliya
Said, D. Kiango
2006
Kingereza - Kiswahili.
24.
Shujaa okonkwo
Riwaya
EAPH
1973
Kingereza - Kiswahili.
25.
Uhuru wa watumwa
Riwaya
Thomas Nelson

Kingereza - Kiswahili.










Utanzu ulioingiza zaidi fasihi ya kigeni ni tamthiliya. Hii ni kwa sababu tamthiliya na muundo wake ni zao toka Ulaya. Hapa Afrika tulikuwa na sanaa za maonyesho tu baada ya ujio wa wakoloni ndio tamthiliya zikaingizwa Afrika kwa lengo la kuchekesha. Baadhi ya wataalamu kama vile Mulokozi (1996) anaeleza kuwa Afrika kulikuwa na sanaa za maonyesho. Anasema tamthiliya asili yake ni huko Ulaya ambapo zilitokana na miviga na viviga na ziliathiri sana sanaa za maonyesho baada ya kuingia Afrika. Kutokana na maeleza haya tunaweza kusema kuwa ujio wa tamthiliya umeathiri sanaa za maonyesho za jadi. Hivyo utanzu ulioingiza fasihi ya kigeni ni tamthiliya kwani hata muundo wake ni wamagharibi. Hapa Afrika tamthiliya zilitafsiriwa kwa lengo la kuigizwa. (Mwansoko na wenzake 2006).
Lugha ambazo zimejitokeza zaidi kufanikisha suala la tafsiri ni Kingereza, Kiswahili, Kijerumani na Kikerewe. Lugha iliyojitokeza sana ni Kingereza zaidi ya Kijerumani na Kikerewe kama nilivyozionyesha katika jedwali.
Utanzu unaokabiliwa na changamoto na nyingi wakati wa kufasiri ni ushairi. Baadhi ya wataalamu kama vile Mwansoko na wenzake (2006; 43) wakimnukuu Newmark (1988) wanaeleza wazi kuwa ushairi ndio utanzu mgumu zaidi kufasiri katika fasihi. Sababu ya ugumu huu ni ushairi umebinafsishwa sana na una mshindilio mkubwa wa mawazo. Wanaeleza kuwa katika ushairi kizio cha kwanza cha maana ni neno kinachofuatia ni mstari. Mstari ni dhana yenye maana zaidi katika ushairi kuliko katika tanzu nyingine. Kwa maelezo haya tunaweza kueleza changamoto za ushairi ni kama vile ushairi umesheheni sitiari, tamathali za semi, umbo lenye mpangilio maalumu, sheria za mashairi ya kimapokeo kama vile vina, mizani na mishororo. Vipengele hivi ni vigumu hasa katika kuvitafutia visawe vyake. Ili kutatua tatizo hili lazima mfasiri azingatie vipengele vyote na awe na uweledi wa taaluma husika ya fasihi.
Katika uchambuzi kwa kutumia kitabu cha “Black hermit” kilichoandikwa na Ngugi wa Thiong’o (1968) na kutafsiriwa kama “Mtawa mweusi” na EAEP ltd (2008). Katika    kutathmini ama tafsiri ni bora au ni mbovu Newmark (1988) anapendekeza mbinu au njia zinazotumika katika kutathmini. Mbinu hizo ni mbinu ya ulinganishi kati ya matini chanzi na matini lengwa, mbinu ya uasili, mbinu ya kupima uelewa, mbinu ya kupima usomaji, mbinu ya kupima ulinganifu na mbinu ya tathmini rejeshi. Katika makala hii nitatumia mbinu ya ulinganishi kata ya matini chanzi na matini lengwa. Katika kutumia mbinu hii nitazingatia vipengele vya; sarufi, muundo, upotoshaji wa maana kwa kuzingatia udondoshaji, uongezaji, ufafanuzi wa ziada pamoja na uteuzi mbaya wa visawe (msamiati). Tofauti hizi husababishwa na sababu za kiisimu, kiutamaduni, kihistoria na kimazingira. Tukianza na;
Sarufi; katika kipengele hiki tunazingatia suala la upatanisho wa kisarufi. Ni jukumu la mfasiri kuhakikisha kwamba anazingatia na kuhifadhi upatanisho wa kisarufi kati ya matini chanzi na lengwa. Lakini wakati mwingine kipengele hiki hakitekelezeki. Mfano wafasiri wa tamthiliya ya “Black Hermit” iliyotafsiriwa kama “Mtawa Mweusi” hawajazingatia upatanisho wa kisarufi na kufanya matini ya tafsiri ipoteze ubora wake na hivyo kuwa mbovu.

Mfano: Matini chanzi:  sorting out beans spread  in a basin. (uk. 1)

             Matini lengwa:  akichagua harage katika bakuli. (uk. 1)

             Matini chanzi: if this be a curse put upon me (uk. 4)

            Matin lengwa: kama hili ndilo laana nililopewa (uk. 4)

            Matini chanzi: away from influence af tribal elders (uk. 43)

            Matini lengwa: atengwe na maongozi ya wazee wa kabila (uk. 65)
Katika matini Kiingereza sentensi ipo sawa lakini mfasiri anapotosha upatanisho wa Kisarufi kwa kutumia “harage” badala ya “maharage”. Katika sentensi ya pili ya Kiingereza “if this be a curse put upon me” limetafsiriwa kama “kama hili ndilo laana nililopewa”badala ya “kama hii ndio laana” tungo hizi zimefanya kukosekana kwa upatanisho wa kisarufi katika matini lengwa na katika sentensi ya tatu neno “maongozi” linapaswa kuwa “uongozi”.
Muundo; huu ni mpangilio wa kazi husika ya fasihi. Katika tamthiliya ya “black hermit” mtunzi ametumia muundo sahihi wa tamthiliya kwa kufuata mkondo wa kiaristito naa majina ya wahisika yapo mwanzoni na kufuatwa na maelezo ya wahusika au vitendo. Lakini wafasiri wa “mtawa mweusi” wamekiuka kabisa muundo uliopo kwenye matini chanzi hivyo kusababisha tafsiri kuwa tenge. Wafasiri wametumia muundo wa filamu ambapo majina ya wahusika yanakaa katikati na kufuatwa na maelezo au vitendo.
Upotoshaji wa maana; jukumu lingine la mfasiri anatakiwa azingatie maana ile ile ya mwandishi. Lakini wakati mwingine wafasiri hawazingatii hili. Baadhi ya sababu zinazo sababisha upotoshaji wa maana katika tamthilia ya “black hermit” ni pamoja na;
Udondoshaji; hapa mfasiri huacha baadhi ya vipengele vilivyopo katika matini chanzi kwenye matini lengwa. Kwa mfano;

                               Matini chanzi; forced community work.

                               Matini lengwa; kazi za kulazimishwa.

                                    Matini chanzi:  This temptation harping on weak flesh (uk4)

                             Matini lengwa; Jaribu hili linalirudia rudia mwili wangu (uk.5)


                              Matini chanzi; ask me to ……… to …………., Oh, Oh.   (uk. 33)

                              Matini lengwa; kaniambia ni …… ni…………….       (uk. 49)

Katika mifano hii kuna baadhi ya maneno ya yaliyoachwa yaani hayajafasiriwa kama vile “community”, “weak”na “oh, oh”.
Uongeza; hapa katika kipengele hiki mfasiri anaweza kuongeza vionjo na madoido ambayo hayakwepo katika matini chanzi hadi kufikia kiwango cha kupotosha maana. Kwa mfano katika tafsiri (zao) “mtawa mweusi” mtafsiri ameongeza baadhi ya maneno; mfano;

                       Matini chanzi ; opens in a street corner   (uk. 18)

                       Matini lengwa ; lilianzia mahali fulani mjini    (uk. 24)

                       Matni chanzi; can’t you se             

                       Matini lengwa; wewe mwenyewe huoni

                       Matini chanzi; ooo my mother wept              

                       Matini lengwa; ooo mama yangu aliangusha kilio

                       Matini chanzi; you insist?       (Uk. 38)

                       Matini lengwa; anaendelea kushikilia uzi   (uk. 56)

 

Uteuzi mbaya wa msamiati; Katika suala la hili yawezekana mfasiri akachagua maana isiyo sahihi kati ya maana nyingi zilizo katika lugha lengwa za neno katika lugha chanzi. Kwa mfano;

                Matini chanzi:                                         Matini lengwa

               … in a basin (uk.1)                               …katika bakuli  (uk.1)

                 …carrying    (uk. 1)                             …akichukua  (uk.1)
 
                  Do without husband                                siwezi kuishi bila mwanaume

                   I have tasted the pains of beating             nimeona maumivu ya mapigo.
Katika tafsiri ya Kiswahili neno la kiingeraza “basin” limefasiriwa kama “bakuli” badala ya “beseni”, neno “carrying” limetafsiriwa kama “akichukua” badala ya “akibeba”, neno “do” limetafsiwa kama “kuishi” badala ya “kufanya”, neno “tasted” limetafsiriwa kama “nimeona” badala ya “nimeonja” na kauli ya mwishi inatakiwa kuwa “kuliko hii”. Uteuzi wa msamiati katika matini legwa umepotosha maana iliyokusudiwa na mwandishi wa matini chanzi.
                      Mchango wa tafsiri katika fasihi linganishi ni pamoja na huu ufuatao;
Tafsiri inatusaidia kulinganishi utamaduni wa jamii moja na nyingine. Mfano mzuri ambazo inatuelezea utamaduni wa kabila la Marua lililopo Kenya katika suala la desturi zao ambalo mume akifariki mke anarithiwa na kaka mtu au mdogo mtu. (uk.38). Mila na desturi hizi hapo awali katika jamii za waafrika hususani hapa nchini katika familia mke akifa alirithiwa. Lakini suala hili kwa sasa jamii imeliacha kwa kiasi Fulani kutokana na maendeleo ya elimu.
Tafsiri inatusaidia kulinganisha itikadi za jamii za Kiafrika. Kupitia  kabila la Marua waafika walikuwa na mtazamo hasi wa kutochanganyikana na wala kutokuoana wala kuolewa na wazungu kutokana na wazungu kuwatawala kipindi cha ukoloni. Hali hii inadhibitishwa na maongezi ya Remi (uk. 52). Lakini kwa upande wa wazungu wao wanaitikadi chanya kwa waafrika. Wanaamini kuwa mapenzi hayajalishi rangi wala kabila bali watu kupendana. Haya yanathibitishwa na maongezi ya Jane. (uk.53). Baada ya uhuru waafrika wengi wakuwa na mitazamo hasi kwa wazungu kutokana na matendo ukoloni.
Tafsiri inatusadia kulinganisha historia ya jamii katika vipindi tofauti. Kwa mfano jamii ya  Marua kipindi ukoloni matatizo yalivyokuwa tofauti na  yale ya uhuru. Hivyo historia hii inatudhihirishia hata katika jamii zetu matatizo yaliyoletwa na ukoloni yalikuwa tofauti na yale ya uhuru.
Changamoto katika kufasiri zinajitokeza katika mambo yafuatayo;
Kwanza kutokuwa na ujuzi wa lugha na sarufi inayohusika. Ni jukumu la mfasiri kujua vizuri lugha anazozishughulikia kiundani zaidi ikiwa ni pamoja na sarufi sahihi, miundo, mitindo nakadhalika. Kama mfasiri hajui basi husababiasha upotofu wa tafsiri na umbovu.
Kutokuwa na taaluma ya uwanjwa maalumu. Wafasiri wengi wanafasiri pasipo kuangalia taaluma zao mahususi. Kwa mfano mtaalamu wa isimu anafasiri matini za kifasihi lazima kwa hali yoyote atasababisha utenge wa tafsiri.
Kutokuwa na vifaa vya kukuwezesha kutoa tafsiri nzuri na bora. Vifaa kama vile kamusi za matini mahususi katika taaluma mahususi husababisha ugumu wa kupata visawe husika.
Tafauti za kiutamaduni, itikadi, mazingira na historia husababisha changamoto kubwa katika tafsiri.
Pia tofauti za kiisimu na maendeleo ya sayansi na tekinolojia yanasababisha changamoto kubwa katika tafsiri mathilani sayansi na tekinolojia huleta istilahi ambazo ni vigumu kuzipatia istilahi zake.
Naweza kuhitimisha kwa kusema kuwa ingawa tafsiri ni nyenzo muhimu sana katika kukuza fasihi ya Kiswahili kuna baadhi ya upotoshaji wa ujumbe uliokusudiwa kutafsiriwa kutokana na mambo kadhaa kama vile itikadi ya mfasiri, historia, utamaduni na mazingira aliyopo mafasiri.

Marejeo

           East African Educational Publishers Ltd (2008) Mtawa Mweusi. Kenya: Sitima Printers  

                          Stationers Ltd.

          Mulokozi, M. M (1996) Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu

                     Huria.

          Mwansoko, H.J.M. na wenzake (2006) Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu.

                    Dar es Salaam: TUKI.

         Newmark, P. (1982) Approaches to Translation. Oxford: Pergamon.

         Newmark, P. (1988) A Textbook of Translaton. London: Prentice Hall.

          Ngugi wa Thing’o (1968) Black Hermit. Kampala-Uganda: East African       Educational                            

                           Publishers Stationers Ltd

      Nida, A. E. na Charles, R. T. (1969) The Theory and Practice of Translation. Netherlands:

                     EJ. Brill.

        Ruhumbika, G. (1978) “Tafsiri za Kigeni katika Ukuzaji wa Fasihi ya Kiswahili” Makala

                    kwenye Semina za Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili Dar es Salaam.

         Wamitila, K. W. (2003) Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publication.






CHIMBUKO LA USHAIRI.

Katika makala hii tutajadili kwa kina kuhusu chimbuko la ushahiri wa Kiswahili kwa kutumia nadharia mbili kama kiunzi cha uchambuzi huu. Kabla ya kueleza chimbuko la Kiswahili ni vyema tukaeleza nini maana ya ushairi. Dhana ya ushairi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo:

Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi  ya kuwa na sanaa ya vina ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari wa maneno.
Mnyampala anasema kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora sana katika maongozo ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.”
Amri Abeid (1954:1) anasema kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana.”
Wataalamu wengine wanaeleza kuwa ushairi ni kauli zenye hisia na ubunifu, mpangilio fulani wenye urari, uwasilishaji wa tajiriba au mawazo ya mtunzi kwa maana ambayo huibua tajiriba kama hiyo katika nyayo za wasomaji au wasikilizaji na kutumia lugha ya picha yenye wizani wa sauti.
Mulokozi na Kahigi (1982) wanasema ushairi ni “sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalum na fasaha na wenye muwala, kwa lugha ya picha, sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kuleta wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisia fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.”
Hivyo basi kutokana na fasili za wataalamu mbalimbali  tunaweza kusema kuwa ushairi ni kazi ya sanaa yenye kuandikwa au kuimbwa kwa kufuata kanuni za ushairi au kutofuata kanuni za ushairi. Hii ina maana kwamba ushairi waweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa ilimradi ushairi huo uwe na ujumbe unaogusa hisi za wasomaji au wasikilizaji.
Baada ya kuana maana ya ushairi pia dhana ya chimbuko inafasiliwa na TUKI (2004) kuwa ni mwazo au asili ya kitu.
Baadhi ya wataalamu wameweza kuelezea chimbuko la ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia mitazamo au nadharia mbili ambazo ni kama zifuatazo:
Nadharia ya kwanza inadai kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu.
Na nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la jamii ya waswahili wenyewe.
(1)   CHIMBUKO LA USHAIRI NI UJIO WA WAARABU
Nadharia hii ya kwanza isemayo kuwa chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu ambayo inaungwa mkono na wataalam mbalimbali kama vile Lyndon Harries (1962) na Knappet (1979)
Kwa mujibu wa Lyndon (1962) “Swahili Poetry” anatoa hoja tatu ambazo kwa yeye zinadhibitisha kuwa ushairi wa Kiswahili umetokana na uarabu. Hoja hizo ni ushairi wa Kiswahili umetokana na Uislamu, ushairi ulianzia kwenye upwa wa kaskazini mwa Kenya hususani Lamu. Na maudhui ya ushairi wa Kiswahili yalitokana na ushairi wa Kiarabu. Utungo wa kwanza wa ushairi andishi wa Kiswahili ni Tambuka, Mwengo bin Athmani (1728)
Kutokana na nadharia hii ubora wake ni kwamba nadharia hii au mtazamo wa Harries kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni kwamba umesaidia wengine kuendelea kuchunguza zaidi kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili.
Lakini nadharia hii ina udhaifu kwani si kweli kwamba ushairi wa Kiswahili uliletwa na Uislamu bali ulikuwepo hata kabla ya ujio wa Uislamu, kwani ushairi hautenganishwi na jamii husika. Hivyo jamii za waswahili walitumia nyanja mbalimbali za ushairi katika shughuli zao mbalimbali au shughuli zao za kila siku, kama vile; shughuli za kilimo na ufugaji.
Pia ushairi wa Kiswahili ulianza karne ya 10BK na ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kughanwa kwa ghibu bila kuandikwa. Wataalam wengi wanakubaliana kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo.
Pia udhaifu mwingine katika mtazamo wake wa kusema kuwa ushairi ulianzia pwani ya kaskazini ya Kenya si kweli kwa kuwa waswahili walikuwepo hata sehemu nyingine kama vile Kilwa na Bagamoyo ambapo ushairi wa Kiswahili ulitumika.
Hivyo tunaweza kusema kuwa hoja ya kusema ushairi wa Kiswahili ulitokana na Kiarabu haina mashiko kwa kuwa waswahili walikuwepo hata kabla ya waarabu na walikuwa na ushairi wao isipokuwa ujio wao ulileta athari kubwa kwa kuwa ulichanganya na mambo ya dini ya kiislamu pamoja na hati.
Naye Knappert (1979) “Four centuries of Swahili verse” anasema; “Ushairi wa Kiswahili ulichipuka kwenye upwa wa Kenya kutokana na nyimbo na ngoma za waswahili na ulianza katika karne ya 17 na pia ni ushairi wa Kiislamu wenye kuchanganya sifa za tungo za kiafrika na za kiajemi.
Mkabala huu una ubora kwani  Knappert amekubali kuwa, ushairi wa Kiswahili ulitokana na waswahili wenyewe.
Hata hivyo hoja yake ina udhaifu kidogo kwani  ushairi wa Kiswahili ulianza kabla ya karne ya 10 BK na pia amejikita katika maudhui ya mambo mengine kama vile siasa, uchumi na kijamii. Vilevile amechanganya chimbuko la ushairi wa Kiswahili na Uarabu.

(2)   USHAIRI NI ZAO LA WASWAHILI WENYEWE
Nadharia hii ya pili inasema kuwa ushairi ni zao la waswahili wenyewe. Nadharia hii imejadiliwa na wataalamu mbalimbali akiwemo Shaban Robert, Jumanne Mayoka (1993) na F.E.M.K. Senkoro, Mulokozi na Sengo.
Kwa mujibu wa Mayoka (1993) anasema ushairi umetokana na jamii ya wanadamu wenyewe na umesheheneza ukwasi mkubwa wa lugha ambayo imekuwa ikitumika katika hatua zote za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika historia ambayo mwanadamu amepitia, Kwa mfano kuwa msamiati uliotumika tangu enzi za kuishi mapangoni, enzi za uwindaji, ujima, utumwa, vita vya makabila, uvamizi wa wageni, ukoloni na harakati za kupambana na ukoloni hadi kupata uhuru na maendeleo yake.
Kwa mujibu wa nadharia hii tunaweza kupata ubora wa nadharia. Ubora wa hoja hii ni kwamba, kila jamii ina sanaa yake na ushairi ni moja kati ya sanaa hizo ingawa inaweza ikaathiriwa na sanaa ya jamii nyingine. Pia ushairi umekuwa ukikua na kuendelea kadri jamii inavyokuwa na kuendelea.
Ingawa upo ubora lakini kuna mapungufu kadhaa. Udhaifu wa hoja hii ni kwamba si kweli kuwa katika kipindi hicho ushairi ulikuwa tayari umesheheni ukwasi mkubwa wa lugha, na kama ulikuwa kweli umesheheni huu ukwasi wa lugha alipaswa kutuonesha huo utajiri wa lugha anaouzungumzia katika ushairi.
Senkoro (1988) anasema kuwa ushairi uliibuka pale lugha ilipoanza katika kipindi cha uhayawani (kipindi ambacho mwanadamu alipoanza kupambana na mazingira yake) kwenda katika kipindi cha urazini (maana) ili kumwezesha binadamu na mazingira yake kwa mfano, zana za kazi zilizotumika ziliwafanya waimbe kwa kufuata mdundo wa zana hizo.
Hoja hii inathibitisha kuwa chimbuko la ushairi ni waswahili wenyewe, kwani umefanikiwa kueleza kuwa katika jamii yoyote ile maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii huambatana au huenda sambamba na maendeleo ya sanaa mbalimbali ikiwemo ushairi uliotumika katika harakati mbalimbali za maisha ya mwanadamu.
Pamoja na kuwa nadharia hii imeonesha kukubalika na wataalamu mbalimbali kama vile Senkoro, Mayoka na Shekhe Amri Abeid, lakini bado ina mapungufu. Hii ni kwa sababu imeshindwa kuonesha muda maalumu ambapo ushairi wa Kiswahili ulianza na ni wapi ulianza kutumika. Hili ni suala ambalo linahitaji uchunguzi wa kina ili kulibaini.
Hivyo basi, kutokana  na nadharia hizo mbili tunaungana na nadharia inayosema kuwa, chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la waswahili wenyewe, kwa sababu waswahili wana utamaduni wao ambao ulikuwepo kabla ya ujio wa Waarabu. Na waliutumia ushairi huo katika shughuli mbalimbali za kijamii, kwa mfano katika harusi, jando na unyago.

MAREJEO:
        Knappert, J. (1979). Four centuries of Swahili Verse. Heinemann. London.
        Mayoka, J.K. (1993). Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka. Ndanda Mission                                                   

                            Press.Tanzania.
         Mulokozi, M.M. (1996). Fasihi ya Kiswahili.Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.                                                               
 Dar-es-Salaam.
          Senkoro, F.E.M.K. (1987). Ushairi, Nadharia na Tahakiki. DUP. Dar-es-Salaam.
         TUKI. (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu.TUKI.Dar-es-Salaam.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni